MPENI USHAURI JAMANI MAJI YAMEMFIKA SHINGONI JAMANI SIJUI SISI WANAUME TUNAKWAMA WAPI ILA MUNGU TU ATUSAMEHE KWAKWELI👏👏👆
➡ Kaka Immanuel Catylyn Platnumz Kabla hata sijamaliza kufungua mlango vizuri,aliusukuma na teke hakujali kama naweza kuumia,alivyoingia ndani nilimsogelea kwania ya kutaka kumuuliza kulikoni mume wangu 😘😘 ,kabla hata sijazungumza chochote alininasa vibao mashavuni na kunipiga mateke kama kawaida yake akidai nyumba ni yake namsimamisha mlangoni ucku huu saa nane utafikiri yeye ni mlinzi??
➡Nililia kwa sauti ya chini sikutaka kuwaamsha watoto wangu wawili ambao kila siku usiku wamekuwa wakilia kwa ajili yangu pindi baba yao akirudi usiku,alivyoona siliii alinifuata na kuanza kunipigiza ukutani akidai ninakibuli saana😢😢😢,inaniuma sana,Huyo anaenifanyia hivyo ni mume wangu wa ndoa kabisa tuliefunganae ndoa miaka mitatu iliyopita,amekuwa akinitesa sana kuna wakati nilitamani nimwagie maji ya moto au nimweekee sumu kwenye chakula afee lakini ninavyowaangalia wanangu machozi yananitoka naona nitaishia jera na watoto wangu watateseka saana.
➡Nilivumilia yote kwa ajili ya wanangu lakini yote tisa kumi Jana alichonifanyia sijaamini macho yangu niliona kama naota vile kaka imma ,Amekuja na mwanamke mwingine,ananiambia Mimi nikalale na watoto kule tunakotunzia chakula(stoo)
➡Alivyoona nakaidi akatoa mkanda na kuanza kunichapa mbele ya mwanamke wake,hakuona haitoshii ameamua kunifukuza nyumbani kwake usiku huo na wanangu tuliozaa pamoja tena nidamu Yake kabisa😐😐
➡Inaniuma sana sielewi nifanye nini jamani naombeni ushauri wenu huenda nikapona maumivu niliyonayo jamani,msituone tuko kweny ndoa mkadhani tuna raha,jamani tunapitia Mapito mazito mno,wanawake wenzangu hawa wanaume jamani wanatesa saana mimi najuta kuolewa kabisa,Naombeni ushauri weni nimechoka mwenzenu usoo umejaa ngumi tu na mijeredi ya mkanda kama Niko punda.