-->
Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts
Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts

SIMULIZI FUPI:CHOCALATE ILOYOUA MTOTO WANGU.

Udaku Specially - Google Groups

Yapata mida ya mchana jua likiwa limetoa ndimi zake kuiramba ramba dunia hapa jijini dar hali ya joto ilikua juu sana.
Nikiwa ni daktari katika hospitali ya Temeke wodi namba tatu ya wanaume, siku hiyo nilichelewa kufanya "AROUND" ya kupitia wagonjwa wa wodi ile mpaka mida ya mchana bado nilikua sijamaliza zoezil lile.
Nilikuja kukatishwa baada ya kufika kwa mgonjwa aliyelala kitanda moja wapo pale wodini nilipomkuta anabubujikwa na machozi yasiyokawaida shuka aliyolalia ilikua imeloa tepetepe.Niliwajua vema wagonjwa waliokua wodi ile lakini yule aliyekua analia alikua mgeni kulazwa huku katundikiwa dripu
Wajibu wangu ulikua ni kujua Analia nini huwenda anasikia maumivu au kuzidiwa, sikuwa na budi kumfata
"shikamoo baba" nilimsalia kwani alionesha kanizidi umri zaidi ya miaka kumi na tano. Hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kulia, Ukiona mwanaumea analia jua kuna jambo.
"Vipi baba unaumwa sana?" nilimuuliza nikiwa naangalia hali ya joto na mapigo ya moyo.
"Daktari naombeni mniruhusu niondoke kwangu" Sauti ya nzito ya kwikwi ikichanganyika na mpandisho wa mafua iliniambia.
"Kwanini tukuruhusu uende nyumbani angali leo ndio umeletwa, Umeambiwa una tatizo gani mpaka Kulazwa" Nilizidi kumuhoji kwani sikuangali faili lake nijue linasemaje.
"Sijaanza kulazwa leo hii ni siku ya tatu Niko hosptali"
"Mbona sijawahi kukuona?"
"Siku mbili zilizopita nilikua nimelazwa hosptali ya mwananyamala lakini wamenifanyia uhamisho leo asubuhi kwa matibabu zaidi katika hosptali yenu."
"nini zaidi?"
"Daktari Chocolate tu ndio imenifanya hivi" Aliposema hayo aliniangalia kidogo akaendele kabla sijamuhoji swali lingine.
" Unaweza kaaa nikakueleza kilichonitokea halafu nambie utanisaidiaje"
Niliangalia kwanza ile wodi kama kuna mgonjwa anayehitaji msaada ndipo nilipokubali kumsikiliza. Sheria ya pale hosptali sio sawa kwa daktari au ndugu wa mgonjwa
mgonjwa kukaa katika kitanda cha mgonjwa lakini nilikua radhi kuvunja sheria ile moyo ukinisikuma kumsikiliza na wala sikujua kwanini labda ni kwa ajili ya uzito wa ile story.
Hakuwa mgonjwa mahututi wa kutotoa sauti ya juu, nilipokaa pembeni yake alianza kunisimulia.
****
MIMI ni mfanyakazi wa TRA tena kitengo kizuri tu.Naishi kinondoni huko ndio nimebahatika kujenga nyumba baada ya kupambana siku nyingi.
Siku zote nimeishi na majirani zangu vizuri nikifurahi nao, nikicheka nao lakini sikujua kwamba maendeleo yangu yataniletea maadui wakubwa kiasi hiki.
Nyumba isiyokua na mwanamke itakua haijakamilika na ni pengo kubwa sana, nikaamua kuoa miaka kadhaa iliyopita.
Tumeishi na mke wangu kwa furaha.Lakini tatizo lilikua kwenye kupata mtoto kwani tulijaribu kipindi cha miaka miwili hatukubahatika kupata mtoto.
Jitihada za kuanza kutafuta suluhisho la tatizo letu likaanza. Na kwa kuwa nikijua napesa tulianza kuzunguka mahosptalini.
Mwishoni tulikuja kuambiwa tatizo liko kwa mke wangu na matibabu ya haraka yanahitajika, kwangu mbele ya pesa sio kitu cha umuhimu kuliko kupata mtoto. Nilikubali na pesa nikatoa matibabu ya yakaanza.
Ilipita miezi kadhaa baada ya matibabu tulipokuja kujaribu tena Kwa baraka za Mungu akashika mimba baada ya miezi tisa tukabahatika kupata mtoto wa kike tukamuita jina la Bahati kutokana na hali yenyewe.
Bahati alikua bahati kweli kwani hakuna alifikiri ipo siku tutakua na MTOTO lakini mungu pekee ndio anaejua.
Bahati akiwa ana miezi mitatu Mama yake akawa anasumbuliwa na tumbo kila mara ikafka sehemu hawezi kunyonyesha kisa kuumwa tumbo.
Nilimrejesha tena Hospatli ile ile tuliyotibiwa awali walipompima tena waligundua ana uvimbe wa kizazi.
Zilikua ni taarifa za kutisha kwetu hasa pale waliposema ili apone huo uvimbe unatakiwa utolewe kwa operesheni kubwa pia na kizazi chake kitatolewa kwani ndio kinachofanya awe na matatizo yote na kisipotelewa anaweza akaja akafa kwa kushikwa na magonjwa mengine ya kizazi.
Halikua wazo rahisi kulikubalia tukafikiri mchana usiku mke wangu akinigomea katu katu kutoa kizazi lakini hali ya tumbo ilipomzidi maumvu hakuwa na budi kufanyiwa operesheni hiyo akatolewa kizazi kuonesha hawezi zaa tena milele.
MTOTO tuliyekua nae ni mmoja WA kipekee malezi tuliyompa ni zaidi ya MTOTO kwani tulijua huyo ndio wa kwanza na wa mwisho.
Bahati alikua kama mmea baada ya kufikisha umri wa miezi nane alikua ashakua mkubwa mkubwa hata mimi baba yake nilikua nawezi kumtembeza.
Hela nilikua nazo lakini sikubahatika kununua gari wala ile nyumba sikuizungushia uzio. Nikawa na mazoea kila ninapotoka kazini jioni namkuta mke na mtoto wangu wako nje nami kwa furaha wote wawili na wabusu nakumchuku mtoto.
Kicheko kikubwa cha bahati kilikua pale ninaporudi kazini nakumchua alichokua anapenda na pia watoto wengi wanapenda ni kumurusha juu kama tulivyozoea wanaume wengi kuwarusha watoto wetu.
Yale mazoea ya kumrusha yalimea yakazidi mpaka akiwa na umri wa mwaka mmoja bado Tabia ya kutoka kazini nikiwakuta nje namrusha bahati sikuiacha.
Nakumbuka ilikua ndio juzi nikiwa njiani nimetoka kazini furha yangu kubwa ilikua ni kufika nyumbani kujumuika na familia yangu.
Nimezoea kusalimiana na kila mtu hakuna mtua ambaye hanijuj pale Kindondini japo nina uwezo wa kifedha sikutaka kuonesha dharau zangu sasa sjui kwanini. wamenifanyia hivi.
Nikiwa nishapita nyumba kadhaa karibu nifike kwangu Mbele yangu nilikutana NA MTOTO WA makamo kati ya miaka mitatu na nusu au minne wa kiume kashika Biskuiti mkononi.
Kalinisalinia tukaposhona lakini kabla sijapiga hatua kadhaa nilisikia kananiita
"Baba! Baba!" nilipogeuka alinioneshea ule mkono aliobeba biskuti
"Naomba nifungulie hii chokleti yangu" Nilitabasamu kidogo kuona mtoto mdogo kama yule anaomba msaada MTU asiyemjua lakini wanasema mtoto ni malaika.
Nilirudi nikamfungulia ile biskuti aina ya chocolate nikataka kumkbidhia lakini alikataa kwa kichwa
"Mama alinifundisha kama mtu akinisaidia kufungua bithikuti nimpe moja kama shukrani yangu, Kwa hiyo na wewe chukua moja" Kiukweli hakuna siku niliyocheka kwa kumuona mtoto mchangamfu na maneno ya kukonga nyoyo kama yule MTOTO.
Sikutaka kubishana nae nikachukua chocolate moja nikamrudishia pakti lake.
Nataka niondoke tena alinishika mkono
"Kula hapa hapa nkuone" hakika alifundishwa na mama yake tabia nzuri. Ujanja ulinishinda japo sikuzoea kula biskuti ya chokleti lakini siku hiyo ilibidi niile mbele yake ndipo akakubali niondokea bila kujua ile chokleti ndani yake ina nini.
Niliendelea NA safari ya kwenda kwangu dalili yoyote ya tukio baya haikuwepo.
Kama kawaida niliwakuta mke na mtoto wangu kibarazani nikafanya kama nilivyozoea kuwabusu wote wawili nikamchukua Bahati mtoto wangu nikana kumrusha juu juu.
Nilimrusha Mara ya kwanza,ya pili huku namchekesha mama yake akifurahia kitendo kile, mara ya tatu na ndio mara ya mwisho kumshika mwanangu, nilipomrusha Mara ya Nne juu Ghafla kwa juu nilpomrushia nikaona giza na kizunguzungu cha ghafla ata kabla mtoto sijamdaka nilijikuta naenda chini fahamu zikanipotea.
Leo hii nilipoletwa hapa Hosptali ndio nimepata nafuu ya kuamka, asubuhi ndugu walikuja kunitembelea wakaniambia habari ambazo zilinifanya niwe nalia toka mda ule mpaka sasa.
Kumbe siku ile wakati nilipoteza fahamu sikuwa ninemdaka mtoto, Kwa bahati mbaya Bahati MTOTO wangu wa kike wakipekee kwa kukosa mtu wakumdaka alidondoka kwa kichwa mpaka kwenye sakafu nakupasuka kichwa.
Hapa ninvyokwambia maneno haya wanafanya mpango wa mazishi ndio maana nimekuomba mniruhusu niondoke nyumbani hata nikaangalia mwili wa mtoto wangu kwa mara ya mwisho.
Inasemakana mwilini kwangu nikikula sumu sasa sumu gani ya aina ile nimekuja kukumbuka huwenda ni ile chocolate ya yule MTOTO katumwa kunifanyia vile bila yeye au mimi kujua na huyo mtu inaonesha anajua fika kuhusu ninavyorudigi na kumbeba
Tatizo ni kuwa nina kumbukumbu za tukio lile lakini sura ya yule mtoto siiumbuki kabisa mpaka sasa.
Kinachoniongezea Mimi machungu mke wangu atakua kwenye hali gani kwa sababu kizazi kashatolewa Tutapata wapi mtoto mwingine sisi.
*******
Alimaliza hiyo story akiwa anapiga kwikwi za kilio.Nilishangaa koti langu la udaktari linadondokewa na maji kuja kujishika usoni at a Mimi nilikua nalia.
Binadamu wa aina gani mwenye kumfanyia mwenzake ubaya kama huo tena kwa kumtuma MTOTO.?
***USIMUAMINI MWANADAMU YOYOTE*******MWISHO***
FUNZO: Mafanikio yako si kila mtu anayependa jaribu kufanya vitu kwa siri bila kuonekana na mwanadamu yeyote
Mwanadamu ni kama kinyonga nje ngozi ya kondooo ndani ana mwili wa MBWA MWITU....
Wengine wanakuchekea machoni lakini wana chuki moyoni. Usisahau kuweka namba nikuunge na group la Simuli za mazixha pia share na like kma zoote
Share:

⚜ *SOMA SIMULIZI HII UJIFUNZE KITU*

USILETE UTANI KATIKA MAPENZI, NARUDIA... - Elimu ya Mahusiano ...
*🌹Binti mmoja ambaye alitokea katika Familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.*
*🌹Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau Kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya Kijijini.*
*🌹Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa Wazazi wake wamefariki na yeye alikua ndiyo Mtoto pekee, hii ni kwa sababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.*
*🌹Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika Kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.*
*🌹Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona Mama yake kwani alikuja bila taarifa.*
*🌹Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.*
*🌹Binti alimdanganya Mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.*
*🌹Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwakua ashamuona mwanae roho yake imetulia kwani hakuenda kukaa pale alienda tu kumuona.*
*🌹Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi Kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.*
*🌹Walimkuta Mama yake akiwa nnje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama asijitambulishe kwao, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.*
*🌹Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta Mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.*
*🌹Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.*
*🌹Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa Mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yake alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka.*
_____________________
*🌹Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nnje wakati yeye anatoka na gari.*
*🌹Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa manane lakini Mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwa ajili yake.*
*🌹Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia Mama yake. Alimtafuta yule Kaka ambaye alimleta Mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.*
*🌹Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye ya pili ilipita bila kumuona Mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.*
*🌹Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge rafiki yake alisema.*
*🌹“Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Bibi ambaye tulimkuta kwako jana?”*
*``Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.*
*Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bodaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.*
*🌹Na mimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale Bibi wa watu mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”*
*🌹Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.*
*🌹Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.*
*🌹Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.*
*🌹Kila siku ilikua mtu wa kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, jambo lililopelekea afukuzwe kazi*.
*Kafukuzwa nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.*
 *Kama kisa hiki kimekugusa na unampenda sana Mama yako, unakumbuka asili yako #SHARE na marafiki zako
Share:

[SIMULIZI] WALLET ILIYOBEBA HADITHI NZURI YA MAPENZI.

Kamati Maalum:Hakupaswi kuwa na ''dating'' kati ya wakristo ...
MAJIRA ya jioni nikielekea nyumbani, macho yangu yaligota kwenye wallet iliyodondoshwa njiani. Niliiokota na kuifungua ndan ili kuona kama kuna vitambulisho vitakavyowezesha kupata namba za mhusika ili nimpigie. Lakini ndani ya wallet mlikuwa na kiasi kidogo tu cha pesa pamoja na barua iliyooneka kuhifadhiwa mle kwa miaka mingi.
Bahasha iliyohifadhi barua ilikuwa shakavu mno; maandishi pekee yaliyoonekana vizuri ni anuani ya makazi ya mtumaji wa barua hiyo. Niliamua kuifungua barua ili kujaribu kutafuta walau dokezo la kusaidia kumpata mhusika. Mshangao wa kwanza ulionikumba baada ya kuifungua, ni tarehe iliyoandikwa barua hiyo: September, 1957. Barua iliandikwa takribani miaka 40 iliyopita.
Mwandiko mzuri wa kike ulipangwa vema juu ya karatasi ya rangi ya buluu, huku kwenye kona ya juu ya karatasi likipachikwa ua zuri jekundu - ua la upendo. Umahiri na utundu wa maneno ya mahaba uliotumika kuandika barua ile, vilinisismua ngozi ya mwili wangu. Mwandishi wa barua ile, ambaye mwishoni alijitambulisha kwa jina la Hudah, alikuwa akilalamika kwa uchungu, akimfahamisha mpenzi wake aitwaye Adrian, kwamba hawatoonana tena kwa sababu mama yake amemkatalia kuolewa, na ameamua kumhamisha. Pamoja na hayo, Hudah alisisitiza kwamba atampenda daima.
Kwakuwa zaidi ya anuani ya makazi iliyoandikwa juu ya bahasha, hapakuwa na mawasiliano mengine, nililazimika kuwapigia watu wa mamlaka za makazi ili kuona kama wanaweza kunisaidia.
Baada ya mhudumu wa simu kupokea nilisema, "Kumradhi, nina ombi binafsi. Ninajaribu kumtafuta mmiliki wa wallet niliyoiokota. Je, kuna namna yoyote ya kupata namba za simu endapo nitakutajia anuani ya makazi iliyoandikwa kwenye bahasha?"
Kwa uzito wa ombi hilo, mhudumu alipendekeza nizungumze na bosi wake, ambaye baada ya kunisikiliza na kusuasua kufanya maamuzi hatimaye alisema, "Sawa, tunayo orodha hapa ya namba za simu kwenye anuani uiliyotaja, lakini siruhusiwi kukupatia." Alinifafanulia kiuadilifu kabisa kwamba, kwa misingi yao ya kazi itabidi yeye ndiye apige namba hizo na kuwasimulia habari ya wallet kisha endapo wataruhusu, ndipo ataniunganisha nao.
Nilisubiri kwenye simu kwa dakika kadhaa. Kisha akarudi hewani na kuniambia: "Kuna mtu nimempata, nafikiri anaweza kukusaidia."
Baada ya kuniunganisha kwa simu na huyo anayehusika na anuani niliyoikuta kwenye bahasha, nilimuuliza kama anamjua mtu aitwaye Hudah. Baada ya kutafakari akajibj, "Ooh, tulinunua hii nyumba kutoka kwa familia iliyokuwa na binti aitwaye Hudah. Lakini hiyo ilikuwa ni miaka karibu 40 iliyopita."
"Unaweza kujua mahala wanakopatikana kwa sasa?" Nilimuuliza.
"Hapana. Ila nachokumbuka, miaka kadhaa iliyopita Hudah alimpeleka mama yake kuhudumiwa na kulelewa kwenye moja kati ya nursing home (taasisi za kuhudumia na kulea wazee)," alinijibu. "Labda ukiwasiliana nao, wanaweza kumpata huyo binti."
Akanipa jina la hiyo taasisi, na papo hapo nikawapigia na kumuulizia mama Hudah. Walinijibu kwamba mama huyo alishafariki miaka kadhaa nyuma, lakini wanazo namba za simu za mahala wanapoweza kunisaidia kumpata Hudah. Niliwashukuru kwa msaada wao, kisha nikapiga hizo namba. Aliyepokea simu, alinijibu kwamba kwa sasa Hudah amekuwa mtu mzima sana, hivyo naye anaishi kwenye taasisi nyingine ya kuhudumia wazee, kama ilivyokuwa kwa marehemu mama yake.
Kufikia hapo, nilianza kujiona mpuuzi kwa kumfuatilia mtu aliyedondosha wallet, isiyokuwa hata na pesa nyingi zaidi ya barua chakavu yenye zaidi ya miaka 40. Pamoja na hayo, nilijaribu kupiga namba za huko anakulelewa Hudah. Aliyepokea simu alisema, "Ndiyo, Hudahh anaishi nasi hapa."
Nikashusha pumzi. Ingawaje ilikwisha kutimu saa nne usiku, niliomba kama wataniruhusu niende kumwona usiku uleule. Walinikubalia. Niliwashukuru na kuanza kuendesha gari yangu hadi hapo kwenye taasisi yao.
Walionilaki baada ya kuwasili ni mlinzi pamoja mhudumu wa zamu. Baada ya kujuliana hali na kujitambulisha, mhudumu alinichukua hadi hadi ghorofa ya pili, tulipomkuta bi mkubwa mmoja akitazama runinga huku akinywa kahawa. Mhudumu alinitambulisha kwake; alikuwa Hudah.
Pamoja na uzee kukaribisha mvi kichwani na makunyanzi usoni, lakini bado tunu ya urembo iliupamba wajihi wake. Baada ya kusalimiana huku akionesha tabasamu na bashasha, nilimsimulia kuhusu wallet niliyoiokota huku nikimwonesha ile barua. Baada ya kuitazama kwa muda barua ile ikiwa na ua lake jekundu kwa juu, Bi Hudah alishusha pumzi kwa nguvu na kufuta machozi yaliyoanza kutengeneza mifereji mashavuni. Mara akasema, "Kijana, barua hii ndiyo iliyotamatimisha mawasiliano yangu na Adrian."
Baada ya ukimya kutanda kwa muda akaendela, "Hakika nilimpenda sana. Lakini wakati huo, nilikuwa na umri wa miaka 16 tu. Hivyo, mama yangu akanikomesha kuwasiliana naye. Ooh, Adrian alikuwa kijana mtanashati na muungwana sijapata kuona ... Aah, Adrian Majumbi ... Kama utabahatika kumpata, mwambie bado nampenda."
Baada ya macho yake kuanza tena kutirirsha machozi, alitulia kidogo akaendelea, "Unajua, tangu kutenganishwa naye sikutaka tena kuolewa, nikiamini sitapata mwingine wa kufanana naye."
Mwisho mazungumzo, nilimshukuru Hudah na kumuaga. Nikaingia kwenye lifti na kuteremka hadi chini. Nikiwa natoka ndani ya lifti, nikamsikia yule mlinzi aliyenipokea mwanzo akinisemesha, "Vipi, bi mkubwa ameweza kukusaidia?"
"Si sana. Lakini walau nimepata jina la mwisho la huyo mmiliki wa wallet hii nimtafutaye. Japo itachukua muda, si kwa sasa tena. Leo nimetumia muda wangu mwingi kumsaka." Nilijibu huku nikiingiza ile wallet kwenye mfuko wa suruali.
"Hey, hebu ngoja kidogo," mlinzi alisema huku mkono na macho yake vikielekea kwenye ile wallet. "Nadhani nimeijua hiyo wallet, itakuwa ni ya mzee Majumbi. Amekwisha idondosha karibu mara tatu humu, na mimi ndiye nimekuwa nikimuokotea, hivyo popote niionapo huitambua, hasa hicho kiji-capet chekundu kwa juu hunisaidia kuijua."
"Ni nani huyo mzee Majumbi?" Haraka nilimuuliza baada ya kukumbuka kuwa nimetajiwa jina hilo pia na bi Hudah.
"Naye ni mzee anayehudumiwa na kuishi hapa. Nina hakika hiyo ni wallet yake, na atakuwa aliidondosha alipokuwa matembezini."
Mungu wangu! Isije ikawa ndiyo huyo ninayemtafuta. Haya kweli yatakuwa maajabu.
Nilimshukuru mlinzi, kisha haraka nilirudi kwa mhudumu wa zamu. Nikamjuza nilichoambiwa na mlinzi. Tukatoka na kuongozana pamoja kwenye lifti na kupanda hadi ghorofa ya tano. Niliendelea kufanya maombi ili huyo mzee awe ndiye mwenyewe. Tulipofika, tulimkuta mzee Majumbi akijisomea kitabu katika chumba cha mapumziko.
Baada ya kuamkiana, mhudumu alimuuliza kama alipoteza wallet yake. Upesi akajipekua mifukoni na kukiri, "Ooh, haipo. Nimeipoteza tena."
"Basi huyu kijana ameikota, akawa anajaribu kukutafuta akiamini ni yako!"
Nilimkabidhi wallet yake. Na mara baada ya kuitupia jicho, alitabasamu na kunishukuru. Alipotaka kunipa pesa kama bahshishi nilikataa. Nikamwambia, "Labda nina jambo moja tu la kukwambia. Nimesoma barua iliyokuwemo kwenye wallet wakati nikijaribu kumjua mmiliki."
Tabasamu lililotamalaki usoni mwake tangu alipopokea wallet yake, liliyeyuka mfano wa theluji iliyowekwa jikoni. "Umeisoma barua?"
"Sikuishia tu kuisoma, bali mpaka nimemtafuta Hudah na kumpata."
"Hudah?!" Mzee Majumbi aliruka kwa mshituko. "Unapajua anapopatikana Hudah? Siamini. Unaweza kunithibitishia urembo ungali maungoni mwake? Tafadhali nipe habari zake."
"Hudah hajambo, nafikiri ukimwona utakubaliana nami kwamba amekuwa mrembo zaidi ya alivyokuwa ujanani," nilijibu huku nimetabasamu.
Mzee Majumbi alitabasamu kwa faraja na kuuliza tena, "Unaweza kunielekeza anapoishi? Ngoja. Nikwambie kitu, kijana? Kipindi napokea barua hii uliyoisoma, nilikuwa nimezama katika bahari ya huba la Hudah. Kama ulivyoona kilichoandikwa humo, kinaweza kumuumiza na kumsambaratisha yeyote aliyezama penzini. Basi ilikuwa hivyo kwangu - nilikataa tamaa na sikuoa tena. Na mpaka hii leo, niliendelea kumpenda yeye tu."
"Mzee Majumbi," nilimkatisha, "tufuatane huku."
Tulitoka na kwenda mpaka kwenye lifti iliyotuteremsha hadi ghorofa ya pili. Kwa sababu ya usiku kuzidi kuwa mkubwa, utulivu ulihanikiza jengo zima. Wengi walikuwa wamelala. Kwa bahati, tulimkuta bi Hudah peke yake akiendelea kuangalia runinga. Mhudumu akamsogelea.
"Bi Hudah," alimwita kwa utulivu, huku akimnyooshea kidole mzee Majumbi. "Unamfahamu huyo mzee?"
Hudah alivua miwani yake taratibu, akamtazama kwa muda mzee Majumbi bila kusema chochote. Hudah akiwa angali ameduwaa, mzee Majumbi alisema kwa sauti isiyo kubwa wala ya kunong'ona, "Hudah - siamini macho yangu. Ni wewe kweli?"
"Mungu wangu! Adrian ni wewe? Ooh, sitaki kuamini. Adrian wangu!"
Walipovamiana na kukumbatiana, mimi na mhudumu tukatoka zetu nje.
"Tazama maajabu ya Mungu," mhudumu aliniambia wakati tukishuka na lifti, "Hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi zake, kwa ufundi na malengo mahsusi."
Nilibaki kimya huku nikitafakari endapo ningeipuuza wallet ile ningetenda kosa kubwa sana. Hakika hatupaswi kupuuza vitu hata kama ni vidogo namna gani.
Takribani wiki tatu baadaye, nikiwa kazini kwangu nilipokea simu toka kwa yule mhudumu: "Tafadhali jitahidi siku ya Jumapili uhudhurie harusi. Hudah na Adrian wanafunga ndoa!"
Salaale!
Naam. Nilihudhuria. Hakika harusi ilifana vilivyo. Wazee wote wanaohudumiwa katika taasisi hiyo walihudhuria wakiwa wamependeza mno. Bi Hudah alionekana mrembo mara dufu akiwa ndani ya shela, huku bwana Adrian akionekana mtashati ndani ya suti yenye rangi ya samawati. Muda huo mimi nikiwa ndani ya suti ya rangi ya hudhurungi, nilisimama pembezoni mwao kama mshenga. Amaa kweli hawakukosea wahenga waliosema "Kama ipo, ipo tu.". Yaani penzi lililopotea miaka takribani hamsini, limechipua upya baada ya wapenzi waliokuwa wakisubiriana, kukutana tena.
Kama hujawahi kuona wapenzi wazee; mume mwenye miaka 70 na mke miaka 65, wakifurahiana na kupendezana kama vijana wa miaka 30, nitafute nikuoneshe picha yao siku ya harusi.
Share:

MY STORY; ALINIPIGA NIKAVUMILIA, NIMESHINDWA KUNYANYUKA KANITELEKEZA!

Iddi Makengo - ACHA KUWA KIAZI, MWANAUME ANAYEJIAMINI ...

Nilijua kama akinioa atabadilika, nilikaa kimya kila siku aliponipiga sikuongea wala kujibu chochote kwani kila mara nikiongea alikua akiniambia kama nimechoka niondoke na nilipomuambia simtaki tena alikuja kuniomba msamaha. Nilipomsamehe alirudia yaleyale, nilichoka na kuondoka lakini sijui kwanini bado kwa ujinga wangu nilirudi.

Kumbuka hapo alikua mpenzi wangu tu lakini alikua akinipiga kama vile ananimiliki. “Mwanangu ana hasira za karibu, mvumilie tu! Sasa wewe nawe ukimuacha unafikiri atapata wapi mwanamke mwingine wa kumuoa!” Mara kwa mara Mama yake aliniambia pale nilipotaka kumuacha mwanae.

Sio mimi nilikua nikimuambia, hapana, ila kila mara nikigombana na Juma alimuambia Mama yake kuongea na mimi. Nakumbuka kipindi hicho nilikua na mimba yake ya miezi mitano, alikua bado hajanioa, tulikua hatuishi pamoja lakini muda mwingi alikua akiutumia kwangu. Nilikua nimechelewa kutoka kazini, kulikua na kikao ofisini na mimi kama mwandishiwa vikao ilikua ni lazima niwepo.

Alikua anaijua kazi yangu lakini alifanya makusudi tu kwanini nimechelewa na kwanini nililetwa na Gari ya Bosi. Akilazimisha kwanini nisingechukua Bodaboda, alishindwa kuniamini nilipomuambia kuwa sio mimi peke yangu nilipelekwa na Gari, wafanyakazi wote tuliochelewa siku ile tulipelekwa na Gari ya Bosi.

Aliniambia kama nampenda kweli niache kazi lakini nilipokataa basi alianza kunipiga bila kujali hali yangu. Kidogo mimba itoke lakini nashukuru Mungu siku ilipita salama. Alinipiga sana na nilimuambia basi, nilitaka kwenda Polisi ndipo alimpigia simu Mama yake ambaye alinituliza akiniambia maneno ya kuonyesha dhahiri alikua upande wa mwanae.

Baada ya hapo nilijikuta na mchukia tu, mwanzoni alikua akinipiga bado nampenda, najipendekeza kwake lakini baada ya kunipiga nikiwa na mimba mapenzi yaliisha kabisa na nilianza kumuona kama takataka flani. Alijitahidi kuniomba msamaha lakini wapi, sikutamani hata kusikia sauti yake, nilishatoa mimba zake nne wakati wote akiniambia hataki kuzaa na mimi.

Hii ya tano sikua tayari kutoa nilijua kufanya hivyo ningeweza hata kupoteza kizazi. Baada ya kuona sina uchangamfu wa kama awali aliniacha, akaendelea na umalaya wake, akitembea na kila rafiki yangu na kila mtu niliyekua namfahamu, mimi sikujali na kwakua nilikua na kazi yangu sikutaka hata kumsumbua.

Hata nilipojifungua alisema hawezi kuja kumuona mtoto, alikua akisingizia si wake lakini kwa mtu aliyemuona pamoja na kuwa alikua wakike lakini alichukua sura yake kama kopi vile. Mama yake alimsihi sana anisamehe turudiane lakini hakua tayari na mimi sikujua hata alitakiwa kunisamehe nini wakati kila siku ndiyo alikua ananikosea kwa kunipiga bila sababu.

Miaka miwili ilipita bila kuja kumuona mtoto, nilianza kuendelea na maisha yangu na nilipata mtu mwingine ambaye alinipenda mimi na mwanangu, alikua akinijali na kunipa kila kitu. Hapo ndipo nilimuona akirudi, alianza kunitafuta akiniambia kuwa hataki mtoto wake alelewe na mwanaume mwingine, aliniomba msamaha na kunisumbua kila siku.

Sikutaka kumsikiliza lakini naye hakutaka kukata tamaa, bila hata kuongea na mimi alituma wazee wake kwetu, kuja kuongea kuhusu ndoa. Alileta posa hata bila mimi kujua, hapo nilianza kuhisi kua labda kweli kabadilika ananipenda hivyo kwa kumuangalia na mtoto niliachana na mpenzi wangu ambaye alikua ananipenda sana na kukubali kuolewa nayeye.

Kweli mambo yalienda vizuri, miezi mitatu ya kwanza ilikua ni ya amani sana, alionyesha kunipenda na kuficha wivu wake. Lakini nilipata ujauzito wapili, hapo ndipo mambo yalibadilika, alitaka niache kazi nilee watoto kwa kisingizio pesa ninayopata ni ndogo hivyo ni kama naenda kufanya umalaya tu huko kazini.

Sikumuelewa niligoma kabisa, hapo ndipo alianza kukasirika, kuchelewa kurudi na kunipiga kukawa palepale. Siku moja kulikua na kikao, nakumbuka kilikua ni kikao cha kamati ya fedha hivyo mimi kama CC nilipaswa kukaa mpaka mwisho. Nilimpigia simu kua kuna kikao lakini alikataa kiniambia nirudi nyumbani na kama ikifika saa mbili sijarudi basi nisirudi tena kwake.

Kusema kweli nilichanganyikiwa kwani kwa hali niliyokua naiona kingefika hata saa nne usiku. Nilimtumia meseji tu kua kikao kikiisha nitarudi kisha nikaendelea na kikao. Usiku kwenye saa nne hivi kikao kikiendelea, nilisikia mngurumo wa gari, mara gari likasimama na nnje nilisikia mzozo kati ya mlinzi na yeye.

Alikua akilazimishia kuingia kwenye kikao kunichukua, alikua akipiga kelele kusema namtaka mke wangu namtaka mke wangu! Nilijua anataka kuniaibisha, harakaharaka nilimfuata Afisa Utumishi nikamuomba kutoka nikimkabidhi makabrasha ya kuandikia mihtasari. Nilitoka kumfuata na kabla ya kusema chochote alianza kunipiga, alinipiga sana aakaniingiza kwenye gari na kunipeleka nyumbani.

Huko alinipiga na mikanda, mateke ya kila sehemu bila kujali kama nilikua na mimba yake au mtoto alikua anaona. Alinipiga sana kisha kunifungia jikoni. Nilikaa huko nikipata mauivu makali mwilini, niliumia sana mpaka kupoteza fahamu, hakurudi mpaka asubuhi, alirudi na kunifungulia akijifanya kukasirika.

Alianza kulalamika kuwa tabia zangu ndiyo zinamfanya kunipiga na kumpandisha hasira zake za karibu. Sikusema chochote ziadi ya kuomba msamaha ili nisipigwe tena. Alijifanya kukubali na kuniambia niamke nikamuandalie Chai. Nilijaribu kunyanyuka lakini nilishindwa, nilikua siisikii miguu yangu.

Yeye aliona kama kiburi mpaka aliponishika kuninyanyua lakini nilikua mzito, mwili hauna nguvu, na wala sikua na maumivu yoyote kuanzia kiunoni kushuka chini. Alijaribu kuninyanyua tena na tena lakini wapi. Sikujua kinachoendelea lakini nahisi yeye alihisi kitu kwani alininyanyua na kunipeleka kwenye gari.

Alinichukua na kunipeleka Hospitalini, kule alisema kuwa nimeanguka kwenye ngazi lakini Daktari hakuamini, ila sijui alifanya nini nikaanza kutibiwa hivyo hivyo bila PF3. Hapo ndipo nilipewa habari mbaya, nilikua nimevunjika sehemu ya uti wa mgongo na nisingeweza kutembea tena katika maisha yangu.

Kwangu ilikua ni kama msiba, nilishindwa kuamini lakini ilikua hivyo, ndugu zangu walikasirika na kukasirika lakini haikusaidia. Walitaka kumpeleka Polisi lakini nilikataa nikiwaambia haitanisaidia kutembea. Nilikaa Hospitalini kama mwezi mmoja hivi kuona kama kutakua na mabadiliko lakini wapi, ilikua hivyo nilishakua mlemavu na ilibidi tu kukubaliana na hali yangu.

Nilirudi nyumbani na kuwa mtu wa kusaidiwa kila kitu. Mwezi mmoja tu baada ya mimi kutoka Hospitalini aliniambia anataka kunirudisha kwetu kwani yeye hawezi kunihudumia tena, hawezi kuishi na mwanamke mlemavu, nilijaribu kumuambia yeye ndiyo kanisababishia lakini alisema haitasiadia, hata kama ni yeye lakini hawezi kuishi na mimi tena.

Nilijua utani lakini alileta mwanamke mwingine nikiwa mulemule ndani na siku iliyofuata alinichukua na kuja kunitelekeza kwa Mama yangu na mwanangu, mimba ile ilishatoka siku aliponipiga. Ni mwaka sasa hajapiga hata simu ya kunijulia hali, pesa ya matumizi ya mtoto anatuma tu kwa simu hata kuongea na mtoto hawezi.

Sasa hivi nipo tu nyumbani sina kazi sina hili wala lile naishi tu na Mama yangu ambaye naye ni mzee naona anavyppata shida kunihudumia. Nimeandika kisa changu ili wanawake wenzangu mjifunze, mimi yameshatokea siwezi badilisha kitu ila kwako wewe ambaye unapigwa na unaona kama ni kitu cha kawaida unaweza kuabdilika sasa.

Unaona kama ana hasira za karibu nikuambie tu kuwa hana haki ya kukupiga na wewe si lazima kuvumilia mateso. Nibora kuondoka ukiwa na miguu yako miwili na nguvu zako kuliko kusubiri mpaka hali ikufike kama mimi. Nilijipa moyo atabadilika nasikia kabadilika kweli mkewe mpya hampigi lakini mimi nimepata faida gani ya kubadilika kwake?

Najua umenielewa sidhani kama utaendelea kuvumilia kupigwa ukisubiri kuwa mlemavu kama mimi!

****MWISHO;

Share:

MY STORY; MKE WANGU MRUHUSU MAMA YANGU AKUNYANYASE!

maisha_na_mahusiano18 Instagram posts, stories and followers ...
“Mruhusu Mama yangu akunyanyase, muache awe na kisirani, muachea kutukane, kwani akiikuambia kuwa hujui kupika inakupunguzia nini, muche kama akitaka aingie jikoni, haikupounguzii chochote, mimi ndiyo nimekuoa, najua utamu wako, najua napata nini na najua ni kwanini nimekuoa. Yule ni Mama yangu, siwezi kumfanya chochote, siwezi kumpiga, siwezi kumbadilisha, najua unatamani niongee nayeye, lakini ana miaka 69.
Hivi unadhani kuna kitu gani nitamuambia ili abadilike, ishdnai kama Mama anakuchukia, nadhani Mama anchukia maisha yake, wakati nakua kuna vitu nilikua navipenda, walikua wanagombana kila siku na Baba alikua ni mtu wa kumdhalilisha sana Mama, alikua anampiga wkaati mwingine. Ingawa Mama alikua hasemi na walikua hawajawahi kunionyesha lakini najua, nilikua naona.
Mama yangu ni mti mzima, Baba kashafariki, hana mtu wa kuishinaye, ana Kisukari, ana Presha, siwezi kumuacha aishi peke yake, mimi ndiyo mtoto wa pekee kwetu, siwezi kumuacha Mama yangu kwenda kuishi ukweni, dada zangu wameolewa, sasa unafikiri mimi nirtafanya nini? Najua unaumia, najua una hasira, lakini hembu anza kumchukulia Mama yangu kama mgonjwa, mchukulie kama mtu mwenye mawazo yake, amabye ana matatizo ya akili, muache atukane, alalamike.
Jishushe, omba msmaaha na wakati mwingine nikilazimika kukugombeza mbele yake basi jifanye kulia, jifanye kuumia, tukirudi chumbani cheka. Nakuaomba unisaidie hilo mke wangu, nakuomba sana kwakua wewe ndiyo kila kitu kwangu, tuna watoto, ukiondoka unafikiri itakuaje, ukija ukiniambia Mama hivi Mama vile unafikiri nitafanya nini? Naomba niruhusu nimridhishe Mama yangu, amalize uzee wake nipate radhi yake na niwe na amani na wewe?”
Nilimuambia mke wangu ambaye alikua akilia, alikua amemaliza kupika na kutukaribisha chakula mezani, lakini Mama aligoma kula, akaingia jikoni na kujipikia mwenyewe, aliongea maneno mabaya kwa mke wangu, nilijaribu kusihi Mama kunyamaza lakini kila nilipokua nikiongea ndivyoa likua akikasirika, Alianza kulalamika kuwa nampenda mke wangu kuliko yeye, ninataka afe na maneno kibao,kwa alivyokua akilalamika huku akilia kusema kweli nilishindwa kabisa cha kufanya, nilijikuta nakaa kimya.
Hata chakula alichopika mke wangu nilishindwa kabisa kula kwani mama hakutaka nile. Mke wangu naye alikasirika kwani haikua mara ya kwanza, ilikua ni kawaida Mama yangu kumnyanyasa mke wangu, nilishajaribu kumuelewesha mke wangu ila kila siku niliona kama anaumia. Mama ndiyo nilishchoka kumuambia, nilikua katika wakati mgumu sana, kuchagua kati ya mke wangu, Mama wa watoto wangu na Mama yangu mzazi.
“Nimechoka mume wangu, kibaya ananitangaza kwa watu, dada zako wananichukia, wanaona kama na mnyanyasa Mama yao…” Alianza kulalamika.
“Shhhhhh… ishia hapo hapo, Dada zangu hawahusiki kitu hapa, wakuchukie, wasikuchukie sijali, sina kazi ya kuwaridhisha, wapambane na ndoa zao, shida yangu ni Mama nataka umuelewe. Mama yangu anadai umeniloga, umenikalia kichwani,a na maumivu yake, maumivu ya ndoa yake, lakini mimi najau nafanya nini.
Wewe nataka tupange maisha na tumchukulie Mama kama mgonjwa wetu na Mama tumridhishe tu, tumpe kamaani kuwa aananiendesha yeye na si wewe unayeniendesha. Ngoja nikuonyeshe.” Nilinyanyuka na kwenda kwenye Begi langu, nilitoa Document mbili, nikamuonyesha mke wangu.
“Unakumbuka kile kinja ambacho nilinunua, nikaandika jina la Mama?” Nilimuuliza, nakumbuka kilileta shida sana lakini niliamua kuandika jina la Mama kwenye karatasi ya mauziano na mke wangu akawa kama shahidi tu.
“Hati yake hii hapa, angalia ina majina ya nani?” Nilimuonyesha mke wangu, kilikua na jina langu na lake, mimi na mke wangu, alishangaa na kuniuliza ilikuje aliandika jina la Mama yake na kwanini kabadilisha.
“Kila kitu nimefanya hivyo, kuna zile Document nilikuambia usaini siku zile, zilikua ni hati za viwanja, niliamua kufanya hivyo kuwa nitakusuprise ili ujue mimi nafanya nini? Mama yangu ana makaratasi tu ambayo yana majina yake, ambayo hata yamesiniwa na wmenyekiti wkatai wewe una hati ambayo inatoka wizarani. Tena hayo amakaratasi nilimuonyesha tu Mama illi ajue hujanikalia,a ridhike, aone kuwa ndiyo ananiendesha, alkini nilishayachoma moto muda mrefu.
Wewe ndiyo mke wangu, nikifa leo ni wewe utawalea wanangu, hivi kweli kwa akili za kawaida, Mama yeye wmenyewe hawezi kujilea halafu nimuachie wanangu, atawafanya nini, ili dada zangu waje kuchukua mali zangu na kuwapelekea waume zao, hapana, kila kitu mpaka kwa mwanasheria wangu nikiondoka mimi unafuatia wewe si Mama, si Dada wala nani.
Naomba tu unisaidie, ili tuwe na amani ni lazima Mama aamini kuwa hujanikalia na yeye ndiyo kila kitu. Kama hakupigi mpuuzie, muache aongee, sikiliza, omba misamaha, jishushe basi, huna haja ya kushindana na Mama yangu, wewe ni Mke, yeye ni Mama, kwanini mshindane, kila mmoja nampenda kwa nafasi yake.
Nilimuambia mke wangu na alinielewa, Mama yangu hakubaidliak, alikua na hasira na mke wangu, alikua hamuamini lakini mke wangu alibadilika, aliendelea kumpenda Mama yangu, aliendelea kumjali, alimhudumia mpaka siku ya mwisho wa uhai wake. Mama alikua akiamini kuwa mke wangu simpendi, namnyanyasa na namsikiliza yeye tu.
Lakini siku ambayo Mam ayangu anafariki dunia, nilikua hospitalini, mke wangu ndiyo alikua ametoka kumnywesha maziwa kwani hata kula ilikua shida. Alitapika na kugoma kunywa tena, kisha aliniita kutaka kuongea na mimi. Nameno yake ya mwisho yalikua “Mwanangu nakufa, mshike huyo mwanamke, ana tabia nzuri sana, yaani mshike huyo mwanamke hutakuja kuteseka katika maisha yako.
Mwanzo nilikua simpendi lakini umeoa mwanangu, kama nikisikia umemuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine basi nahisi nitageuka nikiwa kaburini, usimuache, ni Mama bora na mwanamke akiweza kuwa Mama basi anakua mke bora. Kuna vile viwnaja vyangu ulininunulia nataka umpe kimoja, viwili baki navyo kimoja mpe yeye….”
Kusema kweli nilishangaa, Mama ambaye tangu kuoa alikua hamtaki mke wangu lakini maneno yake ya mwisho kwangu aliniambia kuwa nimshikilie mke wangu nisije kumuacha. Baada ya kumaliza kuongea aliniambia nimuite mke wangua mnyweshe maziwa tena, nilimuita, lakini Mama alifia mikononi mwa mke wangui, akiwa amempakata anamnyesha maziwa. Ni mwkaa sasa umepita lakini bado maneno hayajanitoka kcihwani.
Picha ya mwisho kichwani kwangu, kumbukumbu ya mwisho ya Mama yangu kichwani kwangu ni ya mke wangu akiw aamempakata Mama yangu. Hata dada zangua mabao Mama likua anawapenda sana, anawasifia na kuwaona wamaana hawakuepo eneo la tukio kumhudumia kwakua tu mmoja alikua kazini, mwingine alinyimwa ruhusa na mume wake na mwingine alikua kasafiri kwakua Mama mkwe wake alikua naye anaumwa.
Leo mke wangu alikua ananishukuru kwa kumuambia aruhusu Mama yangu amnyanyase, nikakumbuka kuwa kuna watu wengi ambao wanashindwa kuchagua kati ya Mama na mke, ushauri wangu, hutakiwi kuchagua, kila mtu ana nafasi yake. Huwezi kumbadilisha Mama yako ila naamini kama ukiongea na Mke wako, ukampa moyo na ukamfundisha naman ya kushi na Mama yako basi utakua na ndoa yenye amani. Hutakiwi kuchagua kwani hakuna mwneye ubora zaidi ya mwenzke bali kila mmoja ana nafasi yake.
MWISHO
Share:

SIMULIZI FUPI... NIMEJIFUNZA KUOLEWA NI MAAMUZI YA MWANAUME SIO MIMI KUTAKA WALA KUMTUMIA MAMA YAKE JIFUNZE NILICHOKIPITIA USITESEKE!

Nina umri Wa miaka 25 nimekuwa kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye naona sasa nimuache tu aendelee na Mipango yake, Nilikutana na Shedrack mwaka 2017 January lakini ninavyokueleza sijawahi kufurahia uhusiano wetu kama watu wengine, nakumbuka ule mwezi Wa kwanza alianza kuonyesha Upendo tulitoka out Mara moja , basi kuelekea mwezi mwingine akaanza ubusy, nikawa navumilia kulingana na Kazi yake, ilimpasa kwenda mkoa kwa miezi sita, binafsi nilimmkumbuka mno, na ukweli hakuna mwanaume nimewahi kumpenda duniani kama Sheddy huyu ni mwanaume wangu Wa kwanza kumpenda katika Maisha yangu sikuwahi kuwaza kuja kuwa na uhusiano na wanaume tofauti tofauti mpaka kumpata Mr right wangu, niliamini Sheddy ndio mwanaume Wa kwanza na Wa mwisho, UZURI Wa sura na rangi yake na umbo lake umekuwa ukinifanya kipofu yani nikawa nahisi siwezi kumuacha mwanaume kama huyu no matter what nitapambana navyoweza, miezi sita ilipoisha alirudi tukonana kwa Mara ya pili! Lakini ilikuwa ni ubungo ilibidi Mimi nimfosi kwenda kumpokea basi akanikubalia shingo upande tulifanikiwa kukaa sehemu pale sheli ubungo nikanunua lunch nk yeye hakutaka kukaa hata yani kila kitu nilikuwa nalazimisha Mimi, hali hii imekuwa ndio maisha yetu, nakatiwa simu, Mara sipigiwi simu wiki hadi wiki mbili mpaka nimtafute, simunyake sishiki wala kuuliza anaongea na nani, basi siku hiyo ndiyo siku nikaweza kumshawishi akanipatia no ya mama yake mzazi na shangazi yake yupo mkoani ambapo ndipo natokea, nikaanza mawasiliano na mama mkwe na shangazi yake RASMI!
Niliwasiliana na yule mama kila siku kila dakika nilifanya vile nikijua Sheddy ni mtoto pekee Wa Kiume Wa yule mama kati ya watoto watatu wawili Wa kike, jambo nililokuja kugundua hakuna Dada yake hata mmoja aliyenipenda, Mara ya kwanza ilinisumbua nikawa nawanunulia vitu vitu baadae nikachoka kwanza walikuwa ni mapacha halafu wapo sekondari boarding, hivyo nguvu yangu nikaihamishia kwa mama, nilikuwa napeleka kila aina ya vitenge vinavyoingia, pesa natuma, vocha naweka, Nguo za dukani namfungia namtuma mtu anapeleka nimefanya hivi kwa miezi sita, nikiamini mama atanikingia kifua mwanae anioe . mpaka tumeingia mwaka huu January ndipo nikakutana na post yako Moja ile ya ACHA KUJITUPA HOVYO nilijiona ni mpumbavu sana kwa sababu hii hapa!
Naukumbuka kuna siku nilikuwa nikichat na Sheddy akaniambia hawezi kusubiria mpaka ndoa nilipomuhoji akitaka Tuoane lini alisema 2019 January, nikamtia moyo awe na NGUVU ya kunisubiria , nikawa namsalia asiingiwe tamaa, japo naye ni mpendwa mwenzangu, kuna siku alipiga simu akaniambia tusionane tena mpaka ndoa maana akiniona atashawishika kufanya ngono na Mimi nikamwambia sawa, jioni akanipigia simu amenimisi ukweli nami nilimiss anasema niende kwake nikamuone tukakutana tunafanya siri mama yake asijue nikaenda naukumbuka usiku huo, niliamua kulala naye nikiamini uhusiano wetu utakuwa IMARA , baada ya siku tatu simu zake zikawa hazipatikani , nikampata siku ya nne akanijibu tu kifupi "Lisa usinipigie simu wala kunitafuta, sijawahi kukupenda niliongozwa na tamaa tu namngoja nitakayempenda naomba uwe huru kutafuta mwingine! Sorry!
Nilitafakari na kuchanganyikiwa, nilipomtafuta mama yake, alikuwa akiongea na Mimi kama hataki vile nilipomuhadithia akaniambia tu asante kwa yote uliyowahi kunifanyia,Mungu atakupa mwingine akakata simu, nililia kama mtoto niliona huu mwaka ni mchungu, mwezi Wa pili ukapita bado Nina maumivu nikaanza kuhudhuria maombi, angalau ikasaidia navyokuambia tarehe mbili mwezi huu Wa nne nimeingia Facebook namuona Sheddy na wadogo zake Wa kile na mama yao pamoja na Msichana mmoja mzuri sana wamepiga Picha kwako Sheddy akaandika nikiwa na mwanamke Wa Maisha yangu, mama yangu na wadogo zangu! Huwezi amini Esther niliblock wote,.
SHARE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU