-->

*ZIJUE AINA ZA WANAUME*

SWALI KWA WADADA...HIVI WANAUME WAREFU NA WEUSI WANA NINI CHA ...*1: MUME BACHELA*
Anafanya mambo kivyake-vyake bila kumshaurisha wala kumshirikisha mke. Muda mwingi anautumia kukaa na marafiki kuliko mkewe. Hayuko siriaz na maisha ya ndoa.
*2: MUME GESI*
Huyu muda wote anachemka mama asidi, ana hasira kali, mgumu, anatawala kila jambo na ni hatari.
*3: MUME MTUMWA*
Anataka kutendewa kama mfalme lakini anamtendea mkewe kama mtumwa. Anataka mkewe kama mtu kwake, asiyestahiki heshima yoyote.
*4: MUME CHA WOTE*
Huyu ni mume wa kila mwanamke. Anawapenda na kuwajali zaidi wanawake wa nje kuliko mkewe. Anapenda kuwapatia pesa wanawake wa nje, na ana marafiki wengi wa kike.
*5: MUME MKAVU*
Mkali na bahili, hajali hisia za mkewe, anafanya ndoa isiwe na raha. Ni mgumu kwelikweli, hataniwi.
*6: MUME PANADOL*
Anamtumia mkewe kama mtatuzi wa tatizo, anampenda mkewe pale tu anapohitaji kitu kutoka kwake. Ni mjanja, anaujua udhaifu wa mkewe na kuutumia kama mtaji wake.
*7: MUME KIMELEA*
Mvivu, anampenda mke kwa ajili ya pesa tu. Anatumia pesa za mkewe kuhonga wanawake. Hana shughuli yoyote na hamsaidii mkewe kwa majukumu ya nyumbani.
*8: MTOTO WA MAMA*
Si muwajibikaji, ana utoto na hawezi kufanya maamuzi yeye kama yeye bila kumuuliza mama yake au ndugu zake; anamlinganisha mke na ndugu, ambapo linapotokea jambo hukimbilia kwa ndugu.
*9: MUME MZURURAJI*
Muda mwingi hatulii nyumbani, anakuja kama mgeni na kuondoka. Anaipatia familia mahitaji yote ya vitu lakini hana muda nao.
*10: MUME MBEMBEZI*
Ni mume mbembezi na mwenye mahaba. Anaipatia familia yake mahitajio ya kimwili na kiroho na atenga muda kwa ajili yao. Anaiongoza nyumba yake kiroho. Anawajibika sana na anaishi na mkewe kama mwenza na msaidizi wake.
JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI LIPI? UMEMFANYA MKEO AWE MTU WA AINA GANI?
UMEFAIDIKA NINI KUTOKANA NA MABAYA YAKO KAMA MUME?
Badilika... Hujachelewa bado......✍️
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU