-->

💕Jee Mapenzi Na Mahaba Ni sawa 💕

UTAMU KITANDANI APP
Mapenzi na Mahaba ni vitu ambayo vinaingiliana kwa pamoja kwa lengo moja ya kuleta ladha katika ndoa. Ingawa kwa upande mwengine unaweza kusema ni vitu viwili tofauti vyenye ladha moja ndani ya ndoa. Kwani kunaweza katika ndoa kukosekana Mapenzi lakini kukawa na Mahaba. Au kukakosekana Mahaba kukawa na Mapenzi na ndoa kama hiyo yenye moja kati ya hayo huwa haijakamilika ladha yake. Kwani ladha ya Ndoa lazima itimie Mambo mawili hayo na zaid ya hayo ili upatikane utulivu.
Wengine wanaweza wasikubaliane nami wakaona ni kitu kimoja. Siwapingi mawazo hayo Kwani kila mmoja na ufahamu wake. lakini wengi wamekubaliana kuwa ni vitu viwili tafauti. Mfano ni kama Chumvi na Sukari ni vitu viwili vinavyofanana lakini kila kimoja kina ladha yake kwenye chakula. Na ukitaka chakula kikolee utamu basi vitu viwili hivi vipatikane kisawasawa.
Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako hisia hizi zinapatikana ndani ya moyo na kuupa moyo utulifu furaha na hisia tafauti na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi hayo!una fanya mahaba ili kudhihirisha na kudumisha penzi lako!
Mahaba ni Safari ndefu ndani ya ndoa ukimpenda mwenza wako tu Moyoni na bila kumuonyesha Mahaba utakuwa unampenda na atajua kuwa unampenda lakini ili kujakuza mapenzi hayo lazima uwe na Mahaba ambazo ni kila Action juu ya Mapenzi yako juu yake. Na matendo hayo yawe Madhubuti ili kuifanya Ndoa iwe Imara vitendo ambayo vitamfanya mwenza wako ajue mahaba juu yako na akasahu maudhi machofu n.k . Mke anaweza kumuangalia mume Jicho la mapenzi kwa kumuangalia tu lakini Jicho hilo hilo linaweza kurembushwa kukazwa Na kukonyezwa huko kwa huba kukalifanya Jicho hilo kuingia kwenye Mahaba .
Nitamalizia tu kwa kusema mapenzi yaso mahaba Ni sawa na nyumba iliyo sanifiwa vyema ila ikawa haina plaster ,rangi hata dari !hakika haitapendeza!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU