-->

WANAWAKE HEBU ZITAMBUE SABABU ZA MUME KUTOKA NJE YA NDOA


1.KUTHAMINIWA
Kutokana na ugumu wa maisha ya kazi,malezi nakadhalika Wanaume wengi huhitaji maliwazo na msaada wa kuonekana kukubaliwa na kupongezwa kwa zile jitihada anazofanya za kupambana na maisha sasa kama jitihada hizo anazofanya Mkewe hataziona na kuzithamini, basi Mwanume huyo yupo tayari kutafuta kuungwa mkono na kusifiwa na kuliwazwa kutoka nyumba ndogo
2.TENDO LA NDOA
• Kama Mwanaume hapati tendo la ndoa kwa ufasaha,kwa mahitaji yake kwa kadri ya kiu yake kukatwa,tendo la ndoa likiwa ni lilelile halina mabadiliko na pia kupewa kwa masharti
• Mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa hajisikii raha ya tendo hana msisimko wa tendo,kiasi Mume akiingia anaona kama kaingia kwa Mume mwenzie Mke yupo baridi hapo napo Mwanaume hutoka nje ya ndoa kwa kutafuta bashasha, mzuka wa tendo ili ajione na yeye ni kidume na anachokifanya kinakubalika ana mkuna mtu kwani ndio asili yake
3.MGUSO WA UPENDO
• Mwanaume anatoka nje pia kwa sababu Mke wake hampi upendo wa kutosha hamjali kuanzia chakula, mavazi, maliwazo bashasha uangalizi wa kina kama anaopata mwanae na hapo ndipo hufikiria kupata matunzo hayo nje kwa nyumba ndogo ili ajisikie vizuri
4.MVUTO
• Sababu nyingine inayomfanya Mume kutoka nje ya ndoa ni Mwanamke anapopoteza umbo lake,urembo wake wa awali ambao Mume alimuona nao mwanzoni kabisa na hapa Mwanamke asipokuwa makini kujitunza kujiweka mwenye mvuto Mume anaweza kutafuta mvuto nje kwani ndio mzuka wake ulipolalia huko
5.KISASI
• Wanaume wengine hutoka nje tu kwa sababu wao walishaumizwa na Wake zao huko nyuma sasa njia pekee ya yeye kujiondelea tatizo lake kichwani huona ni bora kutoka nje kwani hujisikia raha na ahueni kila anapotoka nje kwa kuwa kachukulia kuwa Wanawake wote ni wale wale hamwamini tena Mwanamke japo anamuhitaji hivyo furaha yake yeye ni kubadili tu
6.KUPUNGUA AU KUKOSEKANA KWA MAPENZI
• Pia Mume hutoka nje ya ndoa endapo mapenzi yatakwisha au kupungua kwa Mkewe, kwa kuwa tayari ana watoto na majukumu mengine ya kifamilia ikiwemo mkataba wa kuishi hadi kifo kiwatenganishe njia pekee ambayo humletea faraja ni kuwa na nyumba ndogo na huendelea kubadili Wanawake mpaka pale atakapopa tulizo la moyo wake la dhati akaridhika ndipo hutulia hapo huku akiwa ndani ya ndoa yake kutimiza wajibu tu wa kimalezi na kisheria
• Kulazimishwa kumuoa Mwanamke asiyempenda
7.TAMAA YA MWILI NA MALI
• kundi la Wanaume ambao kwao hawaridhiki na Mke mmoja wao ni kawaida kwao kuwa na Wanawake wengi kwa kuwa uwezo anao wa kifedha na hupenda kujaribu jaribu inakuwa ni hulka yake tu na anaona fahari kumvua chupi kila Mwanamke bila kujali kama ni Mke wa mtu,mwanafunzi,changudoa au la
• Kutoka na mwanamke mwenye uwezo wa kifedha ili mradi apate fedha na kukidhi mahitaji yake na familia yake huku akijua kuwa hampendi huyo mwenye fedha bali ana mpenda Mkewe tabia hizi mara nyingi hutokana na malezi na makuzi ya muhusika
8.USHAURI MBAYA
• Mara nyingi pia huwa ni sababu ya Mume kutoka nje
• Mashoga
• Makungwi… mila na desturi
• Kurithi tabia za wazazi wake
• Vyombo vya habari,,cinema,majarida,vipindi vya Radio na TV
• Makundi ya Kijamii…mijadala mbali mbali
• Ushirikina
• Elimu ndogo ya Kiimani
#ZINGATIO
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏 MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA (ADHABU WAEBRANIA 13:4)
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU