-->

KUNA TOFAUTI KATI YA KUACHANA NA MKE NA KUTENGANA NA MKE!


UTAMU KITANDANI APP
Ukikutana na mume wa mtu, amefunga ndoa na mwanamke mwingine lakini walishatengana labda hata miaka kumi iliyopita, lakini huyo mwanaume hajampa huyo mwanamke talaka hata kama hawana mawasiliano kabisa, hata kama hawkaua na mtoto, hata kama sijui nini na nini kama hajamapa talakja basi jua kuna mambo mawili. Kwanza inawezekana mwanaume bado anampenda huyo mwanamke wake hivyo hataki kumuacha mazima.

Lakini pili inawezekana kuwa mwanaume anaogopa kuwa akimpa talaka huyo mwanamke basi watagawana mali. Ni sababu hizo tu, narudia kwa uzoefu wangu ziko mbili tu, bado anampenda au anaogopa kugawana mali. Sasa usijitie kichwa kichwa na kuingia kwenye mahusiano na huyo mtu kisha mkasema mnafanya mambo kwa pamoja. Kumbuka kuwa hata kama hawaishi pamoja lakini kisheria hao watu ni mke na mume, labda kama walishaanza mchakato wa talaka mahakamani.

Lakini kama hakuna kesi ya talaka mahakamani huyo mwanamke ambaye kuna miaka 50 kamuacha kijijini hata jina lake halikumbuki basi ni mke wake, ana haki zote za mke kana kwamba wanapendana kama jana. Haki zenyewe ni pamoja na anaweza kuamua kukushitaki kuwa unatembea na mume wake jambo ambalo ni kosa kisheria, pili akianzisha mchakato wa mahakamani anaweza kudai mali na inahesabika siku ambayo mchakato umeanza, maana kule ni suhahidi kwamba anaweza kusema hawakutengana bali mwanaume alikua anaishi sehemu A na yeye B kama familia nyingi zilivyo.

Yaani akasema ni kama watani wangu wachaga ambao wanaacha wake Moshi miaka 100 anakuja mjini kutafuta, lakini jingine ambaloi wengi hawawazi ni kama Mungu akimchukua yule mwanamke kisheria ndiyo anatambulika kama mke na wewe ni kama hawara na kisheria, hawara na watoto wa hawara hawarithi. Sikutishi ila huo ndiyo ukweli hivyo sikuambii uachane naye ila kuwa makini katika uwekezaji hasa kama wewe nawe unachangia, unaweza kuhangaika na jamaa halafu kuna mtu yuko huko anakula bata siku anakuja anasema “Mali za mume wangu!”

Nishamaliza ila naomba niwakumbushe kitu kingine kuwa, inamaana kama bado anampenda wakirudiana wewe unawekwa benchi, na kama anaogopa kugawana mali halafu na wewe mnachuma mali tena unachangia.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU