
Mwanaume ni kama Mbwa, kamwe habembelezewi nyama! Narudia mwanaume ni kama Mbwa, kamwe habembelezewi nyama. Ukiona upo kwenye mahusiano kila siku ni kazi yako kumbembeleza mwanaume basi jua kuwa huyo mwanaume hakutaki! Narudia kama unaona kuwa kila siku ni kumbembeleza mwanaume ili awe na wewe basi jua huyo mwanaume hakutaki.
Unakua ni mtu wa kumpigia simu, kumuambia kuw aunataka kuwa naye lakini anakuambia sikutaki, anakukatia simu, hapokei, anakujibu hovyo, aisee dada yangu huyo mwanaume hakutaki! Narudia, huwezi kumbembeleza mwanaume kuwa na wewe, ukiona unabembeleza, unalazimishia, yaani unakua kama unajisukumizia kwake basi jua huyo mwanaume ana mtu wake.
Narudia, mwanaume ambaye hana mtu wake, yaani ni wewe tu au anakupenda wewe pamoja na kuchepuka hahitaji kubembelezwa, kuhongwa, kulazimishiwa, sijui na kupigiwa simu kuta mara mia hapana, anakua na wewe. Kama una miezi sita, mwaka unamhangaikia manaume ili awe na wewe basi jua kuwa unapoteza muda wako, hakutaki! Hakutaki! Hakutaki! Wala usidhani kuwa kuna kitu utafanya umlazimishe aje kwako!
Hapana, anaweza kuja lakini akipata shida flani, labda kafukuzwa kazi na wewe una vipesa, Biashara zake haziendi vizuri na anataka mkopo, kaachwa anataka kipoozeo cha harakaharaka! Acha kujilazimishia Dada yangu, najua inauma lakini kubali kuumia maisha yaendelee, kukataliwa na mwanaume haimaanishi kuwa wewe ni mbaya, haimaanishi kuwa una kasoro, ni kama kuku wengine wanapenda kuku ila kuna ambao wakila kuku wanaumwa!
Tatiozo dada zangu mnakaa, unamng’ang’ania mwanaume, hakutajki lakini unajitutumua mpaka basi, eti unajipa matumaini atanipenda. Miaka mitano mwanaume kashakuambia hakutaki bado unamng’ang’ania, kushtuka umri ushenda ushaota na mbelewele unaanza kulalamika kuwa mimi sina bahari, kumbe ulikua umekumbatia mtu ambaye hata hakutaki, narudia mwanaume ni kama mbwa, ukiona mbwa hali nyama basi kashiba na hataki, hahitaji kubembelezwa!