Hivi ni kweli Uwezo wako umefikia mwisho kiasi kwamba Huwezi kusonga mbele hata kwa hatua mbili zaidi? π€
Unadhani maisha uliyopewa ni kwa ajili ya kula, kulala, kwenda chooni, na kuangalia muvi?
Ile hamasa yako ya kufanya makubwa na kuleta mapinduzi kwenye Jamii yako Imeenda wapi? π€·πΏββοΈ
Ile Ndoto Yako ya kuwa mfano wa kuigwa kwenye ukoo wenu imeenda wapi? π€·πΏββοΈ
Tabia zako njema ulizokuwa unasifiwa kwazo Mtaani kwenu zimepotelea wapi?π€·πΏββοΈ
Sahivi nakuona Umekata tamaa kabisa. Huamini tena kama nawe unastahili kufanikiwa. Umeamua kukaa Pembeni Siku ziende. Raha yako ni kuona Giza limeingia ili Ulale, Siku ipite.
Unadhani uliletwa Duniani kutalii na kuondoka? ππ»ββοΈ
Jitafakari kwa upya.π€
Usikubali kuchezea umri wako na nguvu ulizonazo.
Una Uwezo wa kufanya mambo makubwa sana kuliko yale uliyoyafanya huko Nyuma.
Simama tena.πΊπΎ
Jikung'ute mavumbi na kuanza kusonga mbele.
Ifufue Ndoto iliyokufa ndani yako, Amsha Uwezo uliyolala ndani yako, Simamisha Imani iliyoanguka ndani yako.
Komaa mpaka Utoboe.
Pigana mpaka ushinde.
Tenda mpaka Uone Matokeo makubwa.
Pigana mpaka ushinde.
Tenda mpaka Uone Matokeo makubwa.
Hujachelewa, Ila utachelewa ukighairi kubadilika kuanzia sasa.
Amua Leo kuwa wa Tofauti. Kesho Bora Inatengenezwa Leo.