Hiyo itakuletea uponyaji mkubwa katika NDOA yako.
Kwamba Mke anajua upo kazini nina hakika hawezi kuingilia muda huo kwa mambo ya FAMILIA
Ila jikumbushe kwamba anajua muda wako baada ya kazi unaanza saa ngapi BASI REJEA NYUMBANI uwe umechoka na kuudhiwa ofisini hilo ni jukumu la MAMA kuhakikisha kwamba anasimama kwenye eneo lake, Najua atakupumzisha na kukupatia relief kwa hayo yalojiri, Na kwakuwa ni MUDA WA FAMILIA imani yangu ni kwamba utasuuzika, Lakini ikiwa MUDA wa ofisi ni wako na MUDA wa familia nao unaubana niamini UNAUMIZA SANA MOYO WA MKEO
Ziko athali ambazo zinatokana na hali hiyo nazo ni;
▪ MWANAMKE KUWA MPWEKE.
▪ MWANAMKE KUHISI UONEVU.
Rafiki yangu naomba nikwambie kwamba;
Usionyeshe kwa mkeo mambo ambayo yatamletea taswira kwamba HUMHITAJI ni hatari kuliko unavyodhania, Wanawake WANAPENDA Mume ajuaye kumpa MUDA mkewe, Lakini wewe kama unajidai mchapa kazi sana, Ofisini hukumaliza kazi ukabebelea mafile ukafanyie nyumbani UNAMFUNDISHA NINI MKEO?
Kwamba upo BUSY MBABA😅😅😅
Endelea kuwa BUSY ili mkeo atakapokuwa amejiongeza USIJE MLALAMIKIA MTU KATIKA HUKUMU YA MWANAMKE.
Kazi hata uwe mchapakazi kiasi gani ila UKIFA nafasi yako inachukuliwa na mwingine, Lakini nafasi yako katika FAMILIA yako hata ukifa haiwezi kupata mbadala NANI ATAWAZAA WANAO KWA UHALISIA? Nani ndiye atakuwa MUME WA MKEO kama sio atakuja MTULIZA MUWASHO TU?
Ukiisha OA zingatia maana ya NDOA jitahidi kutenganisha majukumu yako, Mpe mkeo MUDA WA KUFURAHIA PAMOJA NAWE
Lakini kama ndo mnajidai kuoa kwa kujinasibu na VYETI VYA NDOA babu ukiona vipi nunua flame ya A4 weka cheti chako humo, ikibidi ipambe sebuleni ila MWANAMKE AKIKUONDOA MOYONI HILO LITABAKI KUWA PAMBO TU😅😅😅
Maana NDOA ya kweli ni MOYO sasa kama MOYONI umeondolewa kumbe hayo makaratasi yanafaa nini?
Kwenye maisha ya NDOA lilia zaidi kuwa ndani ya NAFSI ya MWENZA WAKO kuliko kujiamini kwa mambo ambayo ni NADHARIA
Amani pamoja na Furaha ndizo nguzo kubwa zinazoweza kutoijua DHIKI
Kwa sababu DHIKI nayo imeua NDOA nyingi lakini ikiwa MWENZA ALIZIDIWA NA UNYANYASAJI ila kama Kuna DHIKI pamoja na AMANI PAMOJA NA FURAHA ndoa hiyo iko hai, Napenda ka neno ka Mwanamke wangu pindi zinapokuja DHORUBA;
"Dadie MUNGU ataleta kheri"
Lakini ujue nampa FULL PACKAGE OF LOVE sasa niige Mimi mwenzio najua kupetipeti, Hawa viumbe ni wazuri mno, Mwanamke anatoka kwao Kuna MAISHA YA FAHARI unakuja kumlaza kwenye kunguni🐞 na wala hawasikii?
Ingekuwa wewe ungesinzia? Hivi kunguni🐞 unamjua unamsikia😅😅
Mwanaume mpatie mkeo MUDA WAKE IPASAVYO kinyume cha hapo UKIONA ANAKUPA MGONGO UJUE JUMA AMESHINDA NAE😎
#Elista_Kasema_ila_Sio_She