-->

USIRUHUSU MTU AWAYE YEYOTE ATAWALE AKILI YAKO AU MWILI WAKO!

Image may contain: one or more people

Kwanza kabisa USIRUHUSU MTU AWAYE YEYOTE ATAWALE AKILI YAKO AU MWILI WAKO! Chukuwa umakini ambao akili yako itabaki bila msongo na mwili wako usiwe na kiherehereee, Mpe mtu sikio lako ila usimpe moyo wako, onyesha kukubari asemalo mtu ila sio kufuata kila asemacho kwani ukikubari kuongozwa utajikuta unakosa mwelekeo, Zisikilize HISIA zako lakini usizipe nafasi zikakuangamiza, Kila MOYO wa mwana wa adam una shauku ya kupokea FURAHA NA AMANI... Shida sio kupendwa ila shida iko kwenye kudanganywa, Pamoja na hayo JE UNAIJUWA SHIDA YA KULIACHA PENDO AMBALO WEWE BINAFSI YAKO UNALIPENDA?
Kuondoka kwenye PENDO ambalo linagusa moyo wako ni ngumu sana, Japo unaweza kuondoka kwa kuangalia yale ambayo hukuahidiwa na mwenza wako, Kinachoweza kulinda UPENDO ni ahadi zile zilikuvuta ikiwa zinatekelezeka, Kungojea ahadi ambazo hata wewe mwenyewe unazikiri hazitekelezeki ni kujidanganya mwenyewe... Mwenye kuthamini UPENDO hujihesabia deni na malipo yake ni KUMPENDA AMPENDAYE! Jipe muda kupanga yenye mafanikio kuliko kujichukulia kawaida mwisho wake ni wewe kushindwa kupokea haja ya moyo wako, Jifunze kukabiliana na UHITAJI WA MWILI kuliko kuruhusu udhaifu mwisho wake sio mzuri, Mwili una nguvu ya kukuangamiza lakini MOYO unaweza kukulinda ni namna tu wewe kutofautisha kati ya MWILI NA MOYO...
#Elista_kasema_ila_sio_sheria.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU