-->

YAMENIKUTA; MALI ZANGU ZILIVYOGEUKA KUWA MALI ZA MAREHEMU!

Wakati namuoa mke wangu nilikua na duka la vyombo, halikua kubwa sana lakini nilikua nikijiona tajiri flani nina uwezo. Mauzo ya laki mbili kwa siku yalikua yakinichanganya, lakini miezi miwili tu baada ya ndoa mke wangu alianza kusema kachoka kukaa nyumbani anataka kufanya kazi. Kusema uikweli nilishajiwekea kuwa siwezi kuoa wmanamke akafanya kazi lakini alipiga kelele sana mpaka nikamruhusu.
Nilimuambia aje tukae naye dukani, alikuja kweli lakini alikaa kwa mwezi mmoja tu akaniambia kuwa Biashara ya vyombo kwa hilo eneo hailipi ni kupoteza muda basi tufungue hardwear kuuza vifaa vya ujenzi kwani hilo eneo dniyo linajengeka. Nilimuona kama mjinga na kuona kama ana tamaa, nilimuambia kama ana pesa yake afungue lakini mimi siwezi kumpa mtaji akaharibu pesa.

Kuna mchezo alikua anacheza hata kabla ya kumuoa na nilikua najua, nakumbuka baada ya kama miezi minne hivi ya ndoa alipokea milioni mbili, aliniambia anafungua hardwear, nilizidi kumuona mjinga kwani niliona kama ni pesa ndogop, nikamuambia wewe hujui Biashara. Lakini hakukata tamaa, alitafuta sehemu akaanza kuuza. Alianza na milioni hizo hizo mbili kama utani, lakini niliona anapanuka.
Biashara yake kubwa alikua anafanya kwa mali kauli. Alikua na mtaji mdogo hivyo hakua na vitu vingi dukani, katika duka lake aliweka kama sample ya vitu mtu akitaka mzigo mkubwa anamuagizia kwa maduka ya jumla anampelekea. Basi baada ya kama mwaka hivi Biashara ilishasimama, alibeba ujauzito, alipoenda kujifungua ilinibidi mimi kubaki na kumsaidia kusimamia duka lake. Hapo ndipo nilijua kuwa mke wanmgu Biashara yake ni kubwa mara mbili kuliko mimi.
Nilishangaa sana kwani mimi nilikua na zaidi ya miaka 10 kwenye Biashara lakini mauzo yangu yalikua hayafiki hata robo ya mauzo ya mke wangu ambaye hakua na hata miaka miwili. Bila kumuambia niliachana na Biashara ya vyombo na kuhamia moja kwa moja pale, aliporudi alikuta ninauza pale, hakulalamika wala kuulizia chochote.
Biashara ilipozidi kuwa kubwa tulitaka kufungua duka la jumla, hapo ndipo nilikutana na rafiki yangu ambaye yeye alikua ni mfanyakazi wa serikali. Alinishauri nimsahawishi mke wangu kuhamisha fremu, ili hiyo fremu niandikishane mkataba mimi na mwenye nyumba na leseni ya Biashara iwe na jina langu. Aliniambia kwa wakati huo kwakua leseni ya Biashara ina jina la mke wangu basi niliacha hivyo hivyo kama ikitoke atukiachana Biashara inakua yake.
Ni kama alinizindua, Biashara ilishakua kubwa ina mtaji zaidi ya milioni mia lakini ilikua na jina la mke wangu. Nilifuatilia fremu kubwa sehemu nzuri na kufuatilia kila kitu, nikamashawishi mke wangu tukahamisha Biashara, kufika kule ndiyo anashanaga kila kitu kina majina yangu. hakulalamika sana kwani bado upendo ulikuepo, Biashara iikua inachanganya, nilitaka kukaa mimi lakini nilikua siiiwezi.
Mke wangu ana mkono wa Biashara, wateja wanmampenda na anajua kuongea na matajiri, anaaminika kirahisi, alikua na uwezo wa kuchukua hata mzigo wa milioni 50 kw amali kauli na akarudisha zote. Niliamua kuwa meneje, nikamuachia mke wangu kila kitu, lakini pesa nilikua nachukua mimi, nafanya mambo ya maendeleo kwa majina yangu. rafiki yangu yuleyule aliniambia kuwa ni ujinga kumuonyesha mke kila kitu.
Kwamba kama mke wangu akijua mali zangu zote, hata kama zina majiha yangu basi tukiachana tunagawana nusu kwa nusu. Alinishauri kufungua Biashara nyingine kimya kimya na kununua viwanja huku nikijenga kimya kimya. Kweli nilimuamini, basi nikawa nachukua pesa siwekezi, nafanya mambo yangu kimya kimya.
Nanunua viwanja najenga bila mke wangu kujua. Mke alipokua akihoji matumizi, kwakua nilikua nachukua pesa dukani labda kununua mzigo, kupeleka Benki lakini mwisho kunakua hakuna kitu. Tulijikuta tunaingia kwenye madani, mke wangu hakuruhusu duka kufa hivyo mara nyingi alikua anachukua vitu kwa mali kauli, lakini kwakua baada ya mauzo pesa nachukua mimi kufanya mambo yangu basi hakua na lesa ya kurejesha.
Alikua na madeni mengi, tulikua tunagombana sana kwanini anakopa, basi akwa hana amani, wakati ana ujauzito wa mtoto wetu wapili mke wangu alikua kama amechanganyikiwa kabisa, lakini mimi sikujali kwani wakatio huo nilishaanzisha mahusiano mengine hivyo nilikua na sehemu ya kupumulia. Alijifungua salama tena kwa shida, lakini hakuweza tena kunyanyuka kibiashara, alikua na madeni mengi na hakua akiaminika tena, watu waliokua wakimkopesha hawakua wanamuamini tena.
Nilimuachia lile duka likiwa na madeni mengi na sikuleta tena mzigo mwingine, mimi tayari nilikua na maduka mengine mawili na nilikua na maisha yangu. kila siku nilikua namlaumu kuwa hana akili, hawezi kutunza pesa na mambo mengine mengine mengi kibao, alikua ni mtu wa mawazo tu na Biashara alikua akifanyia kwaajili ya kulipia madeni. Tuligombana mpaka kufikia hatua nikahama nyumbani na kuhamia kwenye nyumba yangu nyingine ambayo nilijenga kimya kimya bila mke wangu kujua.
Huku nyumbani alipambana lakini hali ilikua mbaya, siku moja nilisikia amekamatwa na kupelekwa mahakamani kwani alikua anadaiwa milioni 120 asmbazo alikopa na kushindwa kulipa. Alikaa mahabusu kwa siku tano, hakua na mtu wa kumuwekea dhamana na mimi nilijifanya kukasirika, nilijitoa kabisa nikajifanya kutokujua kuwa alikua anakopa pesa na kuzipeleka wapi, niliwachukua wanangu na kuwapeleka kwa Mama yangu.
Kila mtu alikua akimlaumu yeye kwani niliwaambia kuwa alikua anakopa peke yake. Ndugu zangu walinishauri nimuache, nimpe talaka kwania taniua kwa madeni.mpresha ilikua kubwa, nilijua nimetoka naye mbali na mali niliz0kua nazo zilitokana na yeye lakini sikutaka kuwa naye, kila nikiwa na mke wangu nilijisikia vibaya, sikuona raha ya kuwa na pesa kwani nilijua kabisa kuwa pesa si zangu kanisaidia yeye.
Baada ya mashinikizo ya watu wengi niliamua kumpa mke wangu talaka, hakuamini kama himemuacha. Pamoja na kuwa nilimtelekeza lakini mke wangua likua akiamini kuwa nitaerudi, mke wangua likua hajuic hochote kuhusiana na mali zangu nyingine, alikua akijua tu kuwa nilikua na matumizi makubwa lakini hakua akijua kama nimejenga nyumba nyingine tatu, nina maduka mawili na Benki nina pesa tu ya kutosha.
Wakati wa kuachana tuligawana nyumba, mimi niliamua kumuachia nyumba kubwa tuliyokua tukiishi na nyingine ambayo haijakamilika nilichukua mimi. Sikutaka kumbana sana kwani nilijua mimi nina maisha yangu. Mambo yote hayo nilikua nikiyafanya kwakushirikiana na rafiki yangu, yeye ndiyo alikua kila kitu kwangu na kweli kwa wakati huo nilijisikia vizuri sana kwani alinisaidia kupata mali nyingi kutoka kwa mke wangu.
Sikuwaza hata kama kanivunjia nfamilia, niliwaza mali. Baada ya kumalizana na talaka nililazimjisha kubaki na watoto ila mke wangu alipambana na kwakua walikua bado wadogo alibaki nao yeye. Niliendekeza Biashara zangu vizuri tu, miezi sita ya kwanza ilikua vizuri, lakini ghafla mambo yakaanza kubadilika, wateja wapo ila si kama zamani, nilisukumana hivyo hivyo mpaka mwaka ukaisha, Biashara bado ni ngumu mwisho nikalazimika kufunga duka moja.
Mambo yalizidi kuwa magumu pale ambapo rafiki yangu ambaye alikua ananisaidia na kunipa mawazo alipofariki dunia ghafla kwa ajali ya gari. Nilihangaika kwa miezi sita nikaona kabisa Biashara zinakufa ndipo niliamua kuchukua mkopo Benki nikiwaka dhamana nyumba yangu moja. Lakini nusu niingie jela kwa utapeli kwani hati niliyoenda nayo Benki ilikua ni feki.
Ni hati ambayo merehemu ndiyo alinisaidia kufuatilia, wakati huohuo nataka kuchukua mkopo basi nipo ndugu zake nao wanaibuka. Mke wake analalamika kuwa nataka kumdhulumu mali zake, nilishangaa kwani mali zilikua ni zangu na mke wake alikua hata hazijui, ni mambo tuliyokua tunafanya mimi nayeye tu wote tukiambiana wanawake si watu wa kuamini. Lakini nilikuja kugundua kuwa nyumba moja niliyokua nikiishi ilikua na jina la mke wa marehemu.
Mbili nyingine zilikua na majina ya watoto wake, na viwanja viwili vilikua na majina ya Mama yake. Vyote hivyo ni yeye alinisaidia kutafuta, kwa maana kuwa, Marehemu alinisaidia kutafuta viwanja, akasimamia kupata hati mpaka ujenzi alikua ni yeye. Malalamiko yaliibuka kuwa nimeghushi hati ili kudhulumu mali za marehemu. Kweli nilishangaa kwani kila kitu kilikua ni changu na marehemu alishafariki miezi sita nyuma ila si mke wala ndugu zake walilalamika.
Nilichokuja kugundua ni kuwa, marehemu kumbe hata yeye alikua anaificha familia yake vitu vyake, yaani aliandika vile vitu majina ya mkewe na wanae lakini alikua hajawaambia chochote. Nilipoenda kuchukua mkopo, wakati wa Benki kuhakiki umiliki wa kiwanja ndipo ikagundulika kuwa kumbe si vyangu, kule halmashauri Marehemu alikua na watu anafahamiana nao na ndiyo walimuambia mke wake. Hapo ndipo alifuatilia na kukuta risiti nyingine ambazo marehemua likua akilipia viwanja vyangu kama vyake.
Nilijaribu kujitetea lakini nilionekana mkosaji, kila mtu aliona kama mimi nilitaka kudhulumu mali za marehemu. Kwamba marehamu alikua akiniamini mimi kama rafiki yake kuliko mke wake, akanionyesha vitu vyake ila baada ya yeye kufariki basi badala ya kuiambia familia yake basi mimi nikaghushi hati za viwanja. Nilitaka kufuatilia lakini kila wakili niliyeenda akaniambia kughushi ni kosa la jinai nitafungwa, nililazimika kuachia kila kitu.
Niliondoka mweupe, sina hata kiwanja kimoja kwani kila kitu alikua akinishughulikia marehemu, nilibaki na biasnara tu amabyao nilishashindwa kuiendesha. Mwisho niliifunga ile Biashara na kurudi kuitafuta familia yangu, nilikuta mke wangu naye alilazimika kuuza nyumba ili kulipia madeni, aliiu
Za bei ya hasara akaenda kupangisha. Nilimuomba sana turudiane lakini alikataa, niliendelea kuishi nikiamini kama atarudi.
Mimi bado nilikua na nyumba ambayo mpaka wakai huo nilikua sijaimalizia hivyo nilimuambia nipo tayari kumuachia ili mradi tu nirudiane naye lakini alikataa. Kuchunguza alikua kwenye mahusiano na kijana mmoja na baada ya mimi kuanza kumsumbua walifunga ndoa na sasa wanaishi wote ana duka lake la nguo kimara. Si kubwa kihivyo lakini kwa ninavyomjua mke wangu ni suala la muda tu atafanikiwa, siwazi tena mali ila nawaza jinsi nilivyopoteza mwanamke mzuri kwasababu ya ubinafsi na kutaka mali ambazo hata nikifa nitaziacha.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU