-->

Nataka kusema nanyi Wanawake aka MAMA ZETU!

Image may contain: 2 people, people standing, beard and outdoor, text that says "HALED ABO RAYA"
Kwanza muijue nafasi yenu katika jamii kwamba PASIPO MWANAMKE DUNIA HAIONGEZEKI
Lakini pia pasipo MWANAMKE maana yake hakuna MAISHA... Kumbe usumbukie nini kuwa TAJIRI na huna Mwanamke? Kwani bila Mwanamke utapataje watoto? Maana yake kipato utakachojipimia kwa upeke yako kinakutoshaπŸ™‹πŸ»‍♂
Mwanamke naomba nikuulize;
Kwanini FEDHEHA MNABEBESHWA NINYI NA SIO MWANAUME?
Maana ziko kazi Wanawake na Wanaume wameajiliwa pamoja lakini MWANAMKE ANAONEKANA KAMA CHOMBO CHA KIVUTIO kuliko Mwanaume lakini mnakuta mshahara mmoja lakini wala hamjui ni kwanini?
Najua hamjui Kwanini mapitia kadhia hiyo ila naomba mnielewe kwa ujumbe huu.
Mwanamke akijitambuwa AMEJIKOMBOAπŸ’ͺ🏽
Na kamwe hawezi kudharaulika wala kuonekana kama mtu fulani tu katika jamiii, Yaani tangu uyaanze MAISHA YAKO WEWE NI MTU WA KUTEGEMEA AKILI YA MWINGINE ILI KUISHI sipendi wanawake wa aina hiyo, Hebu niwaambie jambo dogo KILA ALIYE NA BINTI NA AMPE UJASILI MTOTO WAKE ili ajitambuwe na kuijua THAMANI YAKE kamwe hawezi kuishi maisha ya kushikiwa akili
Naongea na wewe Mwanamke ambaye kila kukicha wewe ni MTUMWA WA MAPENZI😭
Juma alipokuja maishani mwako alitaka ufuate ayatakayo yeye, Akaja Hamis nae akataka ya kwake, Peter yeye akasema hapendi skate zako ni fupi ukaendana nae, Akaja John nae hapendi skate ndefu, Wallah mpaka ukazeeke UTAKUWA USHAPITIA MISHONO YOTE YA NGUO lakini hutamuona hata mmoja akiwa na wewe😭
Maana UPENDO WA KWELI HAUTAZAMI MUONEKANO bali ni ROHO iliyoko ndani kusema na aliyeko mbele yako, Mtambue Mwanaume kwa uhalisia ni MBINAFSI ndo maana anapogundua kwamba Uko na muonekano mzuri kwa jinsi unavyojiweka nadhifu anapambana kuuondoa muonekano huo ili USITAZAMWE NA WENGINE ili akutawale vizuriπŸ™†πŸΏ‍♂
Sio jambo baya JE NA YEYE ANASIMAMIA MISINGI YA UTASHI WAKO KWAKE?
Leo hii katika DUNIA yenye utandawazi unakuta Mwanaume anataka Mwanamke wake avae mavazi aina fulani wakati huo huo anakusaliti kwa Mwanamke ambaye anavaa kama ulivyokuwa unavaa wewe kabla hajakutana na wewe JE TATIZO NI MAVAZI AMA UPENDO? Fikeni mahala wafundisheni watoto wakike kujitambuwa na kuwa na MAAMUZI YAO KWENYE MAISHA YOYOTE YALE maana kinyume chake ni yeye kuwa mtumwa kwa mtu ambaye hajui umuhimu wake wala THAMANI YAKE😭
Niseme kwamba MWANAUME MWENYE UPENDO haoni shida kumpa uhuru wa nafsi Mwanamke wake kinyume chake ANAKUWA MTAWALA KWA MAMBO YASOKUWA NDANI YA UWEZO WAKE Kwani mavazi sio tabia wala tabia haitengenezwi na mavaziπŸ‘˜πŸ‘šπŸ‘—πŸ‘’πŸ‘‘πŸ’ΌπŸ‘’πŸ’„
Wanawake zindukeni acheni kutumika kama CHAMBO KWENYE SAMAKI kwamba unakutana na mwanaume anakutamanisha FURAHA NA AMANI na ukimpa nafsi anakugeuka na kuwa MTAWALA kisa kitanzi cha NDOA
Mama zetu waliishi kwa taabu zao chini ya Baba zetu, Dada zetu kadharika kwa shemeji zetu, Ninyi mnapitia taabu kadha wa kadha pamoja na BEIJING YENU... Jiulize usimpompa misingi ya kujitambuwa BINTI WA SASA kesho yake itakuwaje?
Kataa kuwa MZAZI WA MTUMWA baki kuwa MTUMWA kwa UKOMBOZI wa MWANAMKE AJAYEπŸ™‹πŸ»‍♂
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU