-->

ACHA KUUTESA MOYO WAKO- Naomba Nisikilize Dada Yangu Kipenzi,

UTAMU KITANDANI APP
Unajua Inashangaza Pale Ambapo Mwanamke Mrembo Unang'ang'ana na mwanaume Ambaye Hata Hana Muda wa Kukufikiria.

Yaani Unapoteza Muda Wako Kumuwaza MTU Ambaye Hatumii Hata Sekunde 15 kukukumbuka.

Unamwona kabisa hana Muda Na Wewe lakini unapambana kumshikilia Wakati Mwenzako anataka kwenda.

Unapata Mwanamke uko na kaboyfriend kako ambako kila ukikatafuta kanakwambia Niko bize, kila siku unatuma meseji hazijibiwi MTU huko bize.. Lakini ukimwambia njoo geto nimekumisi atakuja kukukunja siku nzima wala asikwambie kwamba huko bize

Inaumiza kuona kwamba Wanawake Wengi mnaingia na kung'ang'ania Katika Mahusiano yasiyo sahihi kwenu na mnashindwa kujinasua mkitegemea jamaa atabadilika.

Dada unakaa unajiuliza Yule Mwanaume aliyekuwa anakujali, na kukupenda amepotelea wapi mbona mwanzo hakuwa bize kama hivi?? Inafika mahali anasahau hata namna alivokusevu Kwenye simu yake lakini nakuambia siku mnakutana Hawezi sahau kilicho chini ya nguo zako za ndani wala kilicho kifuani kwako.

Kwanini Upoteze Muda Wako Kwa Mwanaume Asiye Kuthamini? Utakaa ulie Mpaka lini Kwa Ajili Ya Mwanaume Anayekutafuta Siku Anataka Kuona Utupu Wako?? Kama kweli Anakupenda Atafanya Muda Kwa. Ajili Yako. Ukiona Hutafutwi Elewa Wewe Sio Mwanamke Wake Wa Pekee. Wewe ni Kamchepuko Mama Kwenye Moyo wake Anatafutwa kila SAA.

Ukiona amekuchangamkia hyo siku basi elewa kwa mwenye mali yake mambo hayako sawa. Basi anakuja kwako spea tairi ili apunguze upweke kwanini lakini?? Nafikiri Nimekwambia Ukweli na Ukweli Ukuweke Huru, usikubali kuwa chaguo la pili kwa mwanaume yeyote.. Wewe ni mrembo unastahil kilicho bora.

Kama ukiamua kuwa chaguo la pili ni jukumu lako ila nimejaribu kukupa uhalisia.

Usiruhusu Mwanaume Yeyote Akuchezee Hisia zako (hata kama ni Mimi😂😂) Usiumize Moyo Wako, wala usijitafutiw huzuni kwa watu wanaojionyesha wazi kwamba ni wapita njia.

Mwisho wa siku Utaumwa na utakufa wala hawatakuja kukuzika Mwenzangu alafu hasara sijui itakuwa ya nani

Maandiko Matakatifu Yanasema: Ulinde Moyo Wako Kuliko Kitu Chochote Maana Huko Ndio Zitokapo Chemichemi Za Uzima.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU