Ni nadara sana kukutana na mtu ambaye hajawahi kuwa na mtu, wapo wanaokutana nao lakini wengi wetu tunatoka kwa wtau, kwa kifupi mapenzi ni kunyang’anyana. Wanaume mara nyingi wakiachwa huendelea na amisah yao, wanakua si watu wa kuomboleza muda mrefu, lakini pia kuna wale wanaume amabao wametoka kuachwa ile haswaa. Yaani kuachana na mwanamke amabye walimpenda sana, labda alikua ni mpenzi amabye kamsomesha, kamfanyia kila kitu lakini mwisho akaja kumuacha.
Alikua ni mke, anamhudumia kila kitu, anamjali lakini akaja kuachwa au ni mpenzi tu hakua anamhudumia lakini aliachwa na baad aya kuachwa akawa kama mtu aliyechanganyikiwa. Kwa maana kuwa katoka kuachana na mpenzi wake, wakati mwingine hata si kwamba kaachwa lakini ni mwanamke wake alimfanyia kitu kibaya akaamua kumuacha, akawa hana namna akamuacha.
Au hata wakati mwingine mwanaume ndiyo alikosea lakini akiamini kuwa mwanamke atamsamehe, kwamba mwanzo alizoea kila akikosea anasamehewa ila wmanamke akmuacha na hajarudi. Iwe vyovyote vile lakini kama unakutana na mwanaume, katoka kuachana ila wakati wa kauchana aliumia sana, akawa kama kachanganyikiwa, kila mkiongea kidogo unakuta ni lazima kumtaja X wake, anamtaja hata kama ni kwa mabaya lakini lazima amtaje.
Kua makini sana na wanaume wa namna hii kwani mara nyingi wanakua hawajapona. Anakutumia ili kumsahau X wake, hapo kuna mawili, kwanza anaweza kumsahau halafu akipona akagundua kuwa alifanya makosa kuwa na wewe hivyoa akakuacha, pili anaweza aasikuache lakinia simsahau X wake, kwmaba hata akakuoa lakini kila wakati akaw anamkumbuka, kila ukifanya kosa anamtaja, ukifanya kitu kizuri anamtaja, yaani kila kitu katika mahusiano yenu ikawa ni huyo x wake tu.
Ukaswa unashindana na X wake au ukaw anaye lakini X akitaka kurudi basi ukaachwa au ukawa kama umeachwa. Kwa maana hiyo, unapokutana na mwanaume wa namna hii, mwanaume ambaye badoa hajamsahau X wake, kama kila dakika ni X na unaona kama kachanganyikiwa basi jitoe mapema, huwezi kumbadilisha, lakini opili hata kama unataka kuwa naye, jipe muda kabla ya kuingia kwenye ndoa au kubeba mimba yake.
Wengi utakuta kwakua wana maumivu wanataka kulipa kisasi, wanataka kushindana na ma X wako, kuwaonyesha kuwa umeniacha lakini mimi bado ninawez akupata mtu mwingine. Watataka kuzaa au kuoa harakaharaka, unakutana naye, ndiyo katoka kuachwa hata miezi sita badoa nataak kukuoa, hapana rudi nyuma, kuweni na mahusiano ndiyo uingie huko kwani ni rahisi huyo mtu kujutia na kukutelekeza.
Mpe nafasi ya kupona kwanza kabla ya kuja kwako, msome mpaka ujue kuwa hata kama hajakupenda kama yule lakini angalau kamsahau au anaonyesha kukupenda. Ila kuingia kwenye ndoa au mahusiano kwakua tu anakuambia anataka kuoa, kwakua anaonekanma yuko siriasi wakati unaona kabis ana maumivu makubwa basi ni kijipotezea muda, ni kuingia kwneye mahusiano na ndoa ya mateso.