-->

NAOMBA NISEME NA WEWE MAMA MWENYE BINTI YAKO

Image may contain: 1 person, standing, outdoor and nature


Wamama msikalili kuwapa mabinti zenu KITCHEN PARTY ili Binti yako akaishi vyema na Mume pamoja na kumjenga kuwa mvumilivu... Ni kweli akavumilie kama ulivyovumilia wewe JE BABA YAKE ANAFANANA TABIA NA MATENDO NA MUMEWE?
Kila bin adam na madhaifu yake kwani HATUJAKAMILIKA ila naomba mtambue jambo moja MATESO ULIYOPITIA WEWE KWENYE NDOA YAKO HAYAWEZI KULINGANA NA MATESO ATAPITIA BINTI YAKO! Pengine wewe umepitia magumu yanayoelezeka ndo maana ukavumilia JE UPO TAYARI KUONA MWANAO AKIKONDA BILA UGONJWA🤷🏽‍♂
Wewe ulijipa uvumilivu huku ukipewa stahiki zako Kama MKE je unajua kwamba wanaume wa siku hizi SIRAHA ZAO NDOA? Mwanao akiishaolewa ujue yeye NDO BABA NDO MAMA Maana yake kipato chake kitampa kuilisha familia yake wala Wanaume wa sasa hawashituki WEWE ULIPITIA HAYO?
Maana ulimjenga kuvumilia sasa Unataka kujua kipi kinamkondesha UNATAKA ASEME LIPI NA TAYARI AMEJENGA UVUMILIVU?
Kuliko kumfundisha Binti yako kwenda kutunza MUME na KUWA MNYENYEKEVU PAMOJA NA UVUMILIVU hebu naomba nikwambie kwamba;
Mjenge binti yako kuwa mwenye FIKRA ili aweze kukabiliana na changamoto ambazo zitakuwa mbele yake💪🏽
Atakapokuwa mwingi wa FIKRA ujue atajua yanayomhusu kuyafanya lakini pia atajua yapi anatakiwa kuyalilia kama BIN ADAM YEYOTE.
Mara zote UVUMILIVU hukuza ugonjwa Kwani muda mwingi utatumia PANADOL ili kupoza maumivu wakati hujajua kiini cha Kwanini KICHWA KINAUMA
Unamfundisha MWANAO akawe mvumilivu kwa MWANAUME MZINZI wakati hata MUNGU amekataa UZINZI na ikibainika anakusaliti PIGA CHINI na kila mmoja abaki na 50 zake🤣🤣
Mwambie Mwanao akavumilie changamoto zinazoelezeka na NDANI YA HAYO KUNA UPENDO PAMOJA NA AMANI🙋🏻‍♂
Mtoto halali akingojea Mume mlevi arudi Usiku wa manane, Mtoto hatulizi MOYO kisa Mwanaume anakuja na Wanawake mbele yake, Mtoto kutwa kupigwa kwa Makosa ambayo Mume kamfanyia BADO UNASEMA AKAVUMILIE?
Hebu uvae uhalisia wa mateso ya MAPENZI n then uone ilivyo ngumu kumwambia UKAVUMILIE MWANANGU
Unapomwambia MWANAO akavumilie Maana yake UNAMFUNGA MDOMO ASIJITETEE je unatarajia Kuna siku atakomboka kwenye mateso ya ndoa yake kama sio ataishi na sauti uliyomsikizisha ya UVUMILIVU? Acha kukatisha ndoto za BINTI YAKO kwa utumwa wako wa FIKRA kwani yahusuyo NAFSI yanahitaji UHURU wa NAFSI💃💃
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🤝🏼
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU