-->

BILA MOYO WAKO KUWA HIVI HUWEZI KUENJOY MAPENZI HATA SIKU MOJA

Image may contain: one or more people, people standing and outdoor

Moyo ni kiungo kilichomo sirini, Hakina urafiki wala hakina ujilani bali maisha ya MOYO YANATEGEMEA FURAHA NA AMANI... Uwapo na penzi lililo na Furaha pamoja na Amani muda wote MOYO HUUNENEPESHA MWILI! Uchunguze MOYO wa mwenza wako kupitia uso wake, Maana MOYO ukiugua uso hukosa nuru na mwisho wake ni mtu kutawaliwa na upweke mwingi, Ukiona mwenza wako hayuko katika hali ya kawaida Mtoe eneo alilopo mtembeze mahala ambako ataona vitu vya tofauti, ihamishe akili ya Mwenza wako kutoka upweke hata Furaha ili uujenge moyo wake, Ushinde moyo wa mwenza wako kwa kubadili hali iliyokuwa inamtesa na kumpa sababu ya kujiona mpya tena! Mapenzi mazuri ni kuushinda moyo wa mwenza wako ili uweze kuwa na Amani, Muda mwingine tatizo linapotokea na kuumiza moyo ni vyema kuondoka eneo hilo japo kwa muda mchache na kuelekea hata linakozamia JUA ama kuliko na milima au Bahari/Ziwa akili ikafikiria hicho unachokitazama ili kusahau hicho kilicho kusababisha ukafika hapo... Mapenzi ya ukaribu ndiyo yanayoweza kuuponya MOYO wa mwenza wako, Ni fahari kuuponya MOYO wa mwenza wako kwani utapata DHAMANA NDANI YA MOYO WAKE! Ushindi wowote una kujituma, Jitume kwenye MAHUSIANO/NDOA yako ili utajwe kuwa unalo pendo la dhati, Kulitetea penzi lako ni USHUJAA! Maana kuudanganya MOYO ni ngumu ila unaweza kuutetea kwa kusimamia unalo liamini.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU