-->

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU.

Ufafanuzi maarufu wa ndoto ambao umembusu mtu, na umempenda sana ...
Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu...
Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu: Panga langu limedondokea mtoni n ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu.
Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili? Jamaa:Hapana.
Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili? Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili? Jamaa akajibu: NDIYO. Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.
Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia? Jamaa akajibu: mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.
Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza: huyu ndiye mkeo? Jamaa akajibu: NDIYO.
Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwanini umenidanganya? Jamaa akajibu: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka n AUNT EZEKIEL, na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu, halafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu, sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.
FUNDISHO
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu, na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote. WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU