Kwanza kabisa UKUBARI KUPENDWA na jingine uwe radhi kumrekebisha Mwenza wako. Njia kuu ya MAPENZI ni kuwa na Mtu ajuaye THAMANI YAKO kinyume cha hilo utakuwa unalazimisha PENDO na gharama ya hilo ni wewe kupoteza nguvu yako mwenyewe hata ukajikuta ukitegemea NGUVU YA MWANAUME kitu ambacho kitakudhoofisha sana.
Nirejee kwenye maana ya MADA YANGU;
Ili Mwanaume akupende ni lazima UMLAZIMISHE AWE NAWE MUDA WOTE hilo litakusababisha kumfanya akuzoee, Mwanaume akikuzoea AMEKUPENDA na kuchomoa hilo hataweza, Hivyo badala ya kwenda KITCHEN PATY kujifunza namna ya kukabiliana na Mwanaume kitandani PAMBANA MWANAUME AKUZOEE ndani ya mazoea ya Mwanaume kumejaa UPENDO na ninajua hilo ndilo hitaji lako, Mwanaume asipokuzoea kamwe hawezi kukupenda, Kwa sababu Mwanaume swala la kubadili Mwanamke kwake ni kipimo cha KAMA ANAKUBALIKA kwa wanawake😅
Sasa ninyi endeleeni kujifunza namna ya kumdhibiti Mwanaume eti sijui mauno mara sijui mnafukiza na udi kwenye nyenyere mkiamini MWANAUME ATATULIA mwajidanganya haswaa, Yapo makabila wanakwenda UNYAGONI na bado wanalilia MAPENZI ije iwe wewe?
Mwanaume anadhibitiwa kwenye MAZOEA hapo hachomoki, Kila mara mfanye awe nawe wallah UTAFURAHIA PENZI HILO😎
#Elista_Kasema_ila_Sio_She