
USIMPE MTU NAFASI NDANI YA MOYO WAKO kabla hujajuwa anakuja kwako kwa mtazamo upi? Wako watu wao hupanga KUWA NA MAHUSIANO ILI KUONDOA STRESS kitu ambacho kwako kitakuangamiza moyo kwani wewe hutajuwa hilo na badala yake UTAJIACHIA UNYAYO HADI UTOSI kumbe unalambishwa mabaki ya uji, Usimpe mtu nafasi akaujuwa UDHAIFU wako, Wengi hutumia udhaifu wako kukuchapa na mwisho wake WEWE NI KUWA MHANGA WA PENZI LAKE... Simama katika msitari ujue kwamba MAPENZI yanaumiza sana lakini pia yanaharibu mtazamo wa ki fikra mwisho wa siku ni wewe kukosa FURAHA NA AMANI katika dunia hii, Mungu hakutuumba kwa mfano wake kwa bahati mbaya maana kama ni MAPENZI kila kiumbe hufurahia kwa namna yao, Kwani hujawahi ona MENDE WAKISHIRIKI KI MWILI?🐞
Kwanini sisi tunafurahia zaidi yao? Kwa sababu tulipewa upendeleo na ndo maana KWA KUTOKUJUWA KWETU MAANA YA UBIN ADAM WETU tumekuwa hatuhurumiani, Mpe MOYO WAKO mtu ambaye anajuwa kuwa WEWE NI MUHIMU KWAKE! Ukikosea ukampa MOYO wako mtu asiyejitambuwa wallah UNAWEZA KUOKOTA MAKOPO laaa uachwe na maradhi ambayo mpaka unakufa utakuwa unajuwa yeye ndiye chanzo, Yanini Mateso na dunia yenyewe ishakwisha hii tunailazimisha tuuu? Be strong enough 💪🏽
#Elista_kasema_ila_sio_she
