-->

MAPENZI YA KWELI HUPIMWA JAMBO HILI LIKITOKEA

Image may contain: 2 people, text

PENDO NDANI YA MIGOGORO!
Kwanza kabisa nikiri kwamba UPENDO WA KWELI HAUOGOPI MITIKISIKO INAYOPITA NDANI YAKE... Upendo ni kukiri udhaifu mbele ya mwenza wako, Upendo wa kweli ni kuonekana king'ang'anizi kwa mtu umpendaye, Ni kweli kabisa wako watu hukereka wakipendwa lakini ni kwa sababu ya kudhani mwenzie hana tena mahala anaweza kupendwa, Upendo wenye nguvu ni ule unaweza kuhimili MIGOGORO ISIYOKWISHA... Ukimpenda mtu na ukamuweka akilini mwako automatically anajaa moyoni, Na mtu anapokuwa amejaa Moyoni ni ngumu sana kuikubari hali ya kutokuwa nae, Shida iko kwakwe mtu ambaye anapendwa JE ANATAMBUWA UPENDO WAKO? Hakuna mzigo mzito anaoweza kuubeba Mtu kwenye Mahusiano ama ndoa kama KUBEBA MWENZA ASIYE TAMBUWA MAANA YA PENZI LAO... Kumpenda mtu ambaye anataka kupendwa yeye bila kuurudisha upendo kwa mwenza wake japo kwa Heshima tu ni hatari kuliko hata majanga yoyote yanayotokana na UPENDO! Migogoro hulijenga penzi la dhati ikiwa wahusika watasimamia kile wanakiamini wao, Mahusiano yenye migogoro huvunjika ikiwa kila mmoja atashupaza shingo yake, lakini ikiwa wenye mahusiano watakuwa na migogoro kwa ajili ya kukosoana na kujengana ili kuziondoa tofauti ambazo ndizo zinawaingiza kwenye migogoro hiyo itakuwa ni njia nzuri na yenye kuwapa nguvu ya kuendelea mbele na mahusiano yao, katika MIGOGORO kuna kujifunza na kujisahihisha, Na katika Migogoro kuna kujitenga na kusababisha na Migogoro, Jifunze kugombana kwa MAFANIKIO na usijaribu kuingia kwenye Mgogoro kwa kumtafutia sababu mwenza wako, Usiombe kukutana na Mtu ambaye Furaha yake ni kuona mwenzie akilia juu yake, UPENDO WA DHATI HAUNA MASHINDANO bali unatawaliwa na maridhiano.
#Elista_kasema_ila_sio_she
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU