-->

SIMULIZI YAKWELI NAYAKUSISIMUA..


Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa binti kijiji cha jirani mbali na wanapoishi..
Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu!.
Yule kijana Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini MAMA yake pia anampenda. Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mzee mmoja ambae umri umeenda (amekula chumvi nyingi) na mwenye hekima na busara pia.
Kijana Alimwambia yule mzee: Moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?
Yule mzee mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia:
Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na yule mzee. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia mtoto wake bila ya ajizi yoyote.
Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyokunjamana kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?*
Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa kazu hiyo. Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri.
Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumfuata yule mzee mwenye busara huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!?
TUWAPENDE WAZAZI WETU!!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU