-->

UNAIJUWA ATHARI YA UTII WA MWANAMKE?

Image may contain: 2 people, people sitting
Wanaume walio wengi wamekuwa wakiingia kwenye ndoa kwa ajili ya kutengeneza HESHIMA... Mwanaume asiye makini humchukuwa Mwanamke kwa malengo fulani fulani, Wapo wanaume ambao wao humchukuwa Mwanamke kuwa kama MSAIDIZI WAKE yaani atamfulia nguo na kujua nguo gani atavaa mumewe, Wapo ambao wao huoa kwa ajili ya mahitaji ya chakula ama huduma za ki mwili, Shida iko kwenye UTII WA MWANAMKE... Mwanamke kwa maumbile anajijua kwamba yeye yuko chini ya mume, Utii ambao mwanamke anao kwa Mwanaume ni wa ki maumbile wala sio wa sababu, Kadiri mwanamke anavyozidi kutii kwa mume ndivyo ambavyo Mwanaume huchukulia utii ule kuwa kama kilema cha mwanamke, Kila bin adam anahitaji KUTHAMINIWA kwa namna yoyote ile, Mwanaume anapokuwa ameubeba UTII wa mwanamke wake kuwa kama kilema ni dhana ambayo imepitwa na wakati, Mwanaume anapokuwa anapuuza utii wa mkewe na kuendelea kumdhoofisha kwa kudhani ni njia salama katika kumfanya mkewe asiweze kuwa huru kwake HUO NI UKIUKWAJI WA MAPENZI na mwisho wa siku ni mbaya sana, Mwanamke kwa kuzaliwa ni kiumbe kinachohitaji USALAMA WA NAFSI kuliko hata wa mwili, Maana katika maisha ya UTII wa mwanamke ndani yake anapata Elimu ya jinsi gani mwanaume asivyopenda kupewa utii, Mwisho wa siku Mwanamke huondoka kwenye ile hali ya UTII na kuwa VUGUVUGU... Na hapo ndipo matatizo kwenye Mahusiano ama ndoa hiyo huanza, Ikumbukwe kwamba UTII wa mwanamke huyo Mume aliuchukulia kama udhaifu, Wakati huo huo Mwanamke katika kumtii mumewe alijikuta anakata tamaa kwa Kwani pamoja na juhudi nyingi za utii lakini alidharaulika, Mara nyingi MWENYE UVUMILIVU hukinai na mwisho wa siku anakuwa na moyo mgumu, Ukimpenda Mtu mpe mambo makuu matatu;
 UTII
HESHIMA
NIDHAMU
Hapo unaweza kutajwa kwa pendo lenye Heshima, Je Mtu huyo anatambuwa hilo? Liko tatizo kwenye namna ya MTU KUTAMBUWA NA KUELEWA UMUHIMU WA MWENZA WAKE... Kutambuwa ni Busara na Kutotambuwa ni Tabia, Kila aliye na BUSARA hutambuwa na kufanyia kazi hilo alilotambuwa, Mpe MOYO WAKO mtu ambaye anatambuwa umuhimu wako kwani hawezi kukupuuza, Huhitaji akili nyingi kujuwa kama uko na Mtu sahihi ama asiye sahihi, Jifunze kutompangia MAKUTANO mwenza wako maana Taarifa humsababisha Mtu ajiandae na akijiandaa ATAKUDANGANYA! Mtii Mtu mwenye kuheshimu utii wako, Kumtii MPUMBAVU utatukanwa kwa utii wako.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU