-->

SIMULIZI FUPI... NIMEJIFUNZA KUOLEWA NI MAAMUZI YA MWANAUME SIO MIMI KUTAKA WALA KUMTUMIA MAMA YAKE JIFUNZE NILICHOKIPITIA USITESEKE!

Nina umri Wa miaka 25 nimekuwa kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye naona sasa nimuache tu aendelee na Mipango yake, Nilikutana na Shedrack mwaka 2017 January lakini ninavyokueleza sijawahi kufurahia uhusiano wetu kama watu wengine, nakumbuka ule mwezi Wa kwanza alianza kuonyesha Upendo tulitoka out Mara moja , basi kuelekea mwezi mwingine akaanza ubusy, nikawa navumilia kulingana na Kazi yake, ilimpasa kwenda mkoa kwa miezi sita, binafsi nilimmkumbuka mno, na ukweli hakuna mwanaume nimewahi kumpenda duniani kama Sheddy huyu ni mwanaume wangu Wa kwanza kumpenda katika Maisha yangu sikuwahi kuwaza kuja kuwa na uhusiano na wanaume tofauti tofauti mpaka kumpata Mr right wangu, niliamini Sheddy ndio mwanaume Wa kwanza na Wa mwisho, UZURI Wa sura na rangi yake na umbo lake umekuwa ukinifanya kipofu yani nikawa nahisi siwezi kumuacha mwanaume kama huyu no matter what nitapambana navyoweza, miezi sita ilipoisha alirudi tukonana kwa Mara ya pili! Lakini ilikuwa ni ubungo ilibidi Mimi nimfosi kwenda kumpokea basi akanikubalia shingo upande tulifanikiwa kukaa sehemu pale sheli ubungo nikanunua lunch nk yeye hakutaka kukaa hata yani kila kitu nilikuwa nalazimisha Mimi, hali hii imekuwa ndio maisha yetu, nakatiwa simu, Mara sipigiwi simu wiki hadi wiki mbili mpaka nimtafute, simunyake sishiki wala kuuliza anaongea na nani, basi siku hiyo ndiyo siku nikaweza kumshawishi akanipatia no ya mama yake mzazi na shangazi yake yupo mkoani ambapo ndipo natokea, nikaanza mawasiliano na mama mkwe na shangazi yake RASMI!
Niliwasiliana na yule mama kila siku kila dakika nilifanya vile nikijua Sheddy ni mtoto pekee Wa Kiume Wa yule mama kati ya watoto watatu wawili Wa kike, jambo nililokuja kugundua hakuna Dada yake hata mmoja aliyenipenda, Mara ya kwanza ilinisumbua nikawa nawanunulia vitu vitu baadae nikachoka kwanza walikuwa ni mapacha halafu wapo sekondari boarding, hivyo nguvu yangu nikaihamishia kwa mama, nilikuwa napeleka kila aina ya vitenge vinavyoingia, pesa natuma, vocha naweka, Nguo za dukani namfungia namtuma mtu anapeleka nimefanya hivi kwa miezi sita, nikiamini mama atanikingia kifua mwanae anioe . mpaka tumeingia mwaka huu January ndipo nikakutana na post yako Moja ile ya ACHA KUJITUPA HOVYO nilijiona ni mpumbavu sana kwa sababu hii hapa!
Naukumbuka kuna siku nilikuwa nikichat na Sheddy akaniambia hawezi kusubiria mpaka ndoa nilipomuhoji akitaka Tuoane lini alisema 2019 January, nikamtia moyo awe na NGUVU ya kunisubiria , nikawa namsalia asiingiwe tamaa, japo naye ni mpendwa mwenzangu, kuna siku alipiga simu akaniambia tusionane tena mpaka ndoa maana akiniona atashawishika kufanya ngono na Mimi nikamwambia sawa, jioni akanipigia simu amenimisi ukweli nami nilimiss anasema niende kwake nikamuone tukakutana tunafanya siri mama yake asijue nikaenda naukumbuka usiku huo, niliamua kulala naye nikiamini uhusiano wetu utakuwa IMARA , baada ya siku tatu simu zake zikawa hazipatikani , nikampata siku ya nne akanijibu tu kifupi "Lisa usinipigie simu wala kunitafuta, sijawahi kukupenda niliongozwa na tamaa tu namngoja nitakayempenda naomba uwe huru kutafuta mwingine! Sorry!
Nilitafakari na kuchanganyikiwa, nilipomtafuta mama yake, alikuwa akiongea na Mimi kama hataki vile nilipomuhadithia akaniambia tu asante kwa yote uliyowahi kunifanyia,Mungu atakupa mwingine akakata simu, nililia kama mtoto niliona huu mwaka ni mchungu, mwezi Wa pili ukapita bado Nina maumivu nikaanza kuhudhuria maombi, angalau ikasaidia navyokuambia tarehe mbili mwezi huu Wa nne nimeingia Facebook namuona Sheddy na wadogo zake Wa kile na mama yao pamoja na Msichana mmoja mzuri sana wamepiga Picha kwako Sheddy akaandika nikiwa na mwanamke Wa Maisha yangu, mama yangu na wadogo zangu! Huwezi amini Esther niliblock wote,.
SHARE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU