-->

WANAWAKE WANAKOSEA SANA HILI HASA KWENYE SUALA LA MAPENZI

Image may contain: 2 people, people sitting and indoor

Mama na Dada zangu kwanza niwapongeze kwa kujaaliwa na MWENYEZI MUNGU mko na kitu kinachowafanya wanaume KUPAGAWAπŸ’ƒ
Lakini pia niwape pole kwa kupewa UDHAIFU WA MAAMUZI na hilo ndilo ambalo linawapelekea kuingizwa kwenye UKATILI USIOELEZEKA😭
Natamani kama niingie kwenye vichwa vyenu nifanye marekebisho kidogo tu Kwani MAWASILIANO baina ya MOYO NA AKILI YA MWANAMKE yako down sana kiasi kwamba Mwanamke anashindwa kujua;
AMETOKA WAPI?
YUKO WAPI?
ANAKWENDA WAPI?
Mwisho wa siku ana "STUCK" Yaani ni kama anaona giza mbele, anasahau alikotoka, na asijue yuko wapiπŸ˜‚
Napendaga kutumia neno moja wahenga walipata kunena "MTAKA NYINGI NASABA HUPATA MWINGI MSIBA"
Yaani alikuwa binti alihitaji MUME lakini kwa kutojua ama kwa uchaguzi wa papara akakutana na MWANAUMEπŸ™†πŸΏ‍♂ Maisha yake yakawa na wingi wa stress, Akajikuta amekuwa MAMA baada ya kupata mtoto lakini alikosa ukaribu wa MUME kwa sababu alikuwa na MWANAUME... Mtoto alipokua alitamani kutaka kujua kama KUTAKUWA NA MABADILIKO YA MWANAUME KUWA MUME lakini alipoona ni ngumu akatafuta AMANI ila hakuipata😭
Kinachofuata ni kuwasikiliza wapiga miruzi huko BARABARANI akina nanihiiiiπŸ’ƒ
Mwanamke anajikuta anakwenda nje ya ndoa yake kutafuta japo RELIEF inauma sana😭
Mapenzi yakuiba always ni MATAMU SANAπŸ‘Œhayanaga MJANJA kila mmoja hujikuta amekuwa ZOBAπŸ˜‚
Hapo ndipo MWANAMKE atapata BURUDANI YA NAFSI mwisho kabisa ni kurudi nyumbani akiwa ameridhika, Unajua kifuatacho?
Ni Mwanamke kuiona NDOA yake kama kambi ya wakimbizi akilinda MTOTO NA HESHIMA KWENYE JAMII lakini asijue kwamba MWANAUME AKIZOEA KUMTESA MWANAMKE NA AKAWA MWINGI WA LAWAMA wallah zikiisha lawama mwanaume huhisi anaonewaπŸ˜‚
Sasa zile lawama Mwanamke alizitoa kwa Mwanaume enzi akiomba FURAHA NA AMANI hapo ndipo Mwanaume nae ataitafuta FURAHA NA AMANI asiione mwisho wa siku ni kujawa wivu na ubabe usiosemeka, Mwanamke asipotumia akili MWANAUME ATAANZA KUJENGA CHUKI NA ROHO MBAYA YA KUTAKA KUMLIPIZA MWANAMKE KWA UBAYAπŸ™†πŸΏ‍♂
Mwanamke hayo hayajui maana MOYO WA MTU NI CHAKA huwezi kujua mwenzio anawaza nini, Hapo ndipo utajua kwamba KOSA LA MWANAMKE NI KUTOAMUA MAAMUZI SAHIHI KWAMBA NDOA IMEKUWA NDOANA BORA KUACHANA ili awe huru kutafuta MUME na sio Mwanaume kama ambavyo alikosea mwanzo, Maana yake MWANAUME ANABAKI KUWEPO NA HUKO NJE ANAKUWA NA MAHUSIANO bila kujua ni hatari MASIKINI wa Mungu alichukulia kawaida ndo unasikia Haya matukio mabaya kabisa juu ya Wanawake, Mapenzi usiyalazimishe kwa aina yoyote ile iwe jamii, watoto, Mali na mambo kama hayo, AMANI na FURAHA hazinunuliwi bali zinajengwa na ujenzi wake ni UPENDO WA DHATI! Kama umeona hamuendani OMBA KUACHANA ila ukiendelea kuwepo na huku mwenzio anaugulia wivu ndani kwa ndani NI HATARI SANA🚫
Wanawake najua mko na UPENDO wa kweli kwa Wanaume na ndo maana Mwanaume anapobadilisha mwelekeo kwenye NDOA yake mara nyingi humpa majeraha makubwa Mkewe kwa sababu wapo wanaume wanaoa bila kuwa na UPENDO NA MWANAMKE HUYO pengine tamaa za kimwili ama kutafuta heshima kwenye jamii kwamba ameoa na Kuna wengine WANAOA KUFUATA MTEREMKO WA KI MAISHA🀦🏾‍♂
Lakini nikiri kabisa HAKUNA MWANAMKE ANAOLEWA HAJAWA TAYARI KUWA MKE NA WALIO WENGI HUINGIA KWENYE NDOA KWA MOYO WA DHATI ndo maana wanapogunduwa kwamba matarajio yao yamekuwa ndoto asipopata kisukari ni BP au akijiongeza atakuwa na MCHEPUKO japo wa kupoza makali ya maumivu, Niwaombe kwa DHATI ya MOYO WANGU WANAWAKE WOTE fungueni macho muone unyanyasaji mnaotendewa na wanaume, Fungueni masikio yenu msikilize kauli za kibabe na maneno yaliyoujaza moyo wa mwenza wako ili UPAMBANUE ili uchukue hatua, Haba na Haba hujaza kibaba πŸ˜‚
Uonapo Mwanaume anakutendea ubaya mdogo bila huruma ujue IKO SIKU UBAYA UTAKUA MKUBWA NA MADHARA YAKE UTAYAJUTIA UKIBAKI HAI ILA UKIPOTEZA UHAI JIULIZE JUU YA MTOTO/WATOTO WAKO NANI ATAWALEA? Dunia iliisha kitambo kipindi cha akina Mtume S.A.W kwa sasa tunailazimisha tu ndo maana matukio ya kikatili na kutendeana mabaya imekuwa rahisi😭
Inuka ki FIKRA usibweteke MAISHA YAKO MBELE YAKO na sio hapo ambapo tayari ulishaona hapakufai, THINKING AT YOUR OWN RISK
#Elista_kasema_ila_Sio_sheriaπŸ™‹πŸ»‍♂
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU