-->

WAKATI UNAVUMILIA HEMBU TAFUTA NA KAKAZI KAKUFANYA

UTAMUZAIDIAPP
Wakati mwingine mpaka basi, mtu kakuoa ulikua na biashara yako, kakupenda na elimu yako kwa maana kua utaajiriwa na utafanya kazi. Umeenda kwake kakudanganya danganya na wewe na uvivu wako umekubali kuacha kazi.
Haya mambo yanenda kidogokidogo, mwanzo alikua anakuheshimu lakini baada ya muda anaona umekua mzigo, anaona kumbe ile kazi sio tu ilikua inakusaidia kununua vinguo vyako lakini pia ilikua inaomoesha na wadogo zako hivyo ni jukumu lake sasa si hataki ufanye kazi.
Anakasirika ananza kukunyanyasa kua kula kulala, sijui ndugu zako wanamsumbu eti anajiona kama vile ameoa familia nzima. Bado hujiongezi anaamua kuchepuka kabisa, tena kwa dharau anakuonyesha anaipa simu michepuko yake ikutukane.
Nawewe usivyojielewa umeamua kuvumilia ukisema Mungu atalipiza, haya hapo poteli ya mbali. Lakini badala uamkie sasa uanze kutafuta kazi unaendelea kulala kwa kisingizio eti hataki nifanye kazi. Pumbavu! Mnatia hasira, mbona wewe hutaki achepuke lakini bado anachepuka.
Sasa haisishii hapo anakutelekeza na watoto ndiyo unaanza kulia, kwenda kusumbua ndugu ambao nao wana matatizo yao, unaenda kwenu kumbwagia Mama yako watoto au kwa Kaka yako kwenda kuharibu ndoa yake kwa kugombana na wifi yako.
Dada yangu acha ujinga, kama mumeo anachepuka na hataki ufanye kazi, muambie Baba nakupenda ila najua kama umefikia hatua unachepuka ipo siku utanitelekeza hivyo sitaki kuadhirika, muambie hata mimi sipendi uchepuke lakini ndiyo hivyo, sina namna navumilia na wewe vumilia nifanye kazi.
Sasa wewe endelea kubembelezea ndoa hapo na kulialia utalia vizuri siku akikutelekeza kabisa. Mwanaume anapochepuka anakua amepoteza haki ya kukupangia kua usifanye kazi au la, ingawa hata hiyo hakuwa nayo huko nyuma ila kama una akili umnielewa kuwa kama ameweza kuchepuka basi anaweza pia na kukutelekeza.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU