Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa majaaliwa ya MUNGU kwamba WEWE ndiye mwenye UPENDO wala sio Mwanaume, Lakini naomba ujue jambo moja;
▪Mwanaume anao upendo zaidi yako ila kwa kufuata vile wewe unampenda, Ndo maana HAKUNA MWANAUME MJANJA KWA MWANAMKE MJANJA.
Yaani MWANAUME ili awe mdhaifu inatokana na Wewe kwa namna ambavyo unaonyesha UPENDO WA DHATI KWAKE ila usiwe na unafiki, Hapo watakurogesha kwamba umemuweka kwenye "KISAHANI" wala hawezi kufurukuta ila kinyume chake MAJANGA.
Nirejee kwenye Maana yangu;
Mwanamke kwa maumbile mnao udhaifu mbaya ambao huo ndo imewagharimu MAHUSIANO NA NDOA zenu bila kujua.
MAZOEA!
Mazoea ya Mwanamke kwa Mwanaume hayo ndiyo yamewaumiza wengi, kwa sababu nature ya MWANAUME kutopenda ilijengeka vichwani mwenu na mkajikuta mnakata tamaa ya kuamini wanaume ila unapopata Mwanaume akakupenda mnachukulia UDHAIFU.
Usimini sana kama ni UDHAIFU Kwani WANAUME HAWATABIRIKI inaweza kuwa amechoka kutanga na njia ama Kuna ka UBORA umejaaliwa, Sasa usijiamini sana kama UKO SPECIAL anaweza kutokea MWANAKHERI akakuondoa kwenye level uliyopo
Kujiamini ndiko kumewaumiza wanawake wengi, Sisemi usijiamini laa hasha KUJIAMINI ninakokutaka ni wewe kuijua THAMANI YAKO ila ukija kwenye Swala la MAPENZI jiweke wewe si Bora kuliko wengine, Kwani iko tofauti kubwa kwenye UBUNIFU maana kila mmoja na kujituma kwake, Kuona Mwanaume hana ujanja kwako ni kosa rafiki yangu, Maana hujui yaliyoko MOYONI MWAKE ila unaishi kwa kufuata kauli na maneno yake, Usiposhituka mapema HUWEZI KUMUONA MWANAUME SAHIHI Kwani unajihesabia haki sana na kujinasibu kwamba UNAPENDWA MNO.
Kwenye MAHUSIANO hakuna mwenye HATI MILIKI ila tunategemeana ki NAFSI na kupeana yaletayo AMANI kinyume chake LOLOTE LINAWEZA KU HAPPEN.