-->

Acha kujiumiza moyo wako kwa kujaribu kulazimisha mahusiano ambayo kimsingi hayawezi kuendelea.

Hauwezi ukamlazimisha mtu kukupenda hata siku moja, hauwezi ukamlazimisha mtu akujali! Huwezi ukamlazimisha mtu awe muaminifu katika mahusiano yenu kama kufanya usaliti ni hulka yake huwezi ibadili. Hauwezi ukamfanya mtu awe vile unavyotaka wewe awe.
Muda mwingine mtu unaemuhitaji sana ni yule ambaye ni bora zaidi kama hutokuwa nae. Inabidi ujaribu kuelewa tu kwamba mambo mengine yamepangwa yatokee. Mambo mengine huja katika maisha yako lakini si kwa madhumuni ya kukaa na kudumu. Usijihangaishe kwa kujaribu kufix kile ambacho kilipangwa kivunjike tu.
Hauwezi kupata uhusiano wenye afya kwa mtu unaemuhitaji ambaye yeye binafsi hawezi kufanya hivyo. Iko hivi, kama ukiwa mvumilivu ku move on na maisha yako utakuja kuelewa kwanini ilikuwa hivyo, na huenda ukajiona ulikua mpumbavu kupoteza muda kwa mtu asie kujali hata chembe.
NIAMINI MIMI! Usiwekeze furaha yako kwa mtu ambae kimsingi hawezi kuitunza furaha yako. Kurasa nyingine hutakiwa kufungwa na maisha lazima yaendelee.
Image may contain: 3 people, text that says "STAR BWOY"
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU