-->

MAPENZI NI MATAMU ila tatizo ni........!

Image may contain: one or more people and people sitting
Maana ukijaribu kuyasogelea mapenzi UMENASA na wakati huo huo utaambulia MAUMIVU YA NAFSI wala usipate japo uponyaji wa moyo, Mapenzi yamekuwa kama DAWA YA MAUMIVU yaani kila anae umia anatafuta Mtu wa kumsahaulisha ATOKAKO wala sio kutafuta kiini cha tatizo la kwanini AMEMUACHA?
Wengi wetu wanajaribu MAHUSIANO kuliko KUYATAFAKARI MAHUSIANO! Imekuwa rahisi kuvua nguo na kujaribu kama mtu anafaa kwa sababu ya mahitaji ya mwili kuliko kujiuliza kabla ya kujaribu MAPENZI kisa hakuna atakaye jua kama UMETUMIKA... Utu wa mtu ni STARA sio kwa mwanamke tu ila hata kwa mwanaume kwa sababu HESHIMA YAMPASA MWELEVU LAKINI FEDHEHA NI KWA WAPUMBAVU! Imekuwa kama ULEVI mtu kuingia kwenye mahusiano akijua kabisa ANAPITA TU. Kuna haja ya kila BIN ADAM kukwepa KUJIDHARIRISHA BINAFSI kisa Mapenzi ni siri, Utu wako unaanza na wewe kujitambuwa thamani yako ndipo wengine tuijue thamani yako, Mtu hawezi kudharauliwa ikiwa yeye mwenyewe ANAJIHESHIMU!
Kwepa kuongeza orodha ya WAPENZI kwa kuitafuta AMANI YA MOYO WAKO maana AMANI ni zao la UPENDO utapewaje AMANI ikiwa mtu uliyenae hakupendi?
Niamini nakwambia NGONO IMEKUWA KAMA KIBURUDISHO WAKATI WA NJAA Kwani wengi wanaamini kupata sex ni mbadala wa UHITAJI WA AMANI YA NAFSI.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU