-->

HUWEZI KUPATA TABASAMU KWA KUMUOMBA USHAURI MTU AMBAYE MOYO WAKE UNALIA!


Mara nyingi sana matatizo ya wanawake wengi hayatatuliwi kutokana na aina ya watu ambao huwaomba ushauri. Tuchukulie una mume mlevi, mzinzi na huna furaha katika ndoa yako, kakuambia uache kazi hivyo kila siku ni kulia. Unaenda kumuomba ushauri rafiki yako, yeye hana mume lakini ana Boyfriend ambaye ukiangalia tabia zake ni bora mume wako mara mia.
Rafiki yako huyu anavumilia mateso akitegemea ndoa, nayeye kama wewe bado ana imani kua ipo siku mtu wake atabadilika na hata ataolewa. Sasa akifikiria akuambie achana na huyo mtu anaona kama wewe ukishidnwa ndoa yeye hataolewa kabisa hivyo ili kupata mwenza, kupata mtu wa kuvumilia naye na ili kujipa matumaini katika hali yake basi anakuambia “Vumilia wanaume wote ndiyo walivyo” anakuambia matatizo yake mnafarijiana.
Anakuambia ndiyo walivyo kwani hata wake yuko hivyo. Lakini unavumilia na baada ya muda unachoka, unaamua kwenda kumuomba ushauri Mama mkwe wako, huyu yeye alikua anamfahamu mtoto wake tangu akiwa mdogo, anajua matatizo yake na kama Mama anataka mwanae awe na familia imara, aache ujinga wake na asiwe ni mtu wa kuoa na kuacha.
Anajua tabia za mwanae na anajua ni wanawake wachache sana wanaweza kumvumilia hivyo anajifanya kua yuko upande wako anakusihi vumilia mambo yatakua sawa. Unavumilia tena na baada ya muda unachoka, maji yamekufika shingoni vipigo vinazidi, unaamua kwenda kuongea na Mama yako mzazi. Unamuelezea shida zako lakini unavyoongea ni kama unamzungumzia Baba yako.
Kumbe nawewe yule Baba uliyekua unampenda, unamuona shujaa alikua anampiga Mama yako kila siku, Mama alivumilia na kuwalea kwakua alikua hana kazi, kwakua alikua hana pakwenda sasa ingawa hata sasa hana furaha lakini anaona anawajibu wa kukuambia vumilia. Huna namna unarudi nyumbani unavumilia ukidhani kua kwa kunyenyekea na kulia kila siku labda mume wako atabadilika!
Unaamini ndiyo ndoa zote zilivyo na ndiyo maisha yalivyo. Unashindwa kukumbuka kitu kimoja kuwa mambo yote ambayo mumeo anakufanyia si mambo ya bahati mbaya wala ugonjwa, hapana ni mambo ya makusudi na unaweza kuyabadilisha. Sikuambii uondoke lakini sikuambii pia uvumilie, nilazima ujifunze kutafuta furaha yako, kutafuta furaha ambayo haitokani na mwanaume.
Yaani maisha yako yasitegemee mwanaume atasemaje au atafanya nini? Uwe na mipaka ya vitu vya kuvumilia na vile vya kutovumilia. Kwamba mwanaume anapokutukana na kukuambia mjinga basi usiumie, anapokuambia Malaya isikuumize kichwa. Uweze kujitengenezea furaha yako mpaka huyo mwanaume aone ni ujinga kukunyanyasa wakati huumii na anajiumiza yeye mwenyewe.
Si jambo la siku moja hivyo hata kama tayari ushanunua Kitabu changu basi usikae tu na kudhani kwa kukisoma mambo yatabaidlika. Hembu changua mambo ambayo yanakuhusu na anza kuyafanyia kazi mpoja moja na kama hutaelewa basi nipigie niulize maswali mengi iwezekanavyo. Acha kua wale watu wa kusema wanaume wote ndiyo walivyo kana kwamba umetembea hata na nusu ya wanaume hapo Kijijini kwenu.
Kwa wale ambao hamjapata Kitabu changu basi ni shilingi elfu kumi na unasoma kupitia Simu yako, hapa Facebook au kwa Computer yako. Hembu anza hatua ya kwanza ya kusema kua silii tena ya kukata mnyororo wa mateso. Kukipata unalipia Shilingi elfu kumi tu kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa no. 0657-552-222 ukishalipia ni Text 0742-381-155 kusema unataka kutumiwa Kitabu kwa njia gani.
IDD MAKENGO
KAMA POST HII IMEKUBARIKI BASI #SHARE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU