-->

JINSI YA KUKABILIANA NA WIVU KATIKA UHUSIANO WA KIMAPENZI.


Wivu ni hisia za ajabu, hususan katika uhusiano wa kimapenzi. Ukiuruhusu wivu kushamiri ndani yako, unaweza kuwa na nguvu yenye madhara makubwa kwako na kwa wengine.
Kwani Wivu unaweza kukufanya ukamuua mtu mwenye suluhisho la shida yako wakati haujui jinsi ya kutoka hapo ulipo.
Hata hivyo, kwa upande mwema, wivu ni hisia za kawaida kabisa na kwamba kuna mikakati ya kimsingi ambayo unaweza kuitumia kuudhibiti.
Mikakati hiyo inaweza kuchukuliwa kwa kupitia hatua zifuatazo:
HATUA YA KWANZA
Piga moyo konde kwa kutuliza hisia zako unapoona wivu unakukamata. Jaribu kutambua mzizi wa hisia hizo. Wivu katika hali halisi ni woga wa kumpoteza mtu au kitu fulani. Wivu huenda sambamba na hasira kwamba mtu fulani amevamia eneo au mali yako.
Fikiria ni nini hasa lengo la wivu wako.
Mara nyingi, watu hutumia hisia zao za wivu katika kutaka kutoa vipaumbele kwenye masuala yanayohusu maisha na uhusiano wao. Hivyo, jiulize ni kwa nini unahisi kuna tishio katika mazingira yanayokukabili.
Kufanya hivyo kutakusaidia kuchukua hatua njema na za busara katika kuelewa ni nini kilicho muhimu kwako.
Kwa mfano ukigundua mume anataka kukuacha, anakusaliti kwa sababu ya ukorofi wako, chukua hatua ya kuondoa ukorofi huo, ili woga wa kuachwa uondoke. Timiza majukumu yako katika uhusiano wako, usiwe mtu wa kumfikiria mwingine na kuacha kujifikiria mwenyewe!
HATUA YA PILI
Ni muhimu kuzitambua fikra na maneno yanayokuja akilini kwako ambayo yanaweza kuchochea hisia za wivu moyoni mwako.
Watu wanaojiona ni wa hali ya chini na wanaoamini kwamba watu wengine wanawatenga, mara nyingi hujikuta katika dimbwi la wivu. Fanya juu-chini utambue fikra zinazokutuma kuwa na hisia za wivu, na badala yake fikra hizo zifute na kupanda fikra za kujiamini.
Iwapo una marafiki ambayo inachochea hisia hizo mbaya, basi ni heri kwenda kutafuta marafiki ambao watakuunga mkono katika hali ya kujiamini.
Hebu jiulize kama mwanaume alikuchagua wewe miongoni mwa wanawake milioni 50, kwa nini usijione mshindi kwake na kujipa nafasi ya kudumu?
Jipe muda wa kukomaa na kujifunza yale yote yanayotokana na wivu.
Huwezi kujenga moyo wa kujiamini katika muda mfupi.
Ni lazima kwanza ujisafishe roho na hisia zako, ufanye mazungumzo na watu wengine ili kupata ujuzi wa kukabiliana na wivu ambao ukizidi huweza kuwa kero ndani ya penzi na hatimaye kuvunja penzi lako
Natamani niendelee ila kutokana na leo nafasi yangu finyu itabidi niishie hapa.
👇
Image may contain: text that says "WIVU NI UGONJWA UKIUENDEKEZA UTAKONDA"
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU