-->

UJUMBE WA LEO: HAYA NDIO MAMBO MAKUU YA KUEPUKA KIPINDI CHA UCHUMBA.

Image may contain: 1 person

Waswahili husema, "Mchumba hasomeshwi" wakiwa na maana kuwa uchumba sio ndoa maana yake hauna WAKFU au KIAPO RASMI cha kuishi pamoja milele bali una AHADI za kuoana ili kuja kuishi pamoja kama mke na mume iwapo kila mmoja akijiridhisha kwa tabia, mienendo, mvuto na hali ya mwenzie kisha kuamua kufanya maamuzi ya mwisho na ndipo NDOA ifungwe.

Ndoa ni ngumu kuvunjika maana tayari wawili mke na mume wameshakula KIAPO RASMI cha kuishi milele hadi kifo kiwatenganishe ndio maana tunasema wamekua "MWILI MMOJA" ila uchumba ni uhusiano ambao bado haujakamilika yaan unaeza vunjika saa yeyote iwapo mmojawapo kati ya binti au kijana hatojihisi kuridhika na alivyo mwenzie kitabia, kielimu, kifedha, kimapenzi, mvuto, hali au namna yeyote atayoona yaeza muwia kero maishani katika ndoa.

Wapo waliokaa katika uchumba miaka 10 ila mwishowe kila mmoja amejikuta akipata chaguo lake jipya tofauti tena ndani ya mda mfupi ndoa zikafungwa na watu wanaishi vizuri. Hapo ndipo tunapopata tafsiri kamili kuwa MAPENZI UPOFU maana utashangaa watu wanaahidiana katika uchumba zaidi ya miaka 10 ila mwishowe kila mtu anapata mwingine na kufunga ndoa NDOTO YAO ya kuoana inabaki kuwa story.

Ni vema baadhi ya mambo mkasubiri hadi muingie rasmi katika ndoa maana katika uchumba bado kila mmoja yupo njiapanda katika kufanya tathmini ya uhakika kujiridhisha ili aamue maamuzi ya mwisho yatayopelekea ndoa. Usijifariji kwa mapenzi na upendo anaokuonesha mchumba wako ukamfanyia yapaswayo kumfanyia mmeo au mkeo UTAJAJUTA BURE pale ambapo usipotarajia ushangae kabadili msimamo ghafla na kuoa au kuolewa na mtu mwingine.

Haya ni baadhi ya mambo mnayopaswa kuyaepuka kipindi cha uchumba, myafanye ndani ya ndoa tu MKISHAOANA:

.
1. Msichange na kununua gari lenu mkiwa wachumba
2. Msichange na kununua shamba, kiwanja au nyumba yenu mkiwa wachumba.
3. Msianzishe biashara ya pamoja mkiwa wachumba.
4. Msikopeshane kiwango kikubwa cha pesa mkiwa wachumba.
5. Msishirikiane kukopa kiwango kikubwa Bank au kwenye taasisi za fedha mkiwa wachumba.
6. Haishauriwi kabisa kwa watu ambao ni wachumba kushirikiana kifedh na mipango iliyotajwa hapo juu wakati wakiwa ni wachumba. Mambo hayo hapo juu yanapaswa yafanywe na watu ambao tayari ni wanandoa.
7. Uchumba sio ndoa, hauna "garantee" wala hauna mashiko. Unaweza kuvunjika dakika yoyote ile na kama mlikuwa mmesha wekeza kila mmoja kwa mwenzake kwa kuamini kwamba si mtakuja kuoana, uzoefu unaonyesha kwamba mara nyingi mmoja kati ya wachumba hao ambaye mali ilikuwa imeandikishwa kwa jina lake huishia na mali ile na kumdhurumu mwenzake bila kujali kwamba mali hizo walikuwa wamechanga wote

8. Msizae watoto kipindi cha uchumba. Siku hizi imekua kawaida kukuta watu tayari wana watoto hadi 6 alafu wanakwambia ni wachumba tu bado hawajaoana.

Hahahahahaaaaaa duh haya bhana mi simo.

Nasisitiza msishirikiane kuchangiana fedha kununua kiwanja au kujenga nyumba mkiwa wachumba.

Wapo walioamua kujinyonga au kunywa sumu baada ya uchumba kuvunjika hivyo CHUKUA TAHADHARI.

Imepenya..... Haijapenyaaaaa????!!!

Kama imepenya comment jambo lolote lingine nililolisahau ili watu waje kulisoma pia katika comment yako.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU