Kila siku unalalamika mume wangu hafanyi mambo ya maendeleo wewe unafanya nini? Unajua kuna kitu wanawake wamejijengea kuwa kitu kama kujenga, kufungua Biashara na kuwekeza kwingine ni mambo ya wanaume, hata kama wanataka kufanya basi wanataka kufanya na wanaume. Ni kweli ni raha kufanya na mwanaume wako hasa kama ni mume wako, lakini ni upuuzi, narudia ni upuuzi kuacha kufanya kwakua eti mwanaume hafanyi!
Umeshajua kuwa mwanaume wako yeye pesa yake inaishia kwenye pombe, lakini badala useme sitabeba majukumu ya kuhudumia familia natakiwa mimi nijenge niwe na chakwangu wewe kutwa kucha kuhangaika naye, kulalamika naye, mwingine anamsukuma mwanaume kununua na kujenga katika kiwanja chenye jina la mwanaume, wakati yeye mwenyewe anaweza kununua kiwanja na kujenga kwake. Ishsu sio kwamba hata mkiachana mgawane hapana ishu nikuwa kama kitu una umiliki nacho ni chako hawezi hata kuuza au kuhongea.
Ndoa za sasa hivi ni tofauti na zazamani, mwanaume siku hizi anaweza kukukimbia na kukutelekezea familia, sasa kama unaona mtu anaishia baa, mtu anapenda ndugu zake pesa zote anapelekea ndugu zake ila bado unajitia kiherehere kujenga kwenye kiwanja chenye jina lake, unamuambia hata muandike majina yenu wawili hataki wewe kiherehere unajenga hivyo hivyo unategemea nini? Iko hivi kama yeye hataki kufanya mambo ya maendeleo na pesa zake basi hazikuhusu ni zake hembu zako chukua fanya maendeleo, jenga nyumba uone kama itabomoka.