-->

HATA KAMA UMEUMIZWA SANA UNAPOTONGOZWA ACHA KABISA HII KAULI!

UTAMU KITANDANI APP

Umeumizwa sana kwenye mahusiano, umelia sana mpaka umekata tamaa. Unakutana na mwanaume mwingine, anakutongoza unaanza kwa kauli hii “Nimeishaumizwa sana mimi siwezi kupenda tena katika maisha yangu na siamini kabisa wanaume!” ukianza na kauli hii Dada yangu jua kabisa kuwa hayo mahuiano hata yakuelekea kwenye ndoa lakini ni kama yamekufa.

Labda ukutane na mwanaume muelewa sana ambaye atasoma saikolojia yako na kujua kuwa, hukuongea hivyo kwakua humpendi bali umeongea kwakua umeumizwa sana na unachogitaji ni mtu wa kukufundisha upendo, mtu wa kukuonyesha dunia nyingine ya raha, dunia ambayo haina maumivu. Ubaya ni kuwa wanaume wa namna hii wako wachache.

Wanaume waliowengi ukimuambia hivi kwanza anakua na hasira, anaona kuwa humpendi, anahisi unamdgharau na kubwa kabisa mbaya zaidi anahisi kuwa bado unamkumbuka X wako, una hisia naye ndiyo maana unasema hivyo. Inakua ngumu kwa mwanaume kusahau maneno hayo, inakua ngumu kwa mwanaume kuamini kuwa umejifunza kumpend,a hata ikitokea akakuonyesha mapenzi, ukampenda na kusahau maumivu yako lakini inakua ngumu yeye kusahau.

Hivyo Dada zangu, hata kama umeumizwa namna hani, hata kama kweli huamini tena wanaume, hata kama humpendi mwanaume wako uko naye tu kwakua Baridi imeizidi au na wew eunataka kuolewa basi, usimuambie mwanaume siwezi kupenda tena au siamaini tena wanaume. Narudia kuna wanaume wachache ni walewa ila wengi si waelewa. Mwanamke unaweza kumuambia hicvi akasahau lakini wanaume ni ngumu, hivyo mengine kaa nayo huna haja ya kumuambia mtu ambaye uko naye kuwa huwezi kumuamini au kumpenda!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU