-->

WIVU NI NINI KWENYE MAPENZI?

Image may contain: 1 person, close-up
Wivu una matawi makuu mawili;
MAUMIVU YA NAFSI KWA JAMBO KUTOKA KWENYE UHALISIA AMA UKWELI NA KUWA KINYUME.
MAUMIVU YA MOYO BAADA YA KUGUNDUWA MWENZA WAKO ANASHIRIKI KI MAPENZI AMA MAWASILIANO YA MAPENZI NA MTU MWINGINE.
Huo au hayo ndo yanayoipa DUNIA YA MAPENZI KUZUNGURUKA🌏🌍🌎
Nikiri kwamba MAPENZI YAKIKOSA UAMINIFU NAYO YAMEKUFA hata kama wahusika watakuwa na sababu zao za kulilinda penzi hilo lisife but LITAKUWA LIMEKUFA🤣
Upendo ni kama YAI🥚 Kwamba kama halijabebwa vizuri na kwa uangalizi mzuri haliwezi kuwa salama, MOYO wenye kumpenda mtu kwa hakika UNAHITAJI UKWELI WENYE MATENDO kuliko ukweli wenye maneno, Ni rahisi sana kumkamata mtu ki FIKRA lakini pia ni rahisi sana kumpoteza mtu huyo😭
Sababu ziko nyingi ila kwa ujumbe huu nitatoa moja;
Uonapo mtu anakuelewa haraka ujue ANAKUAMINI hivyo jiepushe kumdanganya mtu mwenye IMANI NAWE! Maana alivyokuelewa kwa uongo ndivyo ambavyo ATAKUELEWA KWAMBA WEWE HUFAI KUWA NAE.
Ni bora ukweli mchungu ulio mwanzoni mwa tatizo kuliko Maneno yenye kupoza hasira mwisho wake ni KULUNDIKA MAKOSA na hapo ndipo maswali na majibu baina ya MOYO NA AKILI hukinzana hata kupelekea KUBOMOA MISINGI ULIYOJENGA KWA MWENZA WAKO! Usione WATU KUTENDEANA UBAYA UKADHANI NI KITU CHA BAHATI MBAYA mara nyingi sumu ya MAPENZI hutokana na migogoro isokwisha, Ubaya unajengwa ama kutengenezwa na UBAYA na hapo ndipo utakuja kuona WALIOPENDANA SANA WAMEKUWA WAHASAMA😭
Kujenga penzi ni gharama ya vingi, Lakini linaloumiza MOYO NA NAFSI ni pale MTU ANAPOKUWA AMEUTOA MUDA WAKE WOTE KWA MWENZA WAKE na baadaye akagundua kwamba alikuwepo kwa mpito😭😭
Ni kweli kabisa MTU HUDANGANYA BAADA YA KUONA ANAO UHITAJI LAKINI NYUMA YAKE KUNA SIRI AMBAYO IKIWEKWA WAZI HAWEZI KUKUBALIWA HITAJI LAKE lakini ni bora kukomea KUPENDA na usiumize ila uumie wewe, Maana ukidanganya ili UPATE na baadaye uje kugundulika kwamba ulidanganya UTAKUWA HATARI KWAKO lakini pia unaweza kuja kuumia zaidi kuliko kama usingeingia kwenye penzi kwa UONGO
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU