Shida moja ya wanawake iko hivi, kila wakati wanakua Mama tu. Mama wote wana tabia moja, akikuambia kitu ni kwamba ni lazima ufanye, yaani Mama yako akiamka asubuhi akikuambia utaenda shule basi jua utaenda uwe umeumwa au umekufa basi utaenda, akikuambia ni kulala basi utalala, iwe una usingizi au huna utalala na kukoroma utakoroma.
Sasa wanawake wanataka wawe hivyo kwa waume zao, mwanaume ni mlevi kweli, popmbe ni mbaya, labda nakunywa mpaka kujikojolea ni aibu! Lakini huyo bado ni mwanaume, mtu mzima na wewe si Mama yake huwezi kumpangia, utamshauri, utamuelewasha na utaongea ila utaongea mara mbili tu baada ya hapo unaanza kuboa na unakua na kisirani, hata kusikiliza hata nkama unaongea kitu cha maana atakuona wewe kisirani tu.
Najua mnadhani kelele zinasaidia, kuna wakati mnajiambia hawa wanaume ukiwakalia kimya wanaharibikiwa, dada anayeharibikiwa kwa ukimya ni mtotyo, mtu umekutana naye, miaka 30, kakua mpaka kashaota mbelewele unasem aeti ataharibika, aharibike mara mbili! Naomba nikuulize tangu uanze kuongea aache pombe, umalaya, ajali familia, ajenge umjepata faida gani zaidi ya kisirani?
Dada yangu ukijua kuishi na mwanaume utamuendesha unavyotaka na atakusikiliza. Soma kitabu changu, lakini usisome kwa mchecheto wa kumbadilisha mwanaume itakula kwako, soma kwa mchecheto wa wewe kubadilika utaona hata yeye atabadilika.