-->

VIGEZO 5 MUHIMU ZAIDI VYA KUZINGATIA KAMA ANAFAA KUWA MKE AU MUME WA NDOA MAISHA

SIFA ZA MWANAUME/MWANAMKE ANAYEFAA KUWA MUME/ MKE WA NDOA WA MAISHA πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄
VIGEZO 5 MUHIMU ZAIDI VYA KUZINGATIA KAMA ANAFAA KUWA MKE AU MUME WA NDOA MAISHA
πŸ’ŸWanaume huwa wanaangalia Zaidi vigezo vya nje (external/physical factors) ambacho ni kitu kizuri sana na ndio ukweli ili umpende Mwanamke yeyote lazima uwe umemuelewa sura yake maana andio kitu kinachoonekana .
πŸ’ŸLakini sasa nakuambia kigezo cha kukufanya umpende Mtu Mke ni tofauti na kigezo cha kukufanya Umuoe Mtu Mke. Hapa sitajadili sana kuhusu sura ,umbo, macho au kigezo kingine cha nje , Mimi nitaongelea vigezo 5 vifuatavyo vya baada ya hapo vitavyofanya uone anafaa kuoa au kuolewa naye baada ya kuwa nae kama mchumba.
❤️ MCHA MUNGU-----Lazima Mwanamke unayedhamiria kumuoa awe ni Mcha MUNGU sio mpagani au mwenye kuamini Imani za kishirikina potofu , na ni vema mkiwa wote Mwa Mcha MUNGU pamoja na yaani muwe kweli mwasali.
πŸ’ŸMwanamke ambae hamuheshimu MUNGU anaweza kuwa na Imani nyingi na wakati yatapotokea majaribu kwako yeye atawaza kwa waganga tu tofauti na Mke mwema kimbilio lake ni MUNGU , atawaza kukuombea au kupata ushauri kwa wenzake wa Mchao MUNGU na pia ikumbukwe kwenye makusanyiko ya ibada kuna mafundisho ya ndoa huwa Wanawake wanayapokea nyakati zote hivyo Mwanamke Mcha MUNGU ni kito kwako maana unakuwa salama wewe na familia yako na hata nduguzo.
❤️ KAZI, MALENGO NA MTAZAMO MPANA KIUCHUMI NA KIMAISHA: Mwanamke ambae hana kazi nabado mtazamo wake kimaisha na kiuchumi bado hauonekani kuwa anajitambua basi hakufai.
πŸ’ŸLazima Mwanamke awe na kazi , au awe na mtazamo Fulani kimaisha na kiuchumi ambao ukimskiliza unaona kuwa mnaweza kufika mbali , asiwe Mwanamke wa kukutegemea kwa kila kitu hata mawazo ya kukuchangia hana,
πŸ’ŸMwanamke ambae hana kazi lakini ana bidii ya kufanya chochopte kusaidia kuingiza kipato au hata anaweza kutoa ushauri chanya kiuchumi na ukapima ukaona kwamba ana mawazo chanya huyo anafaa, hapa sio lazima awe amesoma bali awe ana bidii katika kazi na ana mawazo ya kukuinua kiuchumi.
❤️ MATUMIZI: Mwanamke mwenye matumizi rough ya juu asiejali fedha na budget hakufai kabisa tangu katika uchumba utajua tu aina ya Mwanamke kama anajua budget ya fedha na anajua matumizi sahihi ya fedha. Usipuuze maana maendeleo ni budget kama atakuwa hana budget nakuambia ukweli hata kama mshahara wako mkubwa bado utajikuta hakuna maendeleo ya maana unafanya katika maisha,
❤️ANAEPATANA NA NDUGUZO NA NDUGUZE : Mwnamke anaeiva na ndugu zako atafanya ndoa yako idumu sana na pia ni uhakika hata lolote likitokea uhakika kulitatua tofauti na asieshirikiana na ndugu zako yani asiyepatana nao . ogopa sana Mwanamke ambae ana bifu na baadhi ya ndugu zako hakufai tena. Maana utagombana na hao ndugu mara nyingi mchohcezi wa ugomvi huo atakuwa ni yeye. Atataka uchukiane na mawifi zake , mashemeji nk.
❤️ANAEKUSIKILIZA NA KUKUTII: Mwanamke unaweza kumkuta akiwa na tabia mbaya , pengine bar , pengine akiwa anadangadanga tu hovyo na matabia ya hovyo ya uzururaji, uvaaji wa hovyo nk .Lakini kama anakuskiliza anaacha kudangadanga, anaacha kuvaa hovyo anaacha ulevi anaacha umalaya na uzururaji na anaamua kwamba atulie na aolewe.
πŸ’ŸKama Mwanamke anakusikiliza tangu mwanzo mkiwa wachumba kuna mambo hupendi unamuambia na anakubali anaacha kabisa basi huyo anafaa , lakini kama utamtaka aache mambo Fulani ambayo hujapendezwa nayo kisha hakutii basi hakufai tena maana baada ya kuolewa jeuri na kujiamini huwa inaongezeka na hapo ni atakusumbua Zaidi.
πŸ‘‚ KWA WANAWAKE: Vigezo ndio hivyo hivyo nimetumia kama mfano lakini wewe zingatia hivyo vigezo utagundua nawe unatakiwa upate Mwanaume mwenye sifa hizo, kwa kifupi sifa hizo ni kwa wote.πŸ™
πŸ™HITIMISHO :Hapa Mwanaume unatakiwa kuwa makini ili kuweza kujua namna ya kuzipima sifa hizi na kujua kama Mchumba wako anazo.
Na , kwa Mwanamke kama huna anza kujisogeza kuja kwenye sifa hizi ama sivyo utaachika mapema kuliko unavyodhani.
πŸ™Na kwa Wanaume hakikisha ana sifa tajwa hapa juu wakati pia umeshaona ana sifa zako nyingine zile physical mnazotumiaga za macho ya nini sijui, kiuno kama nini , sijui kalio gani , sijui kifua kitamu, sijui ngozi laini mara sijui blackbeauty au cheupe nk.
πŸ™OMBI ikiwa kwa namna moja au nyingine kuna kitu umejifunza hapa basi weka comment maoni hapa chini niambie nini umeelewa , na pia amabcho hujaelewa unaweza kuuliza nikafafanua Zaidi , ambacho una mashaka weka comment uliza utafafanuliwa na MUHIMU kama kuna kitu unajua Zaidi kinaweza wasaidia Wanaume wanaotaka kuingia kwenye ndoa maana Wanaume wote lazima mwisho waoe na pia Wanawake waolewe , weka comment ya chochote ambacho unadhani kitasaidia wengine wajifunze naamini utabarikiwa pia.
πŸ’ŸKARIBU SANAπŸ™πŸ™πŸ™
πŸ”΄ UCHUMBA SIO NDOA πŸ’ͺ
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU