▪NGUZO YA KWANZA ni Mwanamke kuwa na hakika kupitia ELIMU yake, Kwa hakika hii ndiyo ambayo ina hakika kuliko kitu chochote kwenye maisha yake.
▪NGUZO YA PILI ni Mwanamke kupata bahati ya MUME na sio Mwanaume, Ikiwa Mwanamke ataolewa na MWANAUME AMBAYE NI MUME kwa hakika hii pia ni sehemu ya Mafanikio yake.
▪NGUZO YA TATU ni Mwanamke Kujaribu KUJINASUA ki maisha kwa kufanya kazi isiyokuwa na uhitaji wa CV kwamba ajitafutie walau pesa itakayoweza kumkimu yeye, Maana yake HAKUSOMA wala HAJABAHATIKA KUWA NA MUME na nguzo hii ndiyo LAST HOPE!
Ni kweli kabisa KESHO YAKO ANAIJUA MUNGU lakini MUNGU huyo huyo alituumba kwa mfano wake, Akatupa akili kwa ajili ya MAISHA Kwani kwenye kuumbwa VIUMBE VYOTE VINA MAUMBILE KAMA YA BIN ADAM lakini Sisi tulipendelewa kwa KUTAMBUWA MEMA NA MABAYA.
Mwanamke fikiria zaidi KESHO YAKO kuliko kuitazama leo ambayo tayari ushaijua.
KWA UFUPI;
Dunia tuliyonayo kwa sasa MWANAMKE kama huna kitu huwezi kumpata MWANAUME ambaye unamtaka wewe, Wanaume halisia wamekuwa ZAO ADIMU kiasi kwamba kila MWANAUME ANAANGALIA UWIANO WA MAISHA kwamba kama utakuwa TEGEMEZI Basi ukubaliane na mambo haya;
¤ MANYANYASO.
¤ UTUMWA.
Lakini Kuna shida nyingine mpo nayo, Yaani hata ukiwa na kazi unaubwaga MOYO wako wote kwa Mwanaume inafika mahala VYA KWAKO VINAKUNYANYASA WHY?
Nihitimishe kwa maana ya Makala yangu ya leo;
Mwanamke USOME, UOLEWE, UBAHATISHE MAISHA ili kuwa na hakika ya kuishi BILA KUWA UMEJITAMBUWA NI KAZI BURE ▪kwamba ELIMU haitakusaidia kwa sababu kutojitambuwa unaweza kutawaliwa na ambaye hajui hata kuandika ila wewe Una DEGREE.
▪Kwamba NDOA inaweza isikusaidie kwa lolote zaidi utazalishwa na kubakia kuwa mlezi wa watoto, wala usiishi kwa Furaha kwenye NDOA yako.
▪Kwamba hata kama una kisimati cha kupata pesa japo HAKUSOMA/HUKUOLEWA ila kwakuwa hujitambui ni rahisi zaidi kuangukia kwenye UTUMWA.
Zaidi ya hapo Kwanini nisiseme MWANAMKE KAMA HUJAJITAMBUWA hata chips🍝 zege inaweza kukupa UDHAIFU?
Mungu akomboe kizazi hiki, Mwanamke tambuwa wewe ndiye TAIFA kwamba bila kuzaa DUNIA HAIONGEZEKI Basi ijue NAFASI YAKO KATIKA JAMII lakini pia JITAMBUWE ili usiishi kinyonge kwa udhaifu wa kijinsia.
#Elista_Kasem_Sio_Sheria 😎