-->

THAMANI YA MTU HUJULIKANA PINDI ANAPOKOSEKANA MTU WA KUZIBA PENGO LAKE.

Image may contain: 2 people, people sitting
Kwanza kabisa fahamu hili:-
 USIMUACHE MTU UNAYEMPENDA MAANA YAWEZEKANA AKAKURUDIA ASIWE NA PENDO KAMA LA MWANZO💯
Huwezi kumlazimisha Mtu ajue THAMANI YAKO lakini ni rahisi kwake kuijuwa THAMANI YAKO ikiwa utaondoka kwake, Na kuendelea na maisha yako huku yeye akijiamini atampata zaidi yako, pindi atakapokuwa ametafuta kwa GHARAMA NA NGUVU ZAKE wala asikutane na wakuvuka kiwango chako zaidi anaokutana nao ni VIWANGO VYA CHINI YAKO hapo ndipo mizani⚖️ yake itaweza kubalance vyema ili kuijua THAMANI YAKO.
Kosa kubwa la kumrudia Mtu aliyekuona huna THAMANI ni hili;
 ATAJIONA YEYE NI WA MAANA KULIKO WEWE.
Na hapo ndipo ataweza kupenyeza DHARAU hatarishi na kama hutagundua mapema ITAKUGHARIMU.
Watu wengi wanaishi maisha ya kudharauliana, Unapompenda Mtu yeye anachukulia kama sababu ya wewe kuwa HUNA UJANJA KWAKE na kama hutagundua mapema utajikuta UNASHUSHWA THAMANI YAKO.
Upendo wa kweli hauna MAIGIZO WALA MAJARIBIO bali ni ujenzi wa dhamana ya umoja wenu, Ndo maana Mimi napenda kusema AKIKUONA WA NINI WEWE MUONE HATAKIWI KUWA NAWE kwa sababu kama aliona simfai kumbe leo nafaa kwa lipi anirudie?
Ijue THAMANI yako ili uweze kujiamini, Hivyo ulivyo ndivyo wanahangaika juu yako ila hujui kujitutumua😂😂
Alipoondoka aliacha maumivu moyoni mwako, Mungu akakuvusha halafu leo anaona unapashwa kuwa wake?
Yapo mambo mawili lazima ujue :-
 YEYE ANATAKA AKUACHE YEYE SIO WEWE.
 KULIPIZA MAUMIVU ALIYOPITIA ULIPOMUACHA.
Lakini kama itakuwa alikupenda kwa DHATI basi atakuwa amejutia kukukosa na pengine kapitia magumu ambayo yamampa FUNZO Mpe nafasi nyingine but USIMPE HAKIKA YA IMANI
Maana MAPENZI yana tabia ya KUTAFUTA USHINDI asije kukupa maumivu makubwa zaidi ya hayo ulipitia.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU