-->

JE TUNAWEZA KUKWEPA MAPENZI?

Image may contain: 1 person, sitting, shoes, child, outdoor and nature
Hapana hatuwezi kuyakwepa Mapenzi kwa sababu moja tu "MAPENZI NDIYO YANAYOIPA DUNIA MABADILIKO"
Mapenzi yana vitu viwili Muhimu;
UHUSIKA.
 KUTOTUMIANA.
Ukiweza kusimamia uhusika kwenye penzi lako huwezi kumuumiza mwenza wako, Usipofikiria kumtumia mwenza wako huwezi kumuumiza, Lakini yote hayo yanayajwa kuwa sehemu ya MAPENZI... Mapenzi ili yawe na nguvu kwenye MOYO wa mwenza wako unawajibika KUMPA PACKAGE YA UPENDO! Package ya upendo ndo nini?
HURUMA
KUSHIRIKI
KUJITOA
URAFIKI
Unapomhurumia Mwenza wako umempa kipaumbele, Unaposhiriki kwenye mambo ya mwenza wako umempa kipaumbele, Ukijitoa kwa mwenza wako maana yake yeye ni kipaumbele chako, Hapa ndipo pagumu kabisa "URAFIKI"
na ndipo palipo na "CREDITS" za kutosha kujenga DHAMANA MOYONI MWA MTU! Kwa hakika ukiweza kuwa rafiki kwa mwenza wako UMEJITWALIA MOYO WAKE na kwa sababu hiyo utakuwa salama sana kwenye penzi hilo, Unajua Kwanini URAFIKI ni kitu chenye nguvu zaidi?
Ukimpa nafasi Mwenza wako akawa rafiki yako maana yake utampa mambo makuu mawili;
MUDA
UHURU
Ukimpa muda maana yake UTAKUWA NAE KWA WAKATI💃
Ukimpa Uhuru maana yake ATAKAPOKUHITAJI UTAKUWEPO💃
Zaidi ya hapo UNATAKA NINI NGW'ANA WANHE?
Kuna wakati naamini MLINZI WA MAPENZI NI MWANAMKE kwa sababu hiyo wenye kuhitaji MUDA NA UHURU NI MWANAMKE... Ukimpa Hivyo vitu Mwanamke UMEJITWALIA AWE WAKO KWA NAFSI YAKE wala hutasumbuka kuishi nae ni rahisi sana, Ila kama Ukiona nakusumbua MNYIME HIVYO VITU MWANAMKE ili ukutane na HASIRA ZAKE.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria💪🏽
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU