-->

UPO WAKATI UKIMTAFAKARI BIN ADAM HUWEZI KUPATA MAJIBU JUU YA MAHITAJI YAKE KWENYE MAPENZI!

Image may contain: 2 people, people sitting and indoor
Mahitaji Muhimu ya Mtu yanatajwa kwa wingi, Mtu anaweza kuwa na mahitaji kumi lakini mtu aliye nae akafanikiwa kuyabeba mahitaji tisa ya mpenzi wake, Kwenye yale mahitaji muhimu ya Mtu likipelea hitaji moja anakuwa bado hajawa na hakika na mahali alipo, Kinachonifanya nimshangae Bin Adam ni pale anapokuwa anatafuta mtu wa kujazia "BASIC NEED" Pengine kilichopelea kujaza mahitaji yake ni kimoja tu, ila anasahau kuwa yule aliyefikia mahitaji tisa anamuona hana maana tena kwa kukosa hilo hitaji lake moja, Hapo ndipo unabaini Mwalimu wa hesabu katika MAPENZI alifundisha hesabu kwa lugha ya kiarabu maana yake mbele nyuma na nyuma mbele... Yaani ajabu ni pale Mtu anaposhindwa kuyabeba madhaifu ya mwenza wake kwa kukosa hilo hitaji lake moja wakati ameweza kufanya mahitaji tisa, Huyo mwenye hitaji moja hawezi hata kufikia mahitaji matatu ila ndiye ataonekana kuwa wa maana kwa sababu tayari MOYO WA MTU HUYO UMETIMIZA HAJA ZAKE na itambidi asimame na watu wawili kwa kutetea MAHITAJI YAKE! Wahenga na misemo yao ndo humfanya mtu kuishi kwa mateso pale linapotajwa neno la "MTAKA NYINGI NASABA HUPATA MWINGI MSIBA" kumkosa wa tisa itakuwa rahisi zaidi pindi akiishajua kila aliloweza kwa nafasi yake kumpa FURAHA NA AMANI mwenza wake lakini bado ni bure, Kumlinda wa moja kwake itakuwa hazina kwa kufikiri huyo ndiye mwenye thamani kubwa maana ameweza kujaza PACKAGE YAKE... Amaa kweli wajinga ndo waliwao, Ukose TISA ili kuilinda MOJA utakuwa na akili kweli? Inauma sana kumtimizia Mpenzi wako yale mahitaji mengi muhimu n then AKASHINDWA KURIDHIKA.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria ðŸ˜Ž
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU