-->

MY STORY; MKE WANGU MRUHUSU MAMA YANGU AKUNYANYASE!

maisha_na_mahusiano18 Instagram posts, stories and followers ...
“Mruhusu Mama yangu akunyanyase, muache awe na kisirani, muachea kutukane, kwani akiikuambia kuwa hujui kupika inakupunguzia nini, muche kama akitaka aingie jikoni, haikupounguzii chochote, mimi ndiyo nimekuoa, najua utamu wako, najua napata nini na najua ni kwanini nimekuoa. Yule ni Mama yangu, siwezi kumfanya chochote, siwezi kumpiga, siwezi kumbadilisha, najua unatamani niongee nayeye, lakini ana miaka 69.
Hivi unadhani kuna kitu gani nitamuambia ili abadilike, ishdnai kama Mama anakuchukia, nadhani Mama anchukia maisha yake, wakati nakua kuna vitu nilikua navipenda, walikua wanagombana kila siku na Baba alikua ni mtu wa kumdhalilisha sana Mama, alikua anampiga wkaati mwingine. Ingawa Mama alikua hasemi na walikua hawajawahi kunionyesha lakini najua, nilikua naona.
Mama yangu ni mti mzima, Baba kashafariki, hana mtu wa kuishinaye, ana Kisukari, ana Presha, siwezi kumuacha aishi peke yake, mimi ndiyo mtoto wa pekee kwetu, siwezi kumuacha Mama yangu kwenda kuishi ukweni, dada zangu wameolewa, sasa unafikiri mimi nirtafanya nini? Najua unaumia, najua una hasira, lakini hembu anza kumchukulia Mama yangu kama mgonjwa, mchukulie kama mtu mwenye mawazo yake, amabye ana matatizo ya akili, muache atukane, alalamike.
Jishushe, omba msmaaha na wakati mwingine nikilazimika kukugombeza mbele yake basi jifanye kulia, jifanye kuumia, tukirudi chumbani cheka. Nakuaomba unisaidie hilo mke wangu, nakuomba sana kwakua wewe ndiyo kila kitu kwangu, tuna watoto, ukiondoka unafikiri itakuaje, ukija ukiniambia Mama hivi Mama vile unafikiri nitafanya nini? Naomba niruhusu nimridhishe Mama yangu, amalize uzee wake nipate radhi yake na niwe na amani na wewe?”
Nilimuambia mke wangu ambaye alikua akilia, alikua amemaliza kupika na kutukaribisha chakula mezani, lakini Mama aligoma kula, akaingia jikoni na kujipikia mwenyewe, aliongea maneno mabaya kwa mke wangu, nilijaribu kusihi Mama kunyamaza lakini kila nilipokua nikiongea ndivyoa likua akikasirika, Alianza kulalamika kuwa nampenda mke wangu kuliko yeye, ninataka afe na maneno kibao,kwa alivyokua akilalamika huku akilia kusema kweli nilishindwa kabisa cha kufanya, nilijikuta nakaa kimya.
Hata chakula alichopika mke wangu nilishindwa kabisa kula kwani mama hakutaka nile. Mke wangu naye alikasirika kwani haikua mara ya kwanza, ilikua ni kawaida Mama yangu kumnyanyasa mke wangu, nilishajaribu kumuelewesha mke wangu ila kila siku niliona kama anaumia. Mama ndiyo nilishchoka kumuambia, nilikua katika wakati mgumu sana, kuchagua kati ya mke wangu, Mama wa watoto wangu na Mama yangu mzazi.
“Nimechoka mume wangu, kibaya ananitangaza kwa watu, dada zako wananichukia, wanaona kama na mnyanyasa Mama yao…” Alianza kulalamika.
“Shhhhhh… ishia hapo hapo, Dada zangu hawahusiki kitu hapa, wakuchukie, wasikuchukie sijali, sina kazi ya kuwaridhisha, wapambane na ndoa zao, shida yangu ni Mama nataka umuelewe. Mama yangu anadai umeniloga, umenikalia kichwani,a na maumivu yake, maumivu ya ndoa yake, lakini mimi najau nafanya nini.
Wewe nataka tupange maisha na tumchukulie Mama kama mgonjwa wetu na Mama tumridhishe tu, tumpe kamaani kuwa aananiendesha yeye na si wewe unayeniendesha. Ngoja nikuonyeshe.” Nilinyanyuka na kwenda kwenye Begi langu, nilitoa Document mbili, nikamuonyesha mke wangu.
“Unakumbuka kile kinja ambacho nilinunua, nikaandika jina la Mama?” Nilimuuliza, nakumbuka kilileta shida sana lakini niliamua kuandika jina la Mama kwenye karatasi ya mauziano na mke wangu akawa kama shahidi tu.
“Hati yake hii hapa, angalia ina majina ya nani?” Nilimuonyesha mke wangu, kilikua na jina langu na lake, mimi na mke wangu, alishangaa na kuniuliza ilikuje aliandika jina la Mama yake na kwanini kabadilisha.
“Kila kitu nimefanya hivyo, kuna zile Document nilikuambia usaini siku zile, zilikua ni hati za viwanja, niliamua kufanya hivyo kuwa nitakusuprise ili ujue mimi nafanya nini? Mama yangu ana makaratasi tu ambayo yana majina yake, ambayo hata yamesiniwa na wmenyekiti wkatai wewe una hati ambayo inatoka wizarani. Tena hayo amakaratasi nilimuonyesha tu Mama illi ajue hujanikalia,a ridhike, aone kuwa ndiyo ananiendesha, alkini nilishayachoma moto muda mrefu.
Wewe ndiyo mke wangu, nikifa leo ni wewe utawalea wanangu, hivi kweli kwa akili za kawaida, Mama yeye wmenyewe hawezi kujilea halafu nimuachie wanangu, atawafanya nini, ili dada zangu waje kuchukua mali zangu na kuwapelekea waume zao, hapana, kila kitu mpaka kwa mwanasheria wangu nikiondoka mimi unafuatia wewe si Mama, si Dada wala nani.
Naomba tu unisaidie, ili tuwe na amani ni lazima Mama aamini kuwa hujanikalia na yeye ndiyo kila kitu. Kama hakupigi mpuuzie, muache aongee, sikiliza, omba misamaha, jishushe basi, huna haja ya kushindana na Mama yangu, wewe ni Mke, yeye ni Mama, kwanini mshindane, kila mmoja nampenda kwa nafasi yake.
Nilimuambia mke wangu na alinielewa, Mama yangu hakubaidliak, alikua na hasira na mke wangu, alikua hamuamini lakini mke wangu alibadilika, aliendelea kumpenda Mama yangu, aliendelea kumjali, alimhudumia mpaka siku ya mwisho wa uhai wake. Mama alikua akiamini kuwa mke wangu simpendi, namnyanyasa na namsikiliza yeye tu.
Lakini siku ambayo Mam ayangu anafariki dunia, nilikua hospitalini, mke wangu ndiyo alikua ametoka kumnywesha maziwa kwani hata kula ilikua shida. Alitapika na kugoma kunywa tena, kisha aliniita kutaka kuongea na mimi. Nameno yake ya mwisho yalikua “Mwanangu nakufa, mshike huyo mwanamke, ana tabia nzuri sana, yaani mshike huyo mwanamke hutakuja kuteseka katika maisha yako.
Mwanzo nilikua simpendi lakini umeoa mwanangu, kama nikisikia umemuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine basi nahisi nitageuka nikiwa kaburini, usimuache, ni Mama bora na mwanamke akiweza kuwa Mama basi anakua mke bora. Kuna vile viwnaja vyangu ulininunulia nataka umpe kimoja, viwili baki navyo kimoja mpe yeye….”
Kusema kweli nilishangaa, Mama ambaye tangu kuoa alikua hamtaki mke wangu lakini maneno yake ya mwisho kwangu aliniambia kuwa nimshikilie mke wangu nisije kumuacha. Baada ya kumaliza kuongea aliniambia nimuite mke wangua mnyweshe maziwa tena, nilimuita, lakini Mama alifia mikononi mwa mke wangui, akiwa amempakata anamnyesha maziwa. Ni mwkaa sasa umepita lakini bado maneno hayajanitoka kcihwani.
Picha ya mwisho kichwani kwangu, kumbukumbu ya mwisho ya Mama yangu kichwani kwangu ni ya mke wangu akiw aamempakata Mama yangu. Hata dada zangua mabao Mama likua anawapenda sana, anawasifia na kuwaona wamaana hawakuepo eneo la tukio kumhudumia kwakua tu mmoja alikua kazini, mwingine alinyimwa ruhusa na mume wake na mwingine alikua kasafiri kwakua Mama mkwe wake alikua naye anaumwa.
Leo mke wangu alikua ananishukuru kwa kumuambia aruhusu Mama yangu amnyanyase, nikakumbuka kuwa kuna watu wengi ambao wanashindwa kuchagua kati ya Mama na mke, ushauri wangu, hutakiwi kuchagua, kila mtu ana nafasi yake. Huwezi kumbadilisha Mama yako ila naamini kama ukiongea na Mke wako, ukampa moyo na ukamfundisha naman ya kushi na Mama yako basi utakua na ndoa yenye amani. Hutakiwi kuchagua kwani hakuna mwneye ubora zaidi ya mwenzke bali kila mmoja ana nafasi yake.
MWISHO
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU