-->

*KWENU WADADA* *πŸ‡MPENDWA BIBI NDIO USHAOLEWA HIVYO TULIZA MACHO YAKO KWA MUMEOπŸ‡*

UTAMU KITANDANI APP
πŸ‡Mpendwa Bibi! Kabla hujaolewa inaewezekana ulikwisha chumbiwa na watu wengine. Posa za uchumba inawezekana zilitoka kwa watu matajiri, wasomi, wenye sura nzuri na kadhalika ambao ungependa wakuoe
πŸ‡Matarajio ya aina hiyo yalikuwa ni jambo la kawaida kabla ya kuolewa. Lakini sasa umechagua mwenzi wako na kuwekeana mkataba wa dhati naye kuwa wapenzi katika maisha yenu yote, hivyo, sahau yaliyopita kabisa. Lazima uyaweke pembeni matamanio yako ya zamani na usahau ofa hizo za zamani. Usimfikirie mwamanume mwingine yeyote isipokuwa mumeo na utafute amani naye. Kama ukifanya vinginevyo, utajiweka katika hali ya mashaka,
πŸ‡Umekubali kuishi na mumeo, jiepushe na kufikiria maisha ya zamani na wala usimlinganishe mumeo na mwanaume mwengine.
πŸ‡kumlinganisha mumeo na wanaume wengine hakuna manufaa yoyote bali ni kujiweka katika hali ya mateso yasiyo na mwisho na kusababisha upate maumivu makali ya akili.
πŸ‡Ewe dada ulioko kwenye ndoa, ukiyaacha macho yake huru, kila mara utapata maumivu ya neva na utanaswa kwenye mtego wa wivu wakati wote.
πŸ‡Kwa kuwatazama waume wengine na kuwatilia maanani na kuwalinganisha na mumeo, utamuona mwanaume ambaye hana dosari. Unaweza kudhani kwamba labda mwamaume huyo amekamilika kwa sababu huzijui dosari zake. Utafikiria kuwa ndoa yako ina mushkeli, na fikira hii inaweza ikawafikisheni mahali penye mwisho wenye hatari,
πŸ‡Mpendwa Bibi! kama unataka ndoa ya kudumu daima milele, kama hutaki mateso ya kiakili, na kama unataka muendeshe maisha ya kawaida, basi acha kuwa mbinafsi na sahau hayo matarajio yako yasiyofaa.
πŸ‡Usiwapongeze wanaume wengine. Usimfikirie mwanaume yeyote isipokuwa mumeo. Usiendekeze fikira hizi
πŸ‡Afadhali ningeolewa na fulani’
‘Ningependa mume wangu aonekane kama . . . . . .’ ‘Natamaani mume wangu angefanya kazi ya. . .. . . . . .’ ‘Natamaani….. Natamaani……. Natamaani….’
πŸ‡Kwa nini ujifunge jela kwa kuendekeza mawazo hayo?
πŸ‡Kwa nini utibue misingi ya ndoa yako?
πŸ‡Kama lolote kati ya matakwa hayo yangefanikiwa kwa kweli, ungejuaje kwamba ungefanikiwa kuridhika zaidi?
πŸ‡Unao uhakika kwamba wake za waume wajulikanao kama ‘hawana dosari; wanaridhishwa nao?
πŸ‡Mpendwa Bibi! mumeo akishuku kwamba unaonesha kuvutiwa na wanaume wengine, atakata tamaa na kuacha kuvutiwa na wewe.
*πŸ‡Jihifadhi na ifadhi kila kitu ikiwemo fikra zako kwa mumeo tu, kwa ajili ya kupsta radhi za AllahπŸ‡*
*πŸ‡Bibie Jitulize kwa mumeo Acha kutolea macho waume wengineπŸ‡*
*Allah awafanyieni wepesi katika ndoa zenu*
πŸ‡....MWISHO......πŸ‡
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU