-->

NINI CHA KUFANYA PALE MPENZI WAKO ANAPOTAKA MTENGANE KWA MUDA/ANAPOTAKA UMPE MUDA!

Image result for MWANAMKE NDOA

Habari, mmimi ni mwanamke wa miaka 31, naishi na mwanaume ambaye nimezaa naye mtoto mmoja, kuna wakati nilimfumania na rafiki yangu akaniomba msamaha yakaisha. Lakini sasa amebadilika, ilikua alete mahari mwaka huu mwezi wa pili ila sasa anasema kuwa niondoke niende nyumbani kwanza kwani hayuko tayari kwa kuoa kwasasa nimpe muda.
Sasa nashindwa nifanyeje kwani bado nampenda na nimeshapoteza muda wangu mwingi kwake. Amesema kuwa baada ya muda atanifuata na kunioa lakini sina uhakika na hilo. Sasa hivi tunafuraha na anaasema mtoto atamtunza nikiwa huko ila atakuja kunichukua akiwa tayari, nimechanganyikiwa sijui nifanyeje.
JIBU LANGU;
Kwanza pole kwa hali iliyokukuta, lakini ndiyo maisha ya siku hizi, kwamba ulishafanya kosa kuishi naye kabla ya ndoa hivyo anaona kua ana haki ya kukuambia chochote wakati wowote uondoke na kwakua hamjafunga ndoa bado na yeye amesema atahudumia mtoto basi hata huna sehemu ya kwenda kulalamika.
Labda kabla ya kukuambia nini cha kufanya nikuambie ni kwanini mwanaume anaweza kukuambia kua nakupa muda ili ajipange ndio atakuchukua. Kuna sababu kama tatu hivi kubwa za mwanaume kusema hivyo, sababau ya kwanza nikuwa anakuacha kistaarabu, sababu ya pili unatabia mbaya ambazo anataka ukajirekebishe na sababu ya tatu hajui anataka nini?
Tukianza na sababu ya kwanza nikua mekua mkiishi vizuri, anakuona kama mwanamke mwema, hujawahi kumkosea lakini kwakua hakupendi, au alikua anakupenda lakini sasa kapata mtu mwingine basi hukuambia kuwa uondoke na yeye ajipange. Kwamba hawezi kukufukuza kama mbwa hivyo anaamua kukuondoa kistaarabu.
Hii hutokea hata kwa wapenzi wa kawaida ambao hukuambia kua mpeane muda hivyo katika muda huo ukiwa mbali, mkiwa hamna mahusiano mazuri basi kwake ni rahisi kukuambia kwaheri. Sababau ya pili nikuwa ameshindwa kukuvumilia na tabia zako (hili kwako silioni) hivyo anakuambia uondoke ukarekebishwe kwenu.
Huyu ni mwanaume ambaye anakupeda na sana ila ameshindwa kukuvumilia na anaona akiendelea kukaa na wewe atachanganyikiwa au hata kukupiga na hataki. Mara nyingi mtu kama huyu mnakua mshakorofishana sana na anakuambia kabisa sababu ya kukurudisha kwenu au kutaka kuishi mbali na wewe.
Kwamba anakuambia anakupenda ila kwakua unatabia flani anataka ukajirekebishe. Huyu anweza kukurudia kama ukijirekebisha kwakua anakupenda. Sababu ya tatu nikwakua hajajitambua, hajui anataka nini katika maisha yake, inawezekana anakupenda lakini anakimbia majukumu, kwamba anajiona hayuko tayari kubeba majukumu hivyo anakuambia uondoke.
Huyu anakua anajipanga anaweza kukurudia au la! Au akakutelekeza kwani anajua utalea mtoto kwakua una uwezo wa kufanya hivyo. Mara nyingi hukuacha kwakua hataki kupangiwa majukumu, hataki kusimamiwa mambo anaogopa kutegemewa hivyo hukurudisha ili ajipange, huyu anaweza kukurudia au akatafuta mwingine na kukuacha.
NINI CHA KUFANYA UNAPOPEWA MUDA?
Suala la mahusiano ni jambo la watu wawili kwamba nilazima kila mmoja amkubali mwenzake na akuabali kuishi naye. Kuna mambo mawili unaweza kuyafanya hapa, kwanza unaweza kugoma kuondoka na ukabaki ukisema liwalo na liwe,ukasema huwezi kutelekezewa mtoto kwenda kulea peke yako basi mkaendelea hivyo hivyo.
Kibaya hapa nikua utaishi maisha ya mateso kwani atafanya mambo kwa kukukomoa, anaweza hata kukuletea wanawake wengine ndani na kwakua hajakuoa hutaweza kulalamika kwani umeng’ang’ania wewe mwenyewe. Lakini kuna jambo la pili ambalo ndiyo ninalolipendekeza ambalo ni kuondoka na hapa kikubwa ni kujua ni namna gani utaondoka?
Ongea Naye; Ukiamua kuondoka nilazima kwanza uongee naye, kama ninavyosema usilalamike, usione kunyong’onyea kutokana na uamuzi wake. Hapana, ongea naye kutaka kujua sababu, kama akikuambia sawa asipokuambia wala usisisitize, kubali lakini muambie mipango yako.
Kwamba muambiwe wewe ungetaka iwe hivi na vile, kwamba ajue kua unaondoka lakini bado unampenda na ungependa kitu flani. Lakini pia muambie kuwa hutasubiri milele kwamba hata kama asipokuambia urudi lini lakini ajue kuwa nawewe una maisha hivyo hutaka akumsubiri tu.
Jipe Muda Wako/Mpe Muda; Hili ni la muhimu sana, yeye kakuambia ondoka na hajakuambia mnaruidiana lini, ukiangalia sababu hapo juu unaweza kuona kua mnaweza msirudiane hivyo usikubali kusubiri milele, hembu na wewe jipe muda , kwamba sema kabisa naondoka naenda kumvumilia kujipanga lakini sitavumilia zaidi ya mdua flani.
Muda wa juu kabisa usizidi miezi mitatu, kwamba kama atafikisha miezi mitatu na hataki mrudiane, sio unamuuliza kila siku hapana, kama yeye tu hataki basi unaendelea na maisha yako unamuacha. Hili ni muhimu sana kwani ukisubiri mpaka mashetani yake yakutake unaweza kusubiri miaka. Mara nyingi wanaume wanaumna hii hukutelekeza kabisa, anakuweka kama kiporo chake hata kukuhudumia hakuhudumii.
Kwamba ataenda kufanya ujinga wake, akafanya mambo yake lakini sasa kama mambo yakiwa mabaya ndiyo anarudia kiporo anakuambia tuendelee. Hapana usikubali kuwa kiporo, jipe muda na kama ule muda ukiisha kabla hajakurudia mpigie simu muambie umechoka kusubiri na mmeachana anaweza kuendelea na maisha yake kwani wewe unaendelea na yako.
Hapo muambie husubiri tena na muambie mtakua marafiki lakini kuhusu mapenzi ushafunga mkataba. Hapa kama alikua anakupenda atakuambia muonane muongee na kama alikua ashakuacha atakuambia kwaheri. Kwa maana hiyo hatua hii ni muhimu kwani ndiyo unajua kama anakupenda au la?
Endelea Na Maisha Yako/Acha Kusubiri; Siku ile tu unaondoka kwake, siku ile ambayo anakuambia anakupa muda basi usisubiri hata dakika tano, endelea na maisha yako kama vile huna mtu, acha kumsubiri. Hapa nikimaanisha kua ingawa kimapenzi umempa muda kama nilivyofafanua hapo juu lakini kimaisha, kiuchumi usimpe hata sekunde.
Usikae na kusubiri labda akinioa nitakua na hiki na kile, kaa ukiwaza kua hakuoi hivyo waza utafanya nini katika maisha yako, kuwekeza kikazi na kibiashara, kwamba uwaze mambo yako ya maendeleo tena bila kumshirikisha. Yaani ishi kipotelia ya mbali kama akirudi poa na asiporudi angalau sitakua nimepoteza muda wangu mwingi.
Punguza kumtafuta ukimpigia simu mara mbili tatu kama hajakupigia yeye tena mpotezee na acha kuonyesha kua maisha yako hayaendi bila yeye. Kwamba katika kipindi hiki yeye anadhani kua huna maisha hivyo atakutaka umnyenyekee, wanawake wengi hukosea kwa kuzidi kunyenyekea.
Kupiga simu mara kwa mara na kila siku kuulizia kama bado wanapendwa. Hili ni kosa kwani unaanza kuwa kero, kama anakupenda atakujali hata kidogo, kama ukimpigia simu mara mbili hajakupigia basi acha hata kama ikipita wiki basi jua haikua rizki, nilazima ujithamini na uonyeshe kuwa una maisha yako.
Lakini kama akikutafuta basi chat naye na ongea naye kama kila kitu kiko sawa na si kama umechanganyikiwa juu yake unasubiria majibu yake ndiyo uendelee na maisha yako. Kumnyenyekea kunaweza kumrudisha mapema lakini kunaweza kumkimbiza moja kwa moja na hata akarudi lakini kwa manyanyaso akijua kuwa unamhitaji kuliko anavyokuhitaji.
Mrudie Kama Hujaanza Mahusiano Mengine; Kuna ule muda ulijipa. Ni muda ambao unaweza kuanza kutafuta mahusiano mapya, lakini haimaanishi kua ukiachana na mtu leo kesho utakua na mtu mwingine, hapana. Lakini sasa kuna kitu ambacho kipo sana, wanaume wengi wakiona umeendelea na maisha yako, wakiona umefanikiwa basi hurudi.
Ndiyo akikuona unafuraha bila yeye ndiyo huanza kujiona mjinga na kuja kuomba msamaha. Sasa kama una mtu mpya na ushaanza kumpenda mtu mpya nakushauri usigeuke nyuma hata kama bado hujamsaaau kwani utajuta. Inawezekana anataka tu kukuharibia ili uwe kama yeye ambaye alikuacha lakini analia kila siku.
Lakini kama muda uliompa umeisha, akarudi wakati na wewe hujapata mtu, akarudi na sababau za kueleweka basi unaweza kumsamehe. Lakini namna ya kumsahehe sasa ndiyo watu wengi hukosea, kuomba kwake msamaha au yeye kusema ashatafakari sasa anatama mrudiane si kitu, kitu ni kujua kwanini alitaka mauchane au kwanini alikupa muda.
Hakukupa muda tu, kuna sababu hivyo nilazima uzijue na muambie kabisa kua kama tutarudiana bila kujua sababu basi ipo siku tutachokana nilazima muongee sababu za kutengana kkwenu ili msirudi kulekule, umuambie na wewe mambo yanayokukera kwake na muelewane kwanza.
Usijisikie tu raha kurudiana na mtu ambaye mlishatengana kwakua tu kaomba msamaha, nilazima muyamalize hayo mambo yaliuyowafanya mtengane kwanzakabla ya kuanza mapmbo mapya. Nimalizie tu kwa kusema kupeana muda si kitu kibaya kama utajua namna ya kudili nacho na kuwekeza katika maisha yako binafasi bila kumsubiri aliyekupa muda
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU