Wanaume wanapokuwa wanatafuta mchumba, amemuona dada fulani akampenda yani atamuonyesha upendo wa hali ya juu, care za kutosha na kumchukulia, kumwelewa na kujitahidi kumfurahisha kila wakati. Yaani kipindi cha uchumba mdada anakuwa kama malkia vile, yani anajiona yupo dunia ya watu wawili, anatamani siku zifike wafunge ndoa ili waishi paradiso ya duniani.
Cha kusikitisha wanaume wengi wakishaoa wanajisahau, wanasahau kama mke bado ni yule binti waliyemchumbia, wanasahau kama mke anahitaji kujaliwa, kusikilizwa, care, romance na mengine kama hayo ili ndoa izidi kustawi. Tena akipata watoto ndio kabisaa, anaishi kama baba fulani, hata kwa mkewe anataka aonekane ndiye mwenye kauli ya mwisho, mkewe habembelezwi tena, kila kitu ni amri, amri tu. Ndoa inakosa msisimko na kubakia tu watu wanaohishi pamoja na kuheshimiana ila intimacy hakuna.
Kuna ugumu gani kuendelea kufanya yale uliyokuwa unayafanya kwa mkeo wakati wa uchumba? Kwanini siku hizi akisema au kutenda jambo usilolitaka unachukulia ni dharau wakatu mwanzoni ulikuwa unajaribu kuelewa sababu. Mke anahitaji kuona mume wake anakwenda extra mile kumfurahisha, na kumuonyesha upendo, wakati mwingine anaplay hard to get ili mume aweze kutumia ujuzi wake romantically kumpata ma sio kumkoromea na kumnunia.
SHARE