-->

KAMA UNAPITIA MAUMIVU YA MAPENZI HEBU SOMA HII

Image result for mapenzi wakubwa

Dada/kaka
Kuna wakati mgumu unaupitia wenye maumivu makali huku ukijiuliza maswali mengi. Dalili zote zinaonyesha umefika mwisho na kila unapogeuka haupati msaada wowote.
.
Ulipofika unajiona huna thamani tena na hutaweza kuinuka tena na hakuna faida ya kuishi tena hapa duniani. Unapofakari unaona hakuna ubishi kuwa sio rahisi kwako kuinuka tena. Masikini we!! Unajiuliza maswali na kutoa majibi mwenyewe. Kama ni kulia umelia sana mpaka machozi yamekauka. Umeomba na kumlilia sana Mungu na hakuna mabadiliko yeyote.

MPENDWA WANGU, UNAPOFIKIA HALI HII KUMBUKA YAFUATAYO:
.
1) KAMWE usijaribu kufikiri kuwa MUNGU amekuacha na hakujali tena. Usijilaumu kwa kuwa Mwenyezi Mungu Bado anakuwazia mema. Badala ya kulaumu endelea kumuamini kwani hutoa siku na saa aliyopanga yeye.
.
2) Unapokuwa kwenye hali hii jipe moyo kwa kuwa na hili nalo utashinda. Kumbuka nyakati tofauti ulizopitia ambazo hatma yake ulivuka. HIVYO NA HILI NALO UTASHINDA na itabakia kuwa historia.
.
3) Jambo moja kubwa unalopaswa kuliepuka ni kujifungia ndani peke yako na kujitenga na wengine. Unapojitenga yapo mawazo yanayokuambia na kujiona kuwa kila mtu hayuko tayari kukusaidia. Mawazo haya yanaweza kukufanya umchukie kila anayepita mbele yako na kumuona kuwa adui yako.

Mwenyezi Mungu bado anao watu wanaokuthamini, wanaokupenda, wanaokuwazia mema na wako tayari kukusaidia wakati wote wa shida na raha pamoja na kwamba wapo wengi wanaoonekana kukutenga na hawapo tayari kukusaidia.

DAIMA KUMBUKA KUWA WAPO WANAOKUTHAMINI na WATASIMAMA daima na wewe. Mpendwa wangu kama upo kwenye hali hii, nakushauri toka ndani ili ukutane na watu wema walioandaliwa wakutane nawe ambao watakushika mkono na kukuondoa katika dimbwi kubwa la mawazo mabaya.

Wanasaikolojia wanasema kwamba MTU aliyekata tamaa anapojitenga ndani basi ni rahisi kufikia maamuzi mabaya ya kujiua. Kwanini ufike huko mpendwa wangu?? KUBALI KUWA NA HILI NALO LITAPITA.
Share:

Related Posts:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © 2025 UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU