-->

KUWA NA MSIMAMO, KATAA UTUMWA KATIKA NAFSI YAKO


NILIWAHI kumwambia binti mmoja hivi: “ Kama kasema hakuhitaji na katika nafsi yake kuna nafasi ya mtu mwingine, achana naye.” Hakukubali. Akasema hapana.
Akasema anampenda sana na moyo wake unamuhitaji kupita kima cha kawaida.
Na hivyo yuko tayari kutumia kila uwezo, kila mbinu na kila njia ili awe na huyo mwanamume kwa kuwa anampenda sana. Sikushangaa sana. Mapenzi ndivyo yalivyo.
Wakati mwingine mapenzi yakitamalaki katika moyo wako, hata hatari iliyo mbele yako huwezi kuiona. Ndivyo ilivyokuwa kwa huyu binti.
Maana mbali na muhusika kuonesha toka awali dalili za wazi za kutomuhitaji ila hakukubali.
Akaamua kupigania penzi lake kwa kila namna. Na baada ya miezi mitatu, akafanikiwa kuwa naye.
Ila baada ya miezi mitano mingine, akarudi tena kwangu na kusema hahitaji tena Mahusiano na yule jamaa.
Sikushangaa sana.
Maana Mahusiano ya namna hii nayajua vema kama kiganja changu.
Binti akasema mbali na kumpenda na kumjali kwa kila hali, jamaa hana anachothamini kwake.
Amekuwa jeuri, mkali bila sababu na wakati mwingine hata kumdharau yeye na familia yake.
Kwa tabia hiyo msichana wa watu akasema amenawa mikono.
Tangu siku ya kwanza niliyaona haya katika uhusiano aliouhitaji.
Kama mtu kakwambia hakuhitaji na zaidi anakuhakikishia kuwa yupo anayemgusa katika moyo wake na kuusisimua mwili wake, haina haja ya kuwa naye.
Mara zote nasema hakuna mapenzi ya upande mmoja yanayoweza kuleta maana.
Hata kama una upendo kama Malaika, ila kama hakupendi basi hakuna mapenzi timilifu hapo.
Kuna raha katika uhusiano pale kila mmoja anapokuwa na hisia na mwenzake.
Pale kila mmoja anapomuona mwenzake katika uzani halisi wa mapenzi na furaha. Katika namna hii hata kama akiwa na tabia mbaya kiasi gani ila kama anakupenda anaweza kubadilishika na mkaishi katika maisha ya amani na furaha.
Tatizo ni moja hapa.
Wengi wanaamini mapenzi ni suala la kuoneana huruma au kulipana fadhila.
Japo fulani anaambiwa kuwa hapendwi ila hakubali na matokeo yake anahitaji kupata huruma kutoka kwa muhusika. Hii ni hatari sana.
Kitaalamu ni vema ukawa nje ya mahusiano kuliko kuwa na mtu ambaye yuko nawe eti tu kwa sababu anakuonea huruma.
Eti anakukubali kwa sababu akikukataa utakuwa mnyonge na rafiki zake watamuita katili. Hii ni zaidi ya hatari.
Hata kama kesho atakubali kuwa nawe.
Ila hakutokuwa na amani na furaha baina yenu. Kwani Mapenzi ya huruma hayaleti furaha.
Mapenzi ya hisia za dhati ndiyo huleta amani na raha katika maisha.
ITAENDELEA.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU