Najau wakati mwingine inaboa, unakaa dukani kwako tangu asubuhi mpaka jioni hakuna mteja hata mmoja, unaboreka kukaa mwenyewe unatamani kutoka kwenda kupiga stori. Lakini moja ya vitu ambavyo vinaboa zaidi ni kuingia dukani na kukuta hakuna muuzaji mpaka akawe wa kuitwa. Kuna wateja wengi sana ambao wanapita bila kuingia dukani kwako kwakua hawaoni muuzaji.
Labda niwaambie kitu kimoja, tabia za wanunuzi wengi ni kuchungulia, kwamba watu wengi hawaondoki nyumbani kwenda dukani kununua kitu. Mara nyingi mtu anapita, anaona kitu kizuri ndiyo ananunua, yaani watu wananunua baada ya kuona na si kupanga kununua. Sasa kama mtu anapita dukani kwako, hana mpango wa kununua kitu, atachungulia.
Kama upo basi atajipirisha kuchagua na hata kujaribu kisha anunue, lakini kama haupo basi atapita. Unajua ni kwanini, hatataka kukuita kwakua hana mpango wa kununua, watu watakaoingia kwenye duka ambalo halina muuzaji ni wale tu ambao wana mpango wa kununua, ambao ni wachache, ni kamaasilimia 10 tu ya wanunuzi wote.
Wale wakupita wakiona hakuna mtu, wanaona aibu kumuita muuzaji huko alipo wakati hawana mpango wa kununua. Ndiyo maana unaona kuwa mtu anapita, anapiga jicho tu haingii, lakini kama upo ataingia. Jambo la pili ni hivi, ukiwa upo dukani kwako, mtu akipita na kupiga jicho utamkaribisha ataona aibu ataingia, lakini umekaa mita mia kule unapiga stori, mtu anakuja, unamuona unaumbia karibu unakuja unakimbia inamkata stimu.
Jambo jingine ni hivi, watu wengi hununua wtau na si vitu, anaingia dukani anona mdada mzuri ili amuangalie vizuri inabidi achague nguo, wakati anachagua anajiongelesha ananunua. Mdaa kapita kaona mdada mwenzake kavaa wigi, aua anamuona mzuri anataka kumthaminisha, kapenda nguo yake, kapenda viatu vyake, ameona mkaka anavutia, anaingia kumthaminisha anajikuta anaangalia na vitu ananunua.
Mwisho ni hivi, inaboa sana kuifika dukani kwa mtu ukute anmetoka. Ushawahi kufika Benki, uko kwenye foleni ndefu unakuta kibao kuwa ametoka unasubiri, aisee inaboa, ndiyo hivyo hivyo kwenye hizi Biashara. Hakuna wateja ila kaa dukani kwako, piga umbea kwa kudokoa dokoa au acha kabisa. Kama una mfanyakazi kila siku ni umbea, ukifika dukani humuoni, mara ya kwanza muambie, ya pili mkate msahahara na ya tatu tafuta mwingine.
TITO