-->

UNAWEZA UKAWA KWENYE MAHUSIANO AU NDOA NA BADO UKAWA MPWEKE!


Image may contain: one or more people, people standing, ocean, sky, outdoor and nature
Ni kweli si kila alie na mahusiano ni mpweke, Kuna watu wako kwenye ndoa ila ni wapweke na kuna wakati wanatamani hata kuondoka kwenye ndoa zao, licha ya kuwa na wenza wao lakini wako watu wanaishi na majuto kila siku juu ya mahusiano waliyopo, Japokuwa mara kadhaa tunalinganisha kuwa UPEKEE na kuwa MPWEKE ni kama Kuna maana moja, hivi viwili havifanani kwa uhalisia lakini kuna vinasaba vya matamshi, Kuwa PEKE YAKO siku zote inamaanisha huzuni, lakini haimanishi unahisi kuchukia upekee wako ama kujitenga au kutojichanganya... Kwahiyo tunaweza kuwa pekee na si wapweke, au tunaweza kuwa pekee na wapweke yote yanaweza kushahabiana kutokana na mazingira, Kuwa bila mwenza/pekee na si mpweke kinaweza kuwa kitu kikubwa Kwani upweke unajengwa na upekee, Lakini bila kuwa na mwenza na mpweke kunaweza kuzalisha matatizo ambayo yataletwa na akili, Unapokuwa hauna mwenza ila si mpweke, ni rahisi kupuuzia misukumo ya nje inayozunguka kuoa/kuolewa na kufurahia kuwa bila mwenza, Lakini unapokuwa hauna mwenza na mpweke ni ngumu zaidi kukaa pembeni ya misukumo ya kuwa jinsi wengine wanavyotarajia jinsi walivyo, Ni rahisi kukubali hivyo ndivyo ulivyo kutokana na kuikubali hali uliyopo, Je UPEKEE unaweza kukutenga na UPWEKE? Majibu ni mepesi sana Hakuna namna ya kukwepa UPWEKE kwa sababu moja tu MAPENZI NI MAISHA! Usiudanganye moyo wako kwamba unaweza kuishi bila MAPENZI bali unatakiwa uujenge MOYO wako kwamba MAPENZI NI MAISHA ili uweze kuendana na Mahusiano utakayokuwepo, Ni magumu ama mazuri lakini tayari ni MAPENZI...
#Elista_kasema_ila_sio_sheria.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU