-->

MRUHUSU MKE WAKO KUKUKATAZA BAADHI YA VITU LAKINI SI KUKUKATAZA KILA KITU!

Mwanadada: DR LOVE
Ni kazi ya mke wako kuangalia mwenendo wako, kukukumbusha kuwa mume wangu sitaki hiki sitaki kile. Ni kazi yake kununa wakai flani kwakua hujamsikiliza. Lakini kamwe! Narudia kamwe! Kamwe! Mwanaume usiwe mtu wa kumsikiliza mke wako kwa kila kitu, anaweza kuwa na akili kukuzidi, anaweza kuwa anaongea ukweli lakini ni lazima wakati mwingine umkatalie baadhi ya mambo tena hata bila sababu ya msingi.
Ukiwa ni mwanaume wa kupelekwa pelekwa, kupigwa marufuku na mke wako basi jua kuwa, mwanzo mke wako atakufurahia, atatamba kuwa mume wangu ananisikiliza kwa kila kitu lakini baada ya muda ataboreka, atakuchoka na ataanza kuona kama kaolewa na dada yake! Atataka kutoka nnje kutafuta mwanaume mwingine. Ni lazima uonyeshe uanaume wako katika nyumba yako, ndiyo ni lazima kila mtu ajue kuwa mwanaume ni nani?
Ninaposema uonyeshe uanaume wako si maanishi kumpiga, kumtuikana au kumnyanyasa, hapana, huo si uanaume! Jifunze tu kukataa baadhi ya mambo tena bila kutoa maelezo. Kwa mfano, anakukataza kila siku sitaki kukuona na flani, inawezekana kweli hiyo rafiki yako ni shida na wewe unajua. Punguza mazoea lakini siku moja kuja naye nyumbani kabisa, na akiongea muambie sitaki kelele zako, mimi ni mtu mzima sipangiwi!
Funga mjadala, tafuta rafiki yake ambaye ni kisirani falani hivi,ambaye unamchikia bila sbabau, hata kama unacmhukia kwakua ana tako kubwa kuliko mkeo, muambie kuwa sitaki kukuona na flani. Siku akilogwa akija naye kwako, toka sebuleni, mshike mkono yule rafiki yake mtoe nnje. Rudi chumbani usitoe maelezo yoyote, chukua simu, ingia kwenye mtandao muache aongee basi mpaka achoke na kupasuka!
Kuna wakati ili wanawake wakuheshimu nilazima uwe kauzu, si kwa kumpiga, kumnyanyasa bali usitabirike. Ufanye kitu bila kujali kama atanuna au atacheka. Kwa mfano, baada ya hii post wengi watatoa povu kusema kuwa Kaka Iddi leo umekosea, unawajaza viburi wanaume. Lakini sitajali, kwakua hata wao wanajua kuwa mwanaume akiwa laini laini, anaendeshwa endeshwa hana maamuzi yake anaboa!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU