-->

HATA UKIWA BUSY KWA KIASI GANI KAMA UNA MWANAMKE UNAMPENDA JITAHIDI UFANYE HIVI KILA SIKU.

 UTAMU KITANDANI APP

Kama una mwanamke wako unampenda na hutaki kumpoteza, hata kama upo bize namna gani basi hakikisha kuwa kwa siku unampigia simu hata mara moja. Hata kama mnaishi pamoja ni mke wako, lakini kama hamfanyi kazi ambayo kila dakika mnaonana basi mchana ukiwa kazini mpigie, msalimie na muulizie kuhusu siku yake. Kama uko mbali naye hakikisha unampigia na kupiga stori kidogo.

Kwa wanaume kinaweza kuwa kitu kidogo lakini kwa mwanamke suala la simu ni la muhimu. Kwa mwanamke mapenzi sio kuhudumia familia tu bali ni kujali na moja ya vitu ambavyo vinawasisimua wanawake ni simu. Lakini unapompigia hembu fanya kama unaongea na mwanamke na si kama unaongea na mwanaume mwenzako, kuna watu wanapiga simu kweli lakini wanakua wagumu kama chapatti za kichaga, hapana, lainika kidogo.

Baada ya kuuliza kuhusu watoto muulizie yeye kuhusu siku yake, sizungumzii yale maswali ya umevaa nini ila muulize kama kala, muulize kuhusu kazini au nyumbani, wakati mwingine hata kama ni uongo muulize vipi unaumwa mbona unaongea kama umechoka choka nini tatizo, hata akudanganye kuwa hajisikii vizuri, tafuta umbea wakupiga naye afurahie kuongea na mume sio unampigia simu akikata amenuna utafikiri alikua anaongea na mwalimu mkuu.

Mimi nishamaliza sasa wewe jifanye mgumu huongei naye wakati dereva Bajaji tu akipigiwa simu njoo nichukue hapa nyumbani anaanza.
“Uko tayari lakini, maana na wewe ukishaanza kujiremba... leo nikija sisubiri hata kidogo, labda uvae lile gauni lako la... ndiyo nitasubir...” madoido mengi anamtania mke wako, anamlegezea sauti wakati wewe unajifanya mgumu wakati bosi wako akikuita ofisini kwake hukai mpaka uambiwe kaa! Badilika maisha yenyewe mafupi unampa nani kisirani, au unafikiri ukinuna ndiyo utajiri!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU